Saturday, January 31, 2015

SIMBA YASHINDA BAO 2- 1 DHIDI YA JKT RUVU TAIFA

Kikosi cha timu ya Simba SCkilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa taifa na kushinda bao 2-1.
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kilichoanza leo.
Makapteni wakisalimiana na marefa kabla ya mechi.
Mashabiki wa Simba wakishangilia.
Wachezaji wa Simba wakiwasalimia mashabiki baada ya mechi.
Timu ya Simba SC, imeshinda bao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu leo Uwanja wa Taifa, Dar. Sasa ina pointi 16.
Mfungaji kwa upande wa Simba ni Danny Sserunkuma kipindi cha kwanza na kipindi cha pili.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)


YANGA: PLUIJM ANA MAISHA MAREFU JANGWANI

Pluijm

Uongozi wa klabu ya Yanga, umesema unaamini kocha wake, Hans van Der Pluijm ana nafasi kubwa ya kuwa klabuni hapo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na falsafa inayoendana na sekretarieti iliyopo madarakani kwa sasa.
Pluijm anatajwa kuwa kocha bora wa Jangwani katika misimu ya hivi karibuni, kutokana na mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi alichokaa na timu msimu uliopita na uongozi unaamini atafanya mambo makubwa kutokana na mtazamano wake, lakini wakatoa angalizo kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na kumuacha kocha afanye kazi yake.
Akizungumzia kasumba ya timuatimua ya makocha, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha alisema uongozi umetokea kumuamini Pluijm kutokana na mawazo chanya aliyonayo katika maendeleo ya soka klabuni hapo na kuamini anaweza kuwa nao kwa muda mrefu.
“Popote pale, kocha uhukumiwa na matokeo mabaya, kwa hiyo katika hili sio kusema Yanga ina tabia ya kufukuza makocha, sema wanafanyiwa mabadiliko kutokana na aina ya matokeo. Lakini naweza kusema kwa sasa ni tofauti kidogo kwa kocha Pluijm. 

“Kwanza ni mtu mwenye mtazamo chanya, tunaendana kimawazo, amekuwa akitupa ushauri chanya katika kuimarisha vikosi vyetu- vijana na wakubwa. Binafsi namuona kama ana maisha marefu Jangwani, ila tu angalizo ni kwa mashabiki wetu, wanatakiwa kuwa wavumilivu na kutodhubutu kuingilia kazi yake. Maana soka la Tanzania limezoeleka kuendeshwa na mashabiki. Tunaamini wakibadilika na kumuacha afanye kazi yake, hakika atatufikisha mbali,” alisema Tiboroha.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, kushoto.

KOCHA SIMBA AILIZA NDANDA, ATAJWA KIKWAZO CHA TIMU


The Hero.... Staam anatajwa kuwa shujaa wa Ndanda ambayo haijafanya vema ligi kuu bara


Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, Amri Said 'Jap Staam' ametajwa kuwa mchawi wa timu ya Ndanda ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu imekuwa na mwendo wa ‘bata’ tofauti na kasi iliyokuwa nayo kwenye ligi daraja la kwanza.

Said maarufu zaidi kwa jina la Staam, kwa sasa yupo na kikosi cha Mwadui akisaidiana na Jamhuri ‘Julio’ Kihwelo ambayo ina nafasui nzuri ya kupanda ligi kuu msimu ujao iwapo tu itashinda mechi zake dhidi ya Polisi Tabora na Burkina Faso.

Habari zilizopatikana zinadai kuwa mashabiki wa timu ya Ndanda wamekuwa wakiuliza kuondolewa kwa kocha huyo, kwani timu ilikuwa ikifanya vema enzi za kipindi chake tofauti na sasa kwenye ligi kuu.

Kwa upande wa Staam alipoulizwa kama anaweza kuwasikiliza tena Ndanda, alisema: “Mhh…ni ngumu ndugu yangu, kwanza nina mkataba na Mwadui na pia kwa kipindi kama hiki ni vigumu maana siwezi kuichukua timu katikati ya msimu, labda ingekuwa mwishoni mwa msimu ili niweze kuanza program zangu mwenyewe,” alisema Staam.
Unakumbukwa sana na Wana Kuchele wa Ndanda

MSIBA WA BABA WA P SQUARE WAVUNJA REKODI, ASKARI WATANDA KILA SEHEMU
Ni huzuni ulichanyanyikana na furaha! Ndivyo inaweza kusema kwa msiba wa matajiri mapacha wawili, Peter na Paul Okoye wa Kundi la P Square ambao wameondokewa na baba yao, Mr. Okoye Fell hapo jana.
Huzuni wa kipekee ni kwamba, wamekubwa na msiba huo ikiwa ni miaka miwili tu tangu waondokewe na mama mzazi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ni kwamba Mr. Okoye alifikwa na umati baada ya kuteleza nyumbani kwake na kuanga chini kwa kutanguliza kichwa chini, ikiwa ni siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Mpaka sasa, hukuna taarifa rasmi za kueleza umauti wake aidha kutoka kwa watoto wake- Peter, Paul wala Jude lakini Lola Omotayo amepost kwenye Ukurasa wake wa Instagram akieleza kofo chake.
Kwa upande mwingine, msiba wao umegeuka kama harusi kutokana na kufunikwa na mastaa kibao kutoka sehemu mbalimbali ambao ndio wametawala msibani hapo, hali iliyouchangamsha msiba huo na kusahau majonzi.
Katika msiba huo, jambo lililowaacha hoi wengi ni hali ya ulinzi kuimarishwa kama vile wanaweza kudhuriwa na mtu yeyote na mpaka sasa haijajulikana walikuwa na lengo gani la kumwaga maaskari.

Wasanii wa Kundi la P Square, Paul (wa kwanza kushoto) pamoja na Peter Okoye anayefuatia, wakiwa na mstaa kibao kwenye msiba wa baba yao kipenzi, Okoye  Marehemu baba yao enzi za uhai wake.

Ulinzi wa kutosha msibani.

Ibada ya mazishi ikisomwa.


Paul kulia na Peter Okoye wakifuatalia masikiliza ibada ya mazishi ya baba yao kipenzi, Okoye Fell aliyefariki jana

XAVI: BIFU LA MESSI MESSI & KOCHA KWISHINEYI!!

Moja ya mechi ambazo Messi alipigwa benchi msimu huu, jambo ambalo si rahisi kusikia kwa nyota huyo.


KIUNGO mwenye heshima ndani ya Barcelona, Xavi Hernández kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu sakata la kutoelewana kwa nyota wa klabu hiyo, Leonel Messi na kocha wake, Luis Enrique ambapo amesema kuwa wawili hao wamemaliza tofauti zao na mambo ni shwari kwa sasa.
Messi na Luis wamekuwa wakiripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na kwamba walikwaruzana kwenye mazoezilakini Xavi amefunguka kuwa. "Kila kitu kimeeleweka, sio ishu kubwa kwa sasa. Kuanzia kwenye makundi yao, tumelichukulia kwa ukubwa unaostahili, lilitokea lakini sasa limebaki historia.
 Akizungumzia timu yake Xavi alisema: "Kila mmoja na shauku ya ushindi. Kila mmoja anajisikia ari ya kushinda na tupo tayari katika hilo."

Amekwenda mbali na kummwagia sifa Neymar kwa kusema: "Ni mchezaji wa kipaji cha juu na tunajisikia faraja sana kuwa naye katika kikosi chetu. Ni mtu wa kipekee ana aina yake ya uchezaji, mwenye uelewa mkubwa wa soka na maisha ya yake anayoishi ni tofauti kabisa. Unatakiwa kujua jinsi gani ya kushinda, kushindwa, lakini hilo ni tofauti kwa Neymar. Ana maisha yake fulani hivi.
Xavi Hernanedz

KOCHA FIORENTINA: CUADRADO SIO WETU TENA, ANAENDA CHELSEA

Hatua moja mbele...kiungo wa Colombia na Fiorentina Juan Cuadrado anaenda Stamford Bridge muda wowote.
Kocha wa Fiorentina, Vincenzo Montella amefunguka kuwa kiungo wa timu hiyo, Juan Cuadrado atajiunga na Chelsea na kuongeza kuwa licha ya kumhitaji lakini isingekuwa rahisi kumbakiza kutokana na ofa kubwa waliotangaziwa ambayo katu kama klabu wasingeipiga chini.
Matajiri wa London, Chelsea, wanatajwa kutenga kitita cha euro milioni 35 kwa ajili ya kuansa saini kiungo huyo raia wa Colombia pamoja na kuwaongezea Mohamed Salah kwa mkopo.
Licha ya kwamba mpaka sasa pande mbili hazigongeana mihuri ya uthibitisho wa biashara hiyo, lakini Montella amesema kuwa anamchukulia Cuadrado kama mchezaji wa zamani wa Fiorentina alipoongea kwenye mkutano wa habari jana Ijumaa jioni.
"Isingewezekana kwa kukwamisha dili lake," alisema Montella. "Kwa mtazamo wangu kama kocha inakatisha tamaa lakini klabu ilikuwa na haki ya kufanya hivyo.
"Mchezaji wa kiwango cha juu ameondoka, ingawa bado naona sifa zake kwa Salah (mbadala wake). Sidhani kumuuza ni sababu yetu kurudi nyuma. 

[Cuadrado] ni mchezaji wa kimataifa  na siku zote alipenda kuwa nasi , pia na mimi najivunia kuwa anakwenda kujiunga na timu kubwa duniani."
Cuadrado kushoto katika moja ya mechi alizoichezea Fio msimu huu, hapa akijaribu kumpita moja wa mabeki wa AS Roma

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...