Saturday, August 31, 2013

SEMINA YA SERENGETI FIESTA KAMATA FURSA YAZIDI KUUNGURUMA MTWARAMkurugenzi wa Vipindi na maendeleo wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo ndani ya Ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara, kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano wa NSSF Makao makuu jijini Dar, Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.

Meneja Kiongozi,Uhusiano wa NSSF kutoka  Makao Makuu jijini Dar es Salaaam, Eunice Chiume akizungumza mapema leo kwenye semina ya Kamata  Fursa Twenzetu, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara mjini ,kulia ni Meneja wa NSSF wa  mkoa wa Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi na Maendeleo wa  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala Mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini hapo, Semina hiyo ni mpango mathubuti wa timu nzima ya Clouds Media Group ambayo inafadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo, na hii hufanyika mapema kabla ya shoo ya Serengeti Fiesta kulindima kwa siku maalum.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha.  
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpo ambaye pia ni mwanachama wa NSSF,akizungumzia fursa mbalimbali alizozipata ndani ya shirika la NSSF,mbele ya wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kushiriki katika semina hiyo,iliyokuwa na mafanikio makubwa.


Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semini hiyo


Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.Katika semini hiyo vijana wemejitokeza kwa wingi.

Msanii wa Kughani mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Mtwara kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huo. 
PICHA:MICHUZI JR BLOG

LULU AZINDUA FOOLISH AGE MLIMANI CITY


 
MSANII wa Filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu' akiongea jambo mbele ya waarikwa na mashabiki zake waliyohudhuria mahali hapo muda mfupi kabla ya uzinduzi wa movie yake ya Foolish Age kufanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judithi Wambura 'Lady Jaydee akitoa burudani kwa mashabiki waliyohudhuria uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ndani ya  Ukumbi wa Mlimani City.

Msanii wa Bongo Fleva Elias Barnaba 'Barnaba Boy', naye alipata fursa ya kutoa burudani kwenye uzinduzi huo.

Mzazi wa marehemu Steven Kanumba akiangua kilio huku akiwa amekumbatiana na Wema Sepetu,muda mfupi baada ya kukutana kwenye shughuli ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Dar.

Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa burudani wakiserebuka na nyimbo hatari za Machozi Bendi,zilizokuwa zikiimbwa na Lady Jaydee katika uzinduzi wa filamu hiyo.
 
Lady Jaydee,Gardener kulia wakiwa kwenye meza ya pamoja na waratibu wa uzinduzi huo.

  Josephat Lukaza akiwa katika pozi  na mrembo mmoja anayetambulika kwa jina la FettyCHEKA AMCHAKAZA MMAREKANI


Francis Cheka (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake kutoka nchini Marekani, Phil Williams. Cheka ameshinda kwa pointi.

BONDIA Francis Cheka ameendeleza umwamba wake baada ya kumgonga Mmarekani Phil Williams kwa pointi. Cheka ameshinda pambano hilo la WBF lililokuwa la raundi 12 ambalo limepigwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Friday, August 30, 2013

DIAMOND AMNUNULIA GARI MZEE GURUMO,VIDEO YAGHARIMU ML.48!!!

 Diamond akiongea jambo kwenye uzinduzi huu.
UZINDUZI wa video mpya ya Nasib Abdul ‘Diamond’ iitwayo My Number One, imeonekana kufuru kutokana na maandalizi yake na aina za kamera zilizotumika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi rasmi wa video hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar, walisema kuwa Diamond ameleta mabadiliko katika tasnia hiyo ya muziki wa Bongo Fleva hasa katika kipengele cha video bora. 
 Akitoa shoo mbele ya waarikwa wake
 Shaa,Master Jay na Madame Litta wakifuatilia uzinduzi huo
 Ay,Salama & Shetta hawakuwa nyuma kutazama zoezi hilo la uinduzi wa my number one ya Diamond
 Mzee Gurumo akiwa ndani ya gari lake muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Diamond kama moja ya zawadi yake.
 Diamond akimkabidhi ufunguo wa gari Mzee Gurumo.
Ray,JB wakishuhudia baadhi ya matukio ya uzinduzi huo
Baadh ya ndugu na jamaa wa Diamond wakifuatilia burudani za uzinduzi huo
Profesa Jay,Antu Mandoza,B2 na Nay wa Mitego katika pozi

Thursday, August 29, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 KUUNGURUMA MTWARA JUMAMOSI HIIWASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya wapatao 15 wanatarajiwa kutoa burudani kwa mara ya kwanza mjini Mtwara kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2013, katika Uwanja wa Nangwanda uliopo mjini hapo. Burudani hiyo itakuwa kivutio tosha kwa wakazi wengi kutokana na kundi kubwa la wanamuziki wa Kizazi Kipya kufanya makamzi kwa pamoja na wasanii wachanga wa mkoani hapo.

Siku hiyo majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 4, kutakuwa na Semina maalumu ijulikanayo kwa jina la Kamata Fursa Twenzetu, yenye lengo la kuwaonyesha wakazi wa pande hizo namna ya kujikwamua kimaisha katika kutumia fursa zilizopo mahali hapo, semina hiyo itaongozwa na viongozi wa Mkoa huo sambamba na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo la usiku.

Siku hiyo pia msanii mkali katika miondoko ya kuzungusha nyonga Snura Mushi anayetamba na kibao cha majanga atakamua sambamba na Nay wa Mitego, Makomandoo, Juma Nature, Matonya, Kassim Mganga, Chege na Temba,Madee, Young Killer, Stamina, Godzilla, Nikki wa Pili, Ommy Dimpoz, Kalapina na Pasha mtoto wa Mtwara wataonyesha umahiri wao katika muziki huo.

MMAREKANI PHIL,CHEKA WAPIMA UZITO TAYARI KWA MPAMBANO WA KESHO


Cheka akipimwa afya na daktari wa TPBO, Donald Madono.
 MABONDIA Francis Cheka na mpinzani wake, Phil Williams wanaotarajiwa kutwangana kesho Ijumaa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, kugombea mkanda wa ubingwa wa dunia wa WBF leo wamepima uzito kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es Salaam.
Mapambano ya utangulizi yatakuwa ni kati ya Thomas Mashali na Mada Mago, Alphonce Mchumiatumbo na Chupaki Chipindi.
Mmarekani Wills naye akipimwa afya ambapo mabondia wote walionekana wako salama kwa ajili ya mpambano huo

ANGALIA NJEMBA HII IKIKANDAMIZA CHAKULA YA MTOTO KWEUPE!!!GAZETI la Morning Post la China Kusini limeripoti kwamba watu wazima nchini humo wanawalipa wanawake fedha ili wawanyonyeshe maziwa yao ya kifuani!

Wanawake wanaojitolea kutoa maziwa yao hulipwa kiasi cha dola 2,700 za Marekani (kama sh. Milioni 4) kwa mwezi ambapo watu wazima hao huweza kuyanyonya maziwa hayo moja kwa moja kutoka vifuani mwa kinamama hao kama watoto wadogo!

Watu wengi wanaona jambo hilo ni la ajabu kwa mwanamme au mwanamke mzima kunyonya matiti ya mwanamke mwenzake. Hata hivyo, nyuma ya kituko hicho kuna habari kwamba watu wanaofanya hivyo ni wale wenye magonjwa sugu na ambao wanashindwa kupata chakula kizuri chenye rutuba ya asili, badala ya vyakula vingi nchini humo ambavyo vimechakachuliwa.

Hivyo katika mazingira ya uchakachuaji huo ambayo yameenea nchini humo, watu wanakimbilia kwenye maziwa ya kina mama ambayo wanaona ndicho chakula halisi na cha asilia na chenye viini vingi vyenye kuimarisha afya ya binadamu.

Pamoja na hivyo, maoni ya watu ni kwamba iwapo watu wengine wanawakodisha kina mama hao kwa ajili tu ya kufanya kitu hicho kama burudani, basi kitendo hicho si cha kiungwana, lakini kama kweli wanafanya hivyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao, hatua hiyo ni jambo jema.

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA WA KANISA LA E.A.G.T AFARIKI DUNIA


 
Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi, Moses Kulola amefariki dunia leo hii.
Habari hizi zimethibitishwa na mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya, Mch. Daniel Moses Kulola kupitia katika akaunti yake ya Facebook. kwa kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU." 

Hivi karibuni marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch. Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa baada ya kupata nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

ALIYEMPASUA AUNT EZEKIEL NI HUYU HAPA


 
Mrembo Yvonne aliyempasua kwa chupa Aunt Ezekiel usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas Posta jijini Dar es Salaam.

MREMBO aliyempasua mwigizaji wa sinema za Bongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ ajulikanaye kwa jina la Yvonne. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, ambapo Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto. 
 Vurugu kubwa ilizuka baada ya tukio hilo na Aunt alikimbizwa hospitali ya Aga Khan huku Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.
 
Mkono wa Aunt Ezekiel  uliopasuliwa na Yvonne kwa chupa.

Wednesday, August 28, 2013

PAMOJA NA CHANGAMOTO ZOTE ULIZOZIPATA ... HONGERA SANA CHAZ BABAHATIMAYE mwanamuziki wa Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’ amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu aitwaye Rehema Sospeter Marwa lakini mambo kadhaa ya kushangaza yamebainika ambayo ni kati ya kasoro zilizoitia doa sherehe hiyo.Ndoa hiyo ilifungwa Jumamosi iliyopita katika Kanisa la St. Peter, Oysterbay jijini Dar kisha sherehe zikahamia kwenye Ukumbi wa Marido, Sinza Makaburini ambako shamrashamra zilichukua nafasi.

CHAZ BABA AKIRI KASORO

Akizungumza na gazeti hili juzi, Chaz Baba alisema wakati anatangaza ndoa baadhi ya watu hawakuamini lakini hatimaye ndoto yake hiyo imetimia licha ya kasoro ndogondogo zilizojitokeza.

MIL. 3 ZA MCHANGO ZADAIWA KULIWA

Akifafanua moja kati ya kasoro zilizojitokeza katika sherehe hiyo, Chaz Baba alidai kusikitishwa na kitendo cha muweka hazina wake aliyemtaja kwa jina la Rehema ‘kutia ndani’ sehemu ya fedha za michango zipatazo shilingi milioni 3.

“Sikutegemea mtu kama Rehema kunifanyia hivi, nilimheshimu na kumuamini sana, nikapendekeza apewe jukumu la kutunza fedha matokeo yake amenifanyia hivi,” alidai Chaz Baba.
WANAKAMATI WALEWA KABLA YA WAALIKWA

Kingine kilichoitia dosari sherehe hiyo ni kitendo cha wanakamati kujipendelea katika suala vinywaji na kuwafanya wawe wa kwanza kulewa kabla ya wageni waalikwa.

Mmoja wa wanakamati ambaye kidogo alionekana kuwa mstaarabu aliliambia Risasi kuwa, alishangazwa na jinsi wenzake walivyokuwa wakiichangamkia pombe na kuwaacha wageni wakitoa macho.

“Ona wenzangu walivyolewa, yaani wamejipendelea wao kwanza badala ya kuwahudumia waalikwa, hii inanishangaza sana,” alisema mwanakamati huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.MADEMU WA CHAZ WAINGIA MITINI

Aidha, licha ya baadhi ya mademu waliowahi kuwa na uhusiano na Chaz Baba akiwemo msanii Husna Idd ‘Sajent’ kutoa ushirikiano katika maandalizi ya sherehe hiyo, wivu uliwazidia na hatimaye kushindwa kuhudhuria.

ILIFANA ILE MBAYA

Licha ya kasoro chache, sherehe hiyo ilifana sana na baada ya kutoka ukumbini maharusi walienda kucheza Twanga.

JK ARUDI KWENYE GAME

 GK akiwa ndani ya Studio za Clouds FM wakati akielezea kuhusu ujio wake.
MSANII mahiri katika anga za muziki wa Bongofleva, Gwamaka Kaihura 'King Crazy GK' leo ameibuka na singo yake mpya iitwayo Baraka au Laana aliyomshirikisha msanii Yuzo. 
GK alikuwa kimya kwa takribani miaka sita baada ya kuwa busy na masomo kitendo kilichopelekea kuupa kisogo muziki kwa muda na kuwafanya mashabiki wake kum-mis katika fani hiyo. 
Memba huyo wa East Coast Team ameachia ngoma yake mpya leo na anataraji kuachia video yake siku ya Ijumaa Agosti 30, mwaka huu. 
Akiongea na MTANDAO HUU, GK alisema kuwa amerudi kwenye game kwa nguvu zote na amewashukuru baadhi ya wadau kama Eric Shigongo, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kumtia hamasa ya kurudi kwa nguvu mpya baada ya kupotea kwa muda.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...