Tuesday, January 31, 2012

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

(TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES – TCU)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013

UTANGULIZI

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities’-TCU) ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council for Technical Education’ - NACTE) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board) inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:

MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”

Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinatakiwa kuwasilisha programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo wa mature entry, Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa na kuratibu utaratibu wa mitihani katika vituo maalum kikanda ili vyeti vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na hatimaye kuweza kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.

Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “Pre-entry” na “Mature Age Entry” na kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa kusudi hili utaanza mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya mitihani yao na kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.


Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-Entry” na “Mature Age Entry”.


1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo wa Pamoja (Central Admission System)


Waombaji watakaopitia mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) wamegawanyika katika makundi manne, ambapo waombaji wa kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa kama “Direct Applicants” na kundi (iv) watatambuliwa kama “Indirect Applicants”

Waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waliohitimu mafunzo ya diploma ya elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo vinavyotambulika na NACTE miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu;
Waliohitimu mafunzo ya Diploma ya Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika) katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waombaji ambao sio wa moja kwa moja (Indirect Applicants) ni wote waliohitimu kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma ya Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita (kuanzia 2009 kurudi nyuma).

1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi yao Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji watakaowasilisha maombi kupitia vyuo husika ni wenye sifa linganishi (Equivalent Qualifications) yaani wenye vyeti vya Astashahada na Diploma ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na NACTE. Ili kukamilisha udahili, wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili vyeti vyao vitambuliwe na kusajiliwa kabla udahili haujaanza.

Vyuo vinavyofundisha programu mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na Diploma ambavyo havina usajili wa NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka iwezekanavyo ili matokeo hayo yaweze kutumika katika utambuzi wa vyeti vya wanafunzi husika.

MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa kuwasilisha maombi ya udahili kwenye CAS umegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:

Kundi la Kwanza – (1 Aprili mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji wote waliomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6), na Diploma ya Ualimu kuanzia mwaka 2011 kurudi nyuma wataanza kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30 Aprili 2012.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
AIRTEL YAFANYA SEMINA KWA MASHIRIKA NA SEKTA MBALIMBALI NCHINI KUHUSU AIRTEL MONEY
Mkurungezi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Kalpesh Mehta akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria seminar hiyo iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili katika makao makuu ya Airtel , lengo likiwa ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (Kushoto) akiongesha kwa vitendo jinsi gani huduma ya Airtel money inavyofanya kazi na kutoa shuluhisho kwa changamoto wanazozipata katika kuendesha biashara kwa wawakilishi kutoka katika makapuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Airtel, pichani anayefata ni Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta na Meneja huduma Airtel money Asumpya Naligingwa.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi kutoka katika makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali leo kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari



Wadau waliohudhuria wakichangia hoja Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.


Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (kushoto) na Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta kwa pamoja wakitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali yaliyoalikwa kupata mafunzo juu ya faida na matumizi ya huduma hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za uendeshaji wa biashara zao. Semina hiyo semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.

-----------------------------
Katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inawafikia watanzania wengi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imeendesha semina ya huduma ya Airtel money kwa wadau na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa shule na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kupambanua faida za kutumia huduma mpya ya Airtel Money katika shughuli zao zinazohusiana na maswala ya kulipa au kupokea fedha.

Akizungumza wakati wa semina iliyohudhuriwa na wadau hao na kufanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania Afisa Mkuu wa Biashara Walingo Chiruyi alisema “lengo la semina hii ni kutaka kujadiliana na wadau wetu faida za kuitumia huduma yetu hii mpya ya Airtel Money katika shughuli zao za kila siku.

Tumegundua huduma hii ni nyenzo muhimu sana katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali.

Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa muhimu kwetu! Aliendelea kusema Bw,

Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile Ada ya shule, Mishahara ya wafanyakazi au vibarua, Kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya Dawasco, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.

Aidha kwa wafanya biashara za usafirishaji huduma ya Airtel money itawasaidia katika kupunguza risk za wizi wa fedha na kuwaakikishia usalama madereva wakiwa safarini kwani malipo yote ya bidhaa baada ya usambazaji hayatafanyika tena kwa pesa taslimu bali kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Kwa mabasi ya abiria wateja sasa wataweza kufanya booking na kulipa nauli kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo mteja hatakuwa na ulazima wa kutembelea kituo cha basi kukata tiketi na kulipia gharama za nauli.

Huduma ya Airtel money pia itapunguza gharama zilizopo katika kupata huduma za kifedha, na kwakupitia mtandao wetu ulioenea zaidi nchi nzima na mawaka waliosambaa kote tuna uhakika wa kuwafikia watanzania wengi zaidi walioko mjini na vijijini aliongeza Bi, Kazimoto.

Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamefaidi kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, Huduma ya Airtel money sasa ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima hivyo ili kukamilsha upatikanaji wa huduma hii ya kisasa na rahisi zaidi.

Posted by CATHBERT ANGELO
POSHO ZA WABUNGE HAZIJAPANDA- RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA UFAFANUZI
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku. 


Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao: 


Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi. 


Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:


Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili. 


Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
VODACOM YATANGAZA PROMOSHENI YA PUNGUZO LA GHARAMA
· *Wateja kupiga simu kwa robo shilingi na Kutuma SMS kwa Sh. 25/-

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza promosheni ya aina yake ya punguzo la gharama za simu kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno- SMS itakayowahusisha wateja wa kampuni hiyo ambao sasa watapiga simu kwa gharama ya ROBO SHILINGI kwa sekunde.


Promosheni hiyo ya siku saba kuanzia Jumatatu Januari 30, 2012 inahusu kupiga simu za ndani ya mtandao wa Vodacom yaani kupiga Vodacom kwenda Vodacom kati ya Saa nne usiku na saa moja asubuhi kila siku kwa wateja wote wa malipo ya kabla

Aidha sanjari na ofa hiyo kamambe Vodacom imetoa pia punguzo la gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno hadi shilingi 25/- kwa ujumbe wakati wote wa siku kwenda mtandao wowote wa simu ya mkononi nchini kwa kipindi cha siku saba nayo pia kuanzia leo Jumatau Januari 30, 2012.

Akitangaza promosheni hizo mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema ni imani yake kwamba katika kipindi chote cha siku saba cha promosheni hiyo wateja watafurahia kwa kufanikishiwa mawasiliano ya biashara, familia, kazi na mengineyo kwa gharama nafuu zaidi.

“Wateja wa Vodacom wakati wote wanafurahia huduma bora, nzuri na zenye kukidhi mahitaji halisi, ni wazi kipindi hiki cha siku saba cha promosheni hii ya punguzo la gharama za upigaji wa simu na utumaji SMS kitawapatia wakati mwengine bora wa kufurahia kuwa wateja wa kampuni inayoongoza soko”Alisema Bw. Rene.

Promosoheni hii inakwenda sawa na azma ya Vodacom ya kutoa fursa ya watanzania kuunganishwa kimawasiliano na kubadili maisha.

Ili mteja wa Vodacom aweze kufurahia promoheni hii ya punguzo la gharama za mawasiliano anapaswa kwanza kujiunga kwa kupiga *100# na kuanzia hapo atakuwa na uwezo wa kufurahia mawasiliano nafuu zaidi nchini miongoni mwa mitandaso ya simu za mkononi.

“Ni fursa nzuri kwa wateja wetu, tunawaomba waitumie ikiwa ya kiwango cha chini zaidi kuwahi kutokea katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi nchini na Vodacom itaendeleza utamaduni wa kuwa kinara wa kubuni na kuleta sokoni promosheni pamoja na huduma zenye thamani na mantiki halisi ya wateja wetu na jamii nzima nchini.” Aliongeza Bw. Rene

Rene aliongeza kwa kusema “Tunapoangalia katika utaratibu wetu wa kawaida wa mfumo wa maisha tanagundua kuwa muda wa kati ya saa nne usiku na saa moja asubuhi ndio wanafamilia hukaa pamoja na kufanya mawasiliano yenye lengo la kupashana habari za familia na hata kazi na biashara baada ya majukumu ya kutwa nzima au kabla ya kuanza siku mpya, hivyo ni imani yetu tumewapa wateja kitu chenye thamani na kinachoweza kutumika vema na kumnufaisha kila mteja.”Aliongeza

Vodacom ikiwa na wateja zadi ya milioni kumi nchini ni wazi promosheni ya aina hii itatoa faida kubwa kwa jamii kwa kuwawezesha kutumia sehemu ya punguzo la gharama ambazo wangengia kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kuelekeza sasa fungu hilo katika matumizi ya mahitaji mengine

MAPACHA WATATU, TID, SUPER SHINE, MR BLU WAWASHA MOTO DAR LIVE





 Wanamuziki wa Mapacha Watatu, Kalala Junior (aliyebebwa) na Khaleed Chokoraa, wakionyesha uwezo wao jukwaani hapo. 
 Mwimbaji wa kundi la Super Shine Modern Taarab, Ally Mikidadi, akiwajibika. 










 Bosi wa TOP Bandi, mwanamuziki TID, akiwajibika.
 Msanii Zuhura akipagawisha mashabiki.
 Mr Blu akitoa burudani kwa kila mtu.
 Dogo Hamidu a.k.a Nyandu Tozi akiwa na Mr Blue.
 Dogo Faume akiwajibika. 

 Msanii wa kucheza na kuigiza, Mpella Shaa ‘Kidevu cha Kuku’ akiwa amekaa juu ya chupa jukwaani hapo.
 Watoto wakiserebuka ukumbini.


Umati uliokuwa ukumbini ukifuatilia burudani hizo. 
---
WASANII wa muziki wa kizazi kipya na dansi Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry Samir ‘Mr Blu’, wakiwa na kundi la Mapacha Watatu ambalo linaongozwa na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’, Junior Kalala ‘Kalala Junior’, na Joseph Michael ‘Jose Mara’, na kundi la muziki wa mwambao la Super Shine,  usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.  Wanamuziki hao walivunja rekodi ya mashabiki wengi waliowahi kushuhudia makamuzi kama hayo katika kituo hicho cha burudani nchini. 

Shoo hiyo pia ilisindikizwa na makundi mengine kama Wakali Dancers, na wasaniii wengine wa Bongo Fleva wakiwemo Zuhura na  Dogo Mfaume na Hejos Band. 

Sunday, January 29, 2012


DK HARRISON MWAKYEMBE AIBUKIA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA KAWE
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo leo.

Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli.
Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika leo kwenye kanisa hilo na kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla ambapo FULLSHANGWE ilishuhudia tukio hilo. 

Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Dk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo leo.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada 
MECHI KATI YA WATANGAZAJI WA RADIO NA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LAFANA KATIKA VIWANJA VYA TTCL- KIJITONYAMA.
Siku iliyokuwa inasubiriwa na Watanzania kuhusiana na mechi kali kati ya Watangazaji, mapromota na waimbaji wa nyimbo za injili waliotegemea kupambana na wacheza filamu (Bongo Movie). Zoezi hili  halikuweza kufanikiwa kutokana timu ya Bongo Movie kuwa na mualiko Zanzibar katika tamasha lao la ZIFF. Badala yake kamati iliamua kupambanisha kati ya Waimbaji wa nyimbo za injili na Watangazaji wa radio za kikriso Tanzania. 

Tamasha lilionekana kuvutiwa na Watanzania wengi. Timu ya Watangazaji ilipigwa bao 2 na Waimbaji kuibuka washindi kwa mabao 5. Mfungaji bora wa watangazaji alikuwa Mtangazaji wa Channel Ten ambaye alikuwa mtangazaji wa radio ya  Praise Power, Boniface Magupa aliyefunga mabao mawili na kujipatia Tsh. 5000 kama mfungaji bora.

Mbali na mashindano ya mpira ya miguu kulikuwa na mchezo wa kufukuza kuku ambapo Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore alijishindia kuku na upande wa watangazaji wa radio, Yusuf Magupa wa Praise Power alishinda na kujipatia kitoeo cha kuku.

Waimbaji kama Martha Mwaipaja, Martha Ramadhan, Glorious Celebration na wengine wengi walionekana kugusa mioyo ya watu kwa  nyimbo zao zenye kumwinua Mungu wetu.

 Baadhi wa wachezaji wakiwa katika kiwanja cha shule ya Kenton Sinza wakijiandaa kuelekea katika uwanja wa Posta-Kijitonyama.
Stori zikiendelea.....

 Timu ya waimbaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Kenton Sinza
 Timu ya Watangazaji ikiwa katika kiwanja cha mazoezi Shule ya Kenton, Sinza

WACHEZAJI WAKIWA KATIKA UWANJA WA POSTA KIJITONYAMA
Bony Mwaitege (aliyevalia jessy nyeupe) akiufuatilia mpira
Goolkeeper wa watangazaji kutoka radio ya Praise Power, DP akiwa ameshikilia bori baad ya kufungwa.


MC  Uncle Jimmy

 Kipindi cha kujitambulisha


 Mashabiki
 Mtangazaji Kisaka



 Kipindi cha mapumziko



 Timu ya Waimbaji katika kipindi cha mapumziko







 Msikilizaji maarufu wa Praise Power a.k.a Mzee wa Kubonya
 Mtangazaji wa Praise Power (kulia), Uncle Jimmy na Mchekeshaji Chavala (kushoto)

 Mzee wa mblogu na mawebsite pamoja na mgarphics, Rulea Sanga (katikati akiwa amezungukwa na waimbaji wa Glorious Celebration
Mtangazaji wa Wapo Radio, Silas Mbise (kulia) akiwa na rafiki zake. Kutoka kushoto ni Jessica na lilian
Watangazaji wa mpira wakiwa katika corner yao
 Waimbakji wa Glorious Celebration wakitoa huduma yao ya juimbaji katika pambalo la mpira



Glorious Celebration Live Band
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Jessica Honore (anayepunga mkono), akiwaongoza waimbaji wenzake baada ya kushuka jukwani


Martha Mwaipaja

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...