Monday, April 21, 2014

UGOMVI WA PETER & PAUL WA P-SQUARE, MKE WA PETER NA KAKA YAO INASEMEKANA NDIO CHANZO


Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.

Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.

Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.

Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.

Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.

After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.

— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014

Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.

Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya

MKAZI WA MOROGORO USIKOKESE MKUTANO HUU...MOROGORO YOTE KWA YESU

TAMASHA LA PASAKA 2014 LAFUNIKA


Edson Mwasabwite

Ni mwendo wa mfululizo, wimbo hadi wimbo. Prophet Keke punde baada ya kupanda jukwaani

Son of Tanzania, Ephraim Sekeleti

Babu na nani? Senior bachelor? mi sijui, ila hawa ni Philemon Rupia na Anthon Joseph wa WAPO Radio FM.

Baadhi ya kinadada wa GWT... glory glory..'vocalists' wa KekeKekeletso
Kila mtu kwa raha zake

Baadhi ya umati uwanjani hapo

mtu na 'wajomba'zake

Moja kwa moja kutoka London nchini Uingereza,

Rose muhando, akiwatahadharisha watu kwa kibao chake kipya cha 'fesibuku'.

Kwani ni jambo lipi hilo yeye asiloliweza? Sarah K anauliza..

Sunday, April 20, 2014

DUDE ‘APIGWA’ TENA!

MGANGA hajigangi! Licha ya kuwa msanii mahiri anayeelimisha jamii jinsi ya kugundua utapeli na kuepukana nao, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibiwa ‘kupigwa’ vifaa vya saluni na vibaka.

Msanii mahiri Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Akistorisha na mwanahabari wetu, Dude alisema juzikati vibaka hao walipanda kwenye dari na kukata ‘celling board’ kisha kuingia ndani ya saluni yake hiyo ya kike inayosimamiwa na mkewe, maeneo ya Jeti-Lumo, Dar na kukomba vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba.

“Ukweli nimechoka sasa kila siku wananirudisha nyuma kimaendeleo kwa kuniibia sijui nifanyeje maana imeshakuwa hatari kwangu, wamechukua TV, madela, redio aina ya sabuufa na vingine vidogovidogo,” alisema Dude ambaye mwaka 2012 na 2013 aliwahi kulizwa vifaa mbalimbali vya nyumbani.

TID, RECHO THT WADAIWA NI WAPENZI

MALOVEE? Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’ na mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’, wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni wa kimapenzi, Ijumaa Wikienda limeinusa.


Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’

Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘mitungi’ kiasi cha kushindwa kuzificha hisia zao.


Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’.

“Mbona ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena wanapopiga mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja mjini Dodoma, waliponda raha kinomanoma,” kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana mashosti zake wa karibu.

“Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani, halafu pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata ‘mambo meupe’ anatumia,” alisema shosti huyo.

Baada ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini kwake THT, Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana muda mrefu hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi.

Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
“Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu wangu kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila ninapokuwa na mwanaume wanasema ni bwana’ngu kitu ambacho si cha kweli kama wanavyonizushia kuvuta bangi.

“THT siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe. Nimekuja kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia uongo,” alisema Recho.

Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo.

“Dah...! Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye,” alisema TID.

BATULI: NILIFURAHI KUKUTA MAGAZETI YA PENDWA BUNGENI
Mwanadada mrembo kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ pozini.

MWANADADA mrembo kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kuwa alifurahi kukuta magazeti Pendwa ya Global Publishers ndani ya mjengo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akipinga stori na paparazi wetu, Batuli alisema aliyaona magazeti hayo hivi karibuni alipokuwa amekwenda mjengoni humo kuwawakilisha wasanii katika Bunge la Katiba akiwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Saimon Mwakifwamba na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’.

’’Magazeti yote ya siku utayapata palepale ila nilifurahi zaidi kuona magazeti Pendwa ndiyo yamepewa kipaumbele zaidi, wauzaji huyaweka mbele kuonyesha vichwa vya habari na ndiyo maana waheshimiwa wanajua sana stori za wasanii,” alisema Batuli.

Magazeti Pendwa yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd ni Ijumaa Wikienda linalotoka kila Jumatatu, Uwazi (Jumanne), Risasi Mchanganyiko (Jumatano), Amani (Alhamisi) Ijumaa (Ijumaa) na Risasi Jumamosi (Jumamosi).

Tuesday, April 15, 2014

SAFARI YA MWISHO ZA MAREHEMU MUHIDIN GURUMO


SNURA ALEWA PENZI LA DVJ HUNTER.Snura Mushi na Dvj Hunter wa Club Maisha Ya Mjini Mbeya wakiwa katika Poz la maha..!Kwa mujibu wa mtu wa karibu aliozinasa picha hizo zilizopigwa huko mkoni Mbeya alisisitiza kwamba jina lake lisitajwe humu mtandaoni, Pia alizidi kufunguka kwamba kabla hajakwanyua picha hizo alibahatika kusikia maneno ya Snura kama ifuatavyo:

Mimi kwa huyu jamaa sina ujanja na kamwe sitosikia la mtu ng'o! Mmmh.. Penda sana Hunter...!
Jamaa aliishia hapo akasema alikuwa anapita tu!

MLIPUKO WA BOMU ARUSHA.


Ulinzi kaitka eneo la baa palikotokea mlipuko (picha: Arusha255 blog) Jumapili, Aprili 13, 2014 ulitokea mlipuko wa kinachodhaniwa kuwa bomu la kurushwa kwa mkono katika baa maarufu kwa maonesho ya mechi za mpira wa miguu wa Ulaya, ijulikanayo kama Arusha Night Park au Matako baa iliyopo maeneo ya Mianzini, mkoani Arusha na kujeruhi zaidi ya watu 20 wengi wao wakiwa wateja waliojazana kushuhudia mechi za soka.
Majeruhi walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu yaharaka, na hakuna taarifa rasmi ya mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya walionusurika wanashuhudia kuwepo watu waliokatika miguu.
Taarifa ya awali kutoka Jeshi la Polisi inaeleza kuwa bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji baada ya kukuta vipande vya vyuma na misumari eneo la mlipuko. Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na mtu anayeendelea kusakwa na Jeshi la Polisi likiwa kwenye mfuko wa plastiki kuelekea katikati ya mashabiki hao.

MTU NA KAKA YAKE, GRACE NA JOSHU KUACHIA ALBAMU YAO YA KWANZA YA MY SAVIOUR GOD

Baada ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080
Tembelea www.rumaafrica.blogspot.com

MUNGU AKUBARIKI

Monday, April 14, 2014

HIZI NDIO HATI YA MUUNGANO BAADA YA KUONESHA IKULU SIKU YA JANA


MZEE WA MIAKA 60 AUAWA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA WILAYANI MAKETE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA
Mwili wa marehemu baada ya kuondolewa eneo la tukio.

Daktari Luvanda kutoka hospitali ya wilaya ya Makete akionesha majeraha ya kichwa cha mwili wa marehemu yanayohisiwa kupelekea kifo chake.

Polisi kutoka kituo cha Tandala na Makete wilayani wakichukua taarifa za mauaji hayo kwenye shamba ulipokutwa mwili wa marehemu.

Askari akizungumza na wananchi waliofika eneo la tukio na kuwaonya kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi pamoja na kushirikiana na jeshi hilo kuwapata watuhumiwa wa mauaji hayo.


Mkazi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe amefariki Dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguuni na mtu/watu wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya, Mrakibu mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni afisa upelelezi Wilaya ya Makete Bw.Gozbert Komba amesema walipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho na kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60) mkazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Wilayani Makete


Bw. Komba amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia Ijumaa wiki iliyopita na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina kwa kuwa marehemu alikuwa mzee na pia kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa na polisi


Pia amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuhakikisha wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa kwani kitendo walichokifanya ni cha kinyama na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji hao walitokomea kusiko julikana

Bw.Komba amekemea vikali suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi wilayani hapo na kuwaomba wananchi wasiwe na tabia hizo za kuwaua wazee kwa imani za kishirikina na kuwataka watii sheria bila shuruti ili kuishi kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla

Mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi ukiwa na majeraha sehemu za kichwani na mguuni ambayo yanadhaniwa kusababisha kifo chake, baada ya watu kupita eneo hilo na kuukuta mwili huo

katika kipindi cha hivi karibuni wilayani Makete kumekuwa na matukio ya mauaji kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi na imani za kishirikina jambo linalotia doa wilaya hiyo kutokana na ongezeko la watu kuchukua sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa wa matukio mbalimbali

MATUKIO YA NYUMBANI KWA MAREHEMU GURUMO
Wawakilishi wa Global Publishers, Sifael Paul (anayeandika kwenye daftari) na Elvan Stambuli mwenye kizibao, wakiandika mchango wa Kampuni ambao ni shilingi 500,000 kabla ya kuwakabidhi ndugu wa marehemu Muhidini Gurumo leo jioni nyumbani kwa marehemu Makubuli, Dar, leo. Atazikwa kesho Masaki, Kisarawe.


Mwakilishi wa Global Publishers, Elvan Stambuli akimkabidhi mjomba wa marehemu Muhidini Gurumo, Yahya Mikole (katikati) shilingi 500,000 ambazo ni rambirambi ya kampuni kwa msiba huo.


…Fedha zikihesabiwa.


Mwakilishi wa Global akizungumza, Stambuli akimtambulisha Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul kwa nguli wa muziki King Kikii ambaye alikuwepo msibani leo.


Mwanamuziki mpapasa kinanda, Abdul Salvado ‘Father Kidevu’ akisalimiana na mwakilishi wa Global.


Hawa ni wadau wa muziki wa dansi wakiwa msibani keo huku wakionesha sura za huzuni.
Rashidi Pembe (mpuliza saksafoni kulia) akiwa na King Kikii msibani leo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...