Tuesday, April 30, 2013

HATIMAYE WEMA AMWANIKA BABA YAKE MTANDAONILeo hii kupitia mtandao wa Instagram, Wema alitupia picha akiwa na baba yake mzazi, mzee Sepetu, huku pembeni akiwepo mtu wake wa karibu sana "Pettiman.

HIVI NDIVYO NEY, ROMA, MADEE WALIVYOFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA‏:

Msaniii wa Miondoko ya Hip Hop Roma Mkatoliki akitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Mwanza waliofurika katika viwanja vya Furahisha mkoani humo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha uliofanyika mwishoni mwa wiki kwa siku mbili mfululizo.
 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) wamefunika kwa kutoa burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel nchini ya airtel yatosha na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika katika viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.

Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.

Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma Khasim ‘Nature’ na kundi lake la wanaume halisi, Roma Mkatoliki, Madee na Ney wa Mitego.

Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na kupata zawadi ya laini na fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel zilizotolewa kwa washindi waliopatikana.

“Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya kutumia huduma hii”alisema msanii Ney wa Mitego.
Akizungumzia Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika katika mikoa sita hadi sasa hapa nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.

Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini Mwanza alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika mahojiano maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel yatosha amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua
mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
“Huu ni Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu wanaokuja kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja huyo.

“Hatukaangi laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia Mwanza ni Mkoa wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na ufugaji hivyo wananchi wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel ambao umedhamiria kuwainua kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii itawasaidia kujifunza Airtel kuna nini ndani ya mtandao huu”alisema Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea katika Mikoa ningine na mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo itahamia Jiji kubwa la Dar es salaam katika viwanja vya Zakhem na kutakuwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali kutokana na wasanii wengi kuwa
jijini humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza ndani ya mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuuu.

Msanii wa Bongo Flava toka kundi la Tip Top Connection lenye makazi yake mtaa wa Manzese Dar es Salaam maarufu kwa jina la Madee akitumbuiza katika tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki hii.
Msanii wa Hip Hop anayeshabikiwa kwa wingi, Nay Wamitego, akikamua wakati wa tamasha maalum la uzinduzi wa Airtel Yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha.
Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya Hip Hop wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la Airtel Yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha.
Wananchi mbalimbali wa mkoani Mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha.
 
Dotnata awekewa sumu kwenye juice, yamwathiri, figo, mbavu na uti wa mgongo
Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.

Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.

Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.

“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.

Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:

“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”

Monday, April 29, 2013

BREAKING NEWS: GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA .Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha. Kwa sasa mamia ya wafuasi wa Chadema wanaandamana na mbunge huyo kuelekea makao makuu ya chama hicho.

HIZI NI PICHA ZA SHOW ALIYOPIGA JANA IZZO BIZNESS WAKATI WA UZINDUZI WA NYIMBO YAKE MPYA

Usiku wa jana katika ukumbi wa disco wa AMBASSADOR LOUNGE, mkali kutoka Mbeya City, talkin about IZZO BIZNESS alikuwa anazindua ngoma yake mpya inayojulikana kama ... Ngoma hiyo inayojulikana kama LOVE ME ilichezwa kwa mara ya kwanza katika disco hilo huku akisindikizwa na wasanii wenzake kama SHAA na BARNABA ambao wameshirikishwa humo ndani ...
IZZO BIZNESS akimvalisha mrembo aliemchagua zawadi ya miwani ambayo aliingia nayo on stage kupiga show ...
 
Mbeya City was in the building ... QUICK ROCKA na IZZO katika BALL PLAYER on the performance ...
IZZO BIZNESS na BARNABA wakikinukisha kwa fans ...
SHAA doing her thang ...
IZZO BIZNESS akiwa na fans baada ya show ... Kulia ni mwanadada WEMA SEPETU ...

Saturday, April 27, 2013

JAGUAR MSANII WA KENYA BUYS A PLANE......AMFUNIKA PREZZO NA KUMFUNGA MDOMOIt is Saturday afternoon and as the clock ticks 3pm, an informer calls me up.
“I have a hot story for you,” the informer says with a hasty tone before losing taste for suspense and urging: “Just get yourself down to the Wilson airstrip… Jaguar…”
“Jaguar? What about Jaguar?” I wonder aloud as the caller disconnects, leaving me confused.
Frantically, I try to reach out to the singer, all in vain as my paparazzi instincts get aroused.
By now, the caller’s number has gone mute. I arm myself with a camera, call my taxi guy James, and command him to head to Wilson. Upon getting there, I make no sight of Jaguar and my frantic efforts to get to the waiting lobby are thwarted by heavy security guards, who don’t give a damn about my rhetoric, that I am a good ol’ scribe in the line of duty, trying to investigate a story.
Worse so, even Jaguar’s mobile phone has been switched off.
As I ponder my next move, to my reprieve, a young man dressed in airport attendant’s gear sighs as he passes by, waving his hand, directing me to follow him. I oblige.
“I am the one who called you. I got some photos for you. Jaguar has just left in his new plane. He was with some musicians, and I am aware they have gone to Naivasha for the weekend,” he drops the shocker, before pulling out his camera in which there is a sequence of pictures of the singer standing by a sporty Bentley convertible and a six sitter plane, both christened with Jaguar’s name.

I can hardly identify the individuals but two look familiar; the two bodyguards Jaguar had been moving with during the campaign period after word went round he was working closely with (now) President Uhuru Kenyatta.
The informer, who now introduces himself, as John wants nothing to do with the story and pictures. In fact, all he asks for is a few coins to quench his throat over the weekend.
“Jaguar bought this plane during the campaigns and he is always coming here over the weekend to fly out. He was in Diani last weekend and now, he has left for Great Lake Resort in Naivasha. The Bentley left with someone else alongside another car,” John informs.
I hand the guy some little cash and in another minute, the pictures are safe in my flash disk… Mission accomplished, almost.

DOTNATA ALISHWA SUMU YA KUMUUA TARATIBU !AMANDA POSH ALIZWWA NA HALI YA MAMA YAKE

Habari ni kuwa muigizaji wa filamu na mfanyabiashara maarufu Nchini Dotnata amewekewa sumu ya kumuua taratibu kwa kipindi cha miezi 8 sasa huku watu waliofanya hivyo wakiwa bado kujulikana. Muigizaji Amanda Poshy ameandika hiki kupitia facebook............................

"Kiukweli kati ya habari iliyonipa mshtuko mkubwa na iliyonifanya nikose nguvu ni kitendo cha mama yangu Dotnata kulishwa SUMU......nazungumzia sumu nikimaanisha sumu......mama yng hana matatizo na mtu...anacheka na kila mtu.....anampenda kila mtu.....hana ugomvi na mtu.....leo mtu unadiriki kumlisha sumu kweli?hayo ndio majibu ya dr baada ya mama yng kuumwa kwa muda mrf majibu yametoka amelishwa sumu ya kummaliza taratibu miezi nane iliyopita......nimeumia sana na aliyefanya kitendo hk atalaaniwa na Mwenyezi Mungu......inshaallah Utapona kwa uwezo wa Allah mama...pole sn...nipo pamoja nawe kwenye maumivu haya unayopitia"

Tunampa pole sana Dotnata na tunamuombea kwa Mungu apone haraka.

JUSTIN BIEBER MATATANI TENA, HUENDA AKAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA.
Polisi nchini Sweden wamedai kukuta dawa za kulevya katika basi linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za kimuziki.
Msemaji wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.

RAISI KIKWETE ASAMEHE WAFUNGWA 40000Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180.

Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya muungano.

Viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani walishiriki kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni ishara ya kuuenzi na kuulinda muungano huo.

Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd.

Wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Baada ya viongozi kuketi katika nafasi zao, gwaride rasmi lenye gadi kumi lilipita na kutoa heshima zao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya hapo vijana wa halaiki walionyesha maumbo mbalimbali kuashiria maendeleo yaliyopatikana nchini kwa muda wa miaka 49 tokea taifa la Tanzania liundwe rasmi kabla ya Wanahalaiki kujipanga na kuonyesha taswira mbalimbali na kuimba wimbo wa kuhamasisha kudumisha muungano.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani hawakuweza kushiriki kwenye maonyesho hayo.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa shughuli za maadhimisho hayo, mjumbe wa Kamati Kuu Chadema ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kujivunia Muungano walionao kwa sababu umedumu kwa miaka 49, akieleza kuwa ni nadra sana kuona nchi za Afrika au Ulaya kuendeleza muungano wenye umri mkubwa kama huu wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuulinda kuendeleza amani iliyopo.

Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini katika kuadhimisha miaka 49 ya muungano.
Wafungwa waliosamehewa ni wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano, ambapo mpaka siku ya msamaha yaani April 26, watakuwa wameshatumikia robo ya vifungo vyao, wafungwa wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na kansa ambao wamethibitishwa na jopo la madaktari.

Pia wazee wenye umri wa miaka sabini au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, wakiwamo walemavu.
Msamaha wa Rais pia umeenda kwa wafungwa walemavu wa mwili na akili na wafungwa ambao hadi siku ya jana walikuwa wameshakaa gerezani kwa muda wa miaka mitano na wameonyesha kuwa na tabia nzuri.

Thursday, April 25, 2013

VURUGU ZA LINDI: NYUMBA 15 ZA VIONGOZI WA CCM ZIMECHOMWA NA MIFUGO YAO IMEKATWA MAPANGA NA WANANCHI

Nyumba zaidi ya saba za kuishi na nane za maduka pamoja na mifugo; vyote vikimilikiwa na viongozi wa CCM, akiwamo mbunge na madiwani wilayani Liwale, vimeteketezwa kwa moto na kuharibiwa na wahalifu.
Mali hizo zikiwamo za viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ilulu, Liwale, vimeteketezwa kwa kilichdaiwa kuwa ni kupinga kulipwa malipo kidogo ya korosho, msimu wa mwaka jana.

Taarifa ya Polisi, ilisema jana kuwa watu wanaodhaniwa kuwa wakulima wa korosho, walijaribu kuzuia gari lililokuwa na malipo ya korosho, wakipinga malipo ya pili ya zao hilo na kufanya vurugu na uharibifu wa mali.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, alionesha wasiwasi bungeni akisema huenda kuna baadhi ya watu, wakiwamo wanasiasa walio nyuma ya matukio hayo ili kuficha uovu wao na wengine kujinufaisha kwa maslahi binafsi.

Waliochomewa nyumba katika vurugu hizo, ni Mbunge wa Liwale, Faith Mitambo, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Liwale, Mohammed Mngomambo, Katibu Mwenezi wa CCM wa Wilaya, Abdallah Chande na Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ilulu, Hamza Mkunguru.

Wengine walioathiriwa na vurugu hizo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Diwani wa CCM, Abas Mtalilo ‘Chigogola’ na madiwani wenzake, Hassan Myao, Musa Mkoyage, Mzee Salehe na Amina Mnoche.

Akizungumza na mwandishi jana, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Hemed Ndimane alisema duka lake la vyakula lilivamiwa na mali zote kuporwa. Ng’ombe watano waliouawa kwa kukatwa mapanga, ni mali ya Mkunguru.

Naye Mitambo alisema nyumba zake mbili zilichomwa moto huku moja ikiteketezwa kabisa, nyingine ikibomolewa paa na kunyofolewa milango na madirisha.

Mbunge huyo alisema Chigogola alichomewa nyumba ya vyumba 11, pikipiki mbili, trekta dogo ‘power tiller’ na ng’ombe wake 12 waliuawa.

Alisema Mngomambo alichomewa nyumba kama alivyofanyiwa Chande; sawa na madiwani wote wa kata za mjini Lindi.

Ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga alisema atatoa taarifa baadaye, lakini taarifa ya makao makuu ya Polisi, Dar es Salaam, ilisema mpaka jana watuhumiwa 19 walikuwa wamekamatwa kwa mahojiano. Vurugu hizo zilizoanza juzi asubuhi, eneo la Liwale ‘B’.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Abdallah Ulenga, Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikutana jana baada ya tukio hilo huku Kamanda akisisitiza kuwa hadi jana mchana walikuwa wakiendelea na vikao, kabla ya kutoa taarifa kamili kwa vyombo vya habari.

Ulenga alisema wananchi hao walivamia maduka na nyumba za viongozi hao na kuziteketeza kwa moto, kutokana na madai kwamba walipata malipo ya pili ya Sh 200 badala ya Sh 600 kwa kilo.

“Lazima tufahamu ni kwa nini, kama mauzo yalikuwa Sh 1,100 kwa kilo, wataalamu wanatakiwa watoe maelezo juu ya malipo hayo yaliyofanywa Liwale,” alisema Ulenga.

Bei ya korosho kwa kilo ilikubaliwa kuwa Sh 1,200 kwa kilo, lakini baada ya kushuka kwa bei katika soko la dunia, ilishuka na kuwa kati ya Sh 1,000, Sh 1,070 na 1,100.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Lindi, Killian Kapamba alisema hajui kama vurugu hizo ni za ununuzi wa korosho au za kisiasa, kwa kuwa mali za viongozi wa kisiasa ndizo zilizoharibiwa.

Alisema inakuwa vigumu kubaini sababu za vurugu hizo kwa kuwa pia Chama cha Msingi cha Ushirika cha Umoja, ambacho ndicho chenye jukumu la kutoa malipo hayo, kilikuwa hakijaanza kutoa malipo ya pili kwa wakulima na wanachama.

Hata hivyo, taarifa kutoka Polisi zilisema baadhi ya viongozi waliodaiwa kuhusika na uchochezi huo, wamekamatwa.

Akizungumza bungeni jana, Malima alieleza kusikitishwa na vitendo vya wananchi kuchukua hatua mkononi na kuharibu mali bila kutoa fursa ya matatizo yao kushughulikiwa.

Malima ambaye alionesha wasiwasi wa wanasiasa kuwa nyuma ya vurugu hizo, alisema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Kawawa (CCM), kuliwasilisha suala hilo bungeni.

Zainabu wakati akitoa hoja hiyo, aliitaka Serikali kutengeneza utaratibu utakaowezesha wakulima hao kulipwa fedha wanazodai, ambazo ni Sh 400 walizopunjwa katika malipo ya korosho.

“Naomba nieleze masikitiko yangu juu ya tukio la jana (juzi) usiku katika wilaya ya Liwale…wakulima wa korosho wameghadhabika na kuamsha mapambano kati yao na polisi, hadi kusababisha uharibifu wa mali zikiwamo nyumba za viongozi,” alisema Kawawa.

Alisema wakulima hao walichukua hatua hiyo, baada ya kutotimiziwa malipo ya korosho ya Sh 1,200 kwa kilo. Alisema awali walilipwa Sh 600 tu, baadaye wakapewa Sh 200 na hadi sasa hawajamaliziwa Sh 400 zilizobaki.

“Kwa maana hiyo wakulima hao walilipwa Sh 800 tu, wanachodai ni tofauti ya Sh 400, nimezungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika amenieleza kuwa bei ya korosho imekuwa ikibadilikabadilika,” alisema Zainabu.

Aliiomba Serikali iingilie kati mgogoro huo kwa kuahidi kama inaweza kufidia Sh 400, ili mkulima wa korosho alipwe Sh 1,200.

Akijibu hoja hiyo, Malima alisema: “Hii lazima tukubaliane kuwa kuna vitu vimejificha humu, sehemu zote ambazo zinalimwa korosho ikiwamo Mkuranga, kuna matatizo ambayo yanasababisha korosho kutouzwa na matatizo haya hayalingani kote, yanatofautiana,” alisema.

Alisema kwingine matatizo ya wakulima wa korosho yanatokana na vyama vya ushirika wakati kwingine kuna matatizo ya wanunuzi.“Sasa mimi nashangaa kwa nini vurugu za namna hii zinaibuka? Kuna sababu nyingi, pengine hata hawa viongozi wa ushirika wanahusika ili kuficha maovu yao au hata tu masuala ya kisiasa,” alisema Malima.

Kutokana na vurugu hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mngulu, kwenda kuongeza nguvu mkoani humo kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa.

Timu hiyo imetakiwa kuhakikisha hali ya amani na utulivu inarejea haraka na waliohusika na uhalifu, wanakamatwa na kufikishwa mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake.

JITEGEMEE ALUMNAE REUNION

Antu Mandoza  Co-Coordinator

Co-Coordinator Antu Mandoza na Wasiwasi Mwabulambo wakishirikiana na kamati ya Jitegemee ikiongozwa na Mkuu wa Shule Mrtin Mkisi, wamaletea Alumnae Reunion siku ya kesho pale pale JKT kuanzia saa 2 asubuhi na kuendelea. Kutakua na michezo yote kuvuta kamba, kukimbiza kuku, basket ball, Volleyball, football pia kukumbushiana enzi kutakuwa na kwata la hiari, msosi na vinywaji vyote, burudani kutakuwa na wasanii waliowahi kusoma Jitegemee akiwemo Mh. Temba na wana TMK, Soggy Doggy, Mabaga Fresh na wengine wengi. Kwa mchango wako wa Tshs. elfu tano (5,000) tu getini. 
WOTE MNAKARIBISHWA.

Tuesday, April 23, 2013

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA TUNDA MAN.

HUYU NDIYO LULU MICHAEL NA PENNY KATIKA MUONEKANO WAO MPYA

MR. NICE AFUNGUKA KUHUSU BEEF LAKE NA WATANZANIA NA NIA YAKE YA KUOA MKENYAMsanii mkongwe aliyekuwa amepotea kwenye chart nchini, Nice Lucas Mkenda ameendelea kutengeneza vichwa vya habari nchini Kenya baada ya jana kuhojiwa kwenye vituo vikubwa vya runinga nchini humo, Citizen TV na NTV.

Katika kituo cha Citizen, Mr Nice ambaye amesainishwa kwenye label ya Grandpa Records, alikuwa akihojiwa live kwenye muda wa taarifa ya habari ya jioni kwa lugha ya Kiswahili inayotazamwa na watu wengi nchini humo na hata Tanzania huku kwenye NTV akionekana kwenye kipindi cha comedy cha The Churchill Show. Haya ni miongoni mwa yale aliyoyaongea Citizen TV.

Kuhusu sababu za kwenda Kenya
Nilikuwa nimesimama muziki muda mrefu kama miaka minne hivi na baadaye nikakutana na kampuni ya GrandPa Records.

Kwakweli walinifuata Dar es Salaam tukaongea maneno mengi ya busara sana kwasababu wao naona wanaona mbele zaidi. Wakaniambia Mzee ‘we umekaa kimya muda huenda ni sababu ya hasira lakini bado watu wanakuhitaji sana kwahiyo kuna vitu vingine hata kama vilikukwazwa vinaweza vikatatulika kwasababu unangojewa tu haujawa wa zamani, bado wewe ni mpya’.

Nimekaa nyumbani 4 years lakini kaja mkenya, kanifuata kwa gharama nyingi sana na kunishawishi you must come back again! kwahiyo nasema wakenya asanteni sana kwa yote mliyonifanyia .

Kuhusu kama ana beef na watanzania
Hapana mimi sina beef na watanzania wenzangu kwasababu kwanza kazi ya muziki ni yangu sio ya watanzania na kila mtanzania ana kazi yake, kila mkenya ana kazi yake.

Kwasababu hata kuna wakenya wanafanya kazi Tanzania wapo Tanzania na walifuatwa hapa Kenya kwenda kufanya kazi Tanzania. Nimekumbana na maswali mengi kwenye interview ‘kwanini usifanye na kampuni za Tanzania?

Nikasema walioniona na wakaona kwamba nahitajika, ni mkenya ndio alikuja kunifuata so ningeacha kufanya naye kazi? Na akanipa faida zake.

Kuhusu wimbo wa Mack Muga wa Ali Kiba
Ali kiba ni mdogo wangu, rafiki yangu na hatujawahi kukorofishana hatujawahi kuwa na beef ya aina yoyote hata sijawahi kumsikia akinizingumzia mahali kwa ubaya.

Haya ninayoyasema hapa , hizo ni story kichaa kwasababu nimeizunguka sana dunia kwakweli, passport yangu inatisha, unaifungua kama gazeti lakini bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kufika South Africa hata siku moja na wala sijawahi kufanya hata interview na kituo chochote.

Na hiyo nimeisikia hapa Kenya hata Tanzania sijawahi kusikia kitu kama hicho.

Kuhusu kuoa
Nadhani ni moja kati ya mambo yaliyonileta hapa nimekuja pia kuoa Kenya, short and clear , atapatikana na nitawaambia hayo ni mambo ya kumwachia Mungu.

LULU FEKI AIBUKA NA KUCHANGISHA PESA FECEBOOK...SOMA JINSI WATU WALIVYOTAPELIWA PESA ZAO
Mtu mmoja ameamua kwa maksudi kabisa kutumia jina la msanii lulu michael lulu na kujikusanyia fedha kwa njia isiyo halali kwa kutumia jina hilo

Akizungumza kwa njia ya simu msanii huyo amelaani kitendo cha mtu huyo kuweka namba za simu na kusema lulu ameongeza nafasi za waigizaji wachanga ,lulu amesema kwasasa amejipanga na ataweka mwanasheria wake ili kulishughulikia hilo kwani inaweza kumchafua sana,

lulu huyo feki anatumia jina la Elizabeth Michael lulu na pia anatumia picha za lulu na anachati na watu kama lulu na hata pesa anazotumiwa anazipokea kama lulu sasa wadau mbali mbali wakichangia hili wameonyesha kukerwa sana na jambo hilo na kuahidi kumshughulikia mtu huyo

Hebu angali hapo chini mwenyewe utaona kila kitu

Elizabeth Michael Lulu

TUMEONGEZA NAFAC 15 ZA KUSAJILI WASANII WACHANGA. PIGA sasa 0716085715 USAJILI

Mtega Semeni wasanii waliokomaa na kubobea ni akina nani na wako wapi hapa Tanzania?
5 hours ago · Like · 2

Godi Mponzi Hakuna mtu ambaye hapendi kutoka kimaisha bongo. Unapo amua kutoa kitu to mass ili uonekane tu is a fool. Inatakiwa serious na unacho kifanya sio kelele kwenye mtandao ili uonekane, we need material or ideological support and critical argument which can equipe and libarate our human mind.
4 hours ago via mobile · Like · 1

Godi Mponzi Hakuna mtu ambaye hapendi kutoka kimaisha bongo. Unapo amua kutoa kitu to mass ili uonekane tu is a fool. Inatakiwa serious na unacho kifanya sio kelele kwenye mtandao ili uonekane, we need material or ideological support and critical argument which can equipe and libarate our human mind.
4 hours ago via mobile · Like

LULU AONYESHA PICHA YA FILAMU YAKE MPYA TOKA APATE DHAMANA......JOKET AWA WA KWANZA KUMPONGEZAKALI ILIOMKUTA PREZZO: AUMBUKA BAADA YA PICHA YAKE YA UTUPU KUVUJA, ICHEKI PICHA HIYO HAPA!Jackson Makini a.k.a. Prezzo is in trouble…..on Saturday after the release of his new and controversial track Liqher, his n*ked photos enjoying some private time with two lasses were leaked to the internet.

Check out the first PHOTO>>>

Source:Daily post

Sunday, April 21, 2013

WABUNGE WACHACHAMAA JUMBA LA MCHUNGAJI LWAKATARE LIVUNJWE

'Hekalu' linalomilikiwa na Mchungaji Getrude Lwakatare.

Wabunge wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya kwamba kuna zuio la mahakama.
Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.

Sambamba na hilo wametaka watendaji wa serikali waliohusika kutoa vibali kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe hatua.

Mbunge wa kwanza kuanza kuzungumzia hilo ni wa viti maalum, Esther Bulaya (CCM) aliyetaja viwanja viwili vyenye namba 2019 na 2020 kikiwemo cha mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani waliojenga nyumba zivunjwe licha ya kuwepo zuio la mahakama.

“Mwaka jana waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka alivunja nyumba za kawaida licha ya zuio la mahakama, lakini nyumba zilizo kwenye viwanja namba 2019 na 2020 hazikuvunjwa kwa sababu ya zuio la mahakama hii ni double standard hatuwezi kuvumilia.

“Wengine wenye nyumba ni viongozi tupo nao humu tena wa kiimani, lakini kwa nini viongozi tunafaya hivi wakati tunatakiwa tuwe wa mfano na tunawafanya viongozi wenzetu washindwe kufanya kazi zao?…hakuna haja ya kuogopa waziri Huvisa (Mazingira) vunja nyumba, haiwezekani kuwa na nguvu ya fedha.

“Wabunge wenzangu tuazimie Manispaa ya Kinondoni na NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), wakavunje nyumba hizo ndani ya wiki moja , naomba kutoa hoja,” alisema.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimweleza; “Haiwezekani kutoa hoja kwa kuingilia vyombo vingine”.

Mbunge ambaye ni kiongozi wa kiimani mwenye nyumba katika eneo hilo la Mbezi Beach aliyejenga katika fukwe ya bahari kwa kuondoa mikoko na kuweka kifusi na kujenga nyumba ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare (CCM).

Naye Mbunge wa viti maalumu, Grace Kiwelu (Chadema) akichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alisema kamati yake ya Ardhi na Mazingira ilitembelea eneo hilo la Mbezi Beach na kukuta aliyejenga katika kiwanja 2019 hakuwa na ofa wala hati.

“Ametumia pesa kuwarubuni watendaji akaondoa mikoko, akaweka kifusi na akajenga nyumba naomba wizara ya Ardhi na ya mazingira wawachukulie hatua watendaiji hao,” alisema.

Akijibu hoja ya Bulaya, kuwa kwanini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuvunjwa wakati nyingine zilivunjwa, mwanasheria mkuu wa Serikali, Frederick Werema alisema:

“Sisi ni wajibu wetu twende mahakamani kusema watu hao wamevunja sheria kujenga hapo. Wao wanaruhusiwa na Katiba na mahakama itafuata sheria.

“Nashauri Bulaya usitoe shilingi kuzuia Bajeti ya Waziri, uje tuone huyo kigogo itakuwaje.”

Hata hivyo, Huvisa alisema: “Nyumba tulizovunja hazikuwa na kesi na hii tuliyoiacha ilikuwa na kesi.”

Jumba la kifahari linalodaiwa kuwa la Mchungaji Lwakatare ambalo lilizinduliwa mwaka jana, limekuwa klikitajwa kuwa lina thamani ya takribani sh bilioni 1.5.

zero99

EXTRA BONGO KUTAMBULISHA WAPYA TANGA.

Bendi ya Extra Bongo inatarajia kutambulisha wasanii wapya hivi karibuni  ndani  ya April 30 itakuwa ndani ya Mamba Club Same , na siku ya Mei Mosi itakua katika   Ukumbi wa Tanga Hotel  ambapo   itamalizia Korogwe na kurudi Dar Ijumaa May 3  itahitimisha ndani ya Mango Garden Kinondoni jijini Dar  kwa kuwatambulisha wanamuziki wawili wapya kutoka kwenye bendi pinzani.Friday, April 19, 2013

RAIS UHURU KENYATTA AMEITANGAZA STRUCTURE YA SERIKALI YAKE KUWA NI HII
President Uhuru Kenyatta unveils the structure of his Government, In exercise of the authority vested in him by the Constitution of Kenya 2010 and in conformity with the expectations of a lean and effective structure, President Kenyatta officially released the list of ministries and state departments that will form the National Executive as follows:
Under the Presidency, there will the Executive Office of the President and the Executive Office of the Deputy President with two ministries:
Ministry of Interior and Coordination of National Government.
Ministry of Devolution and Planning.
Other ministries are: 3. Defence 4. Foreign Affairs. 5. Education which will have the Department of Education and Department of Science and Technology 6. The National Treasury 7. Health 8. Transport and Infrastructure which will have the Department of Transport Services and the Department of Infrastructure.

9. Environment, Water and Natural Resource 10. Land, Housing and Urban Development 11. Information, Communication and Technology (ICT) 12. Sports, Culture and the Arts 13. Labour, Social Security and Services 14. Energy and Petroleum 15. Agriculture, Livestock and Fisheries under which are the Department of Agriculture, Department of Livestock and Department of Fisheries 16. Industrialization and Enterprise Development.
17. Commerce and Tourism which has the Department of Commerce and Department of Tourism 18. Mining, The structure also contains the Office of the Attorney General and Department of Justice.
In the new structure, President Kenyatta has collapsed the ministries from 44 to 18. The reduced structure is geared towards achieving a lean, efficient and effective executive branch of Government.

In the structure, the President has given special focus to the youth, gender, devolution, planning as well as national cohesion and integration which have all been brought under the Presidency.
Also given special focus is mining which is now a stand-alone ministry. Information, Communication and Technology ministry as well as Sports, Culture and Arts are also stand-alone ministries with a view to leveraging on the creative potential of the youth. Infrastructure ministries as well as national resources ministries have also largely been brought under the same roof.

DUME LAJIBADILISHA NA KUWA KAMA MWANAMKE ! HII DUNIA DAH!Yep, all that used to be male. Her name is Amiyah Scott, but she was born ‘Arthur Scott’ in New York in 1988. She's a transgender model and make-up artist. Arthur started the process of turning into a woman when he was 17. He got breast augmentation, booty shots, light filler in the cheeks etc etc. See more photos of her/him after the cut...
 
Arthur Scott turns to Amiyah Scott

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...