Mrembo aliyenusulika kuuwa na kipigo cha chupa kutoka kwa Jack Patrick, akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kushonwa nyuzi tatu.
STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa
na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina
la Hafsa Sasya, Risasi Mchanganyiko linanashuka nayo.
Habari
zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba,
ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani
ya Ukumbi wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.
CHANZO KINATIRIRIKA
Huku sharti la kutotajwa jina lake gazetini
likisisitizwa na chanzo hicho, kilisema: “Unajua yule dada (Hafsa)
anasoma Kurasini na anaishi Kijitonyama, namfahamu vizuri sana.
Walipokutana na Jack pale ukumbini palitokea kutokuelewana kidogo.
“Baada ya muda hali ikawa sawa, watu wakajua yamekwisa. Jack
akaenda zake chooni, aliporudi alikuwa na chupa na kwenda kumpiga nayo
Hafsa. Mabaunsa wakamwondoa Jack ukumbini na kumwingiza Hafsa kwenye
gari lake kwa lengo la kumpeleka hospitalini. Kilichoendelea hapo
sijui.”
PEKUPEKU ZA RISASI
Mwandishi wetu aliingia mzigoni rasmi na
kuanza kuichimba kwa kina habari hiyo ambapo alipata uhakika wa kutokea
kwa tukio hilo na Jack kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay
ambapo alifunguliwa kesi yenye jalada namba OB/RB/1678/13 KUJERUHI.
Baada ya kujiridhisha kwa hilo, zoezi lililofuata lilikuwa ni
kuwatafuta wawili hao ili waeleze wanachokijua kuhusu tukio hilo. Wa
kwanza kupatikana alikuwa ni Jack.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku
ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini
nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”
HUYU HAPA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa
amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile
alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha
akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa;
akanipiga na chupa.
“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya
msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa
sheria, naamini itachukua mkondo wake.”
Mrembo anayekwenda kwa jina la Hafsa akiwa katika hali mbaya muda mfupi baada ya kushushiwa kipigo kikali na Jack Patrick