Saturday, June 30, 2012

UZINDUZI WA SOBBING SOUND NA WATOTO YATIMA

Source: Ray The Greatest

Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuizindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio, Kwanini nimeamua kufanya hivi wadau ni kwa sababu nimeguswa na jinsi wanayoishi watoto yatima katika mazingira magumu ili ni jukumu la Watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini. wadau sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba unaambiwa kuwa kama utoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho...Hivi ni baadhi ya vitu nilivyowapelekea watoto wa kituo hicho wadau kutoa si utajiri bali ni moyo na nimeamua kila sinema yangu inapotoka basi lazima nirudishe shukrani zangu kwa Watanzania wa hali ya chini nitaanzia Dar es salaa na baadaye mikoani wadau ..Watoto wa kituo hicho wakiwa wametulia kufuatilia kinachoendelea..Waandishi wa habari kutoka vituo tofauti walikuwepo kuchukua habari kama kawaida ya wanahabari panapokuwa kuna tukio.Pritesh toka Steps kampuni ya usambazaji hapa nchini alikuwepo kunipa tafu katika jambo ili la kuwasaidia watoto yatima..The Greatest(Ray) nikiwa nimewasili katika kituo cha watoto yatima cha Maunga nikimsikiliza mama mlezi wa kituo hicho.

Mama mlezi wa kituo hicho akiongea machache pamoja na kunishukuru.


Nami nilipata fursa ya kuongea ya kwangu.Zoezi la makabhiano yalianza kama ifuatavyo, hapa nikimkabidhi Mama mlezi kiroba cha unga..Mambo yakiendelea...Nikiendelea na taratibu za kutoa msaada.Niliweza kutembelea maeneo wanapolala ndugu zangu na kama mnavyoona wadau tunahitaji kujitoa kuwasaidia ndugu zetu..
Na hichi ndio choo chao embu angalieni jamani hii n hatari sana kama utakuwa na chochote ama umeguswa kusaidia basi tunaweza kuwasiliana.

Baada ya matukio yote nilipewa nafasi nyingine ya kusaini kitabu cha wageni.


Niliweza kupata picha ya pamoja na watoto hao.


Hapa nikiongea na vyombo vya habari..


Nikipokea shukurani yao.
`Nilifurahi sana kwa kupata nafasi kubwa ya kufika katika kituo cha watoto yatima na hapa wakinisindikiza.

Thursday, June 28, 2012

HIZI HAPA PICHA ZA TWIGA WA TANZANIA ALIYETOKA KWENYE MTANDAO WA UK “DAILY MAIL” AKIOGELEA KTK SWIMMING POOL YA CLUB KILIMANJARO.

Akiwa ni Twiga pekee katika eneo la Kilimanjaro Golf and Wildlife Estate, Tanzania. Alipewa jina la Monduli miaka mitatu iliopita alipowasili katika club hiyo na sasa ana miaka mitatu na nusu.

Mkurugenzi wa estate hiyo, Zummi Cardoso amesema Monduli ana urefu wa ft 13(4m) na anatarajiwa kufikia ft 18 atakapofikisha miaka sita.

Monduli aliingia katika bwawa la kuogelea na kuweka kichwa juu, kitu kisichoshangaza sana kutokana na urefu wa twiga.
SERENGETI FIESTA 2012 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR.

Mmoja wa Waratibu wa maandalizi ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 (pili kulia) Sebastian Maganga akifafanua baadhi mambo mbele ya wageni waalikwa wakiwamo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha hilo uliofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinodoni jijini Dar leo,tamasha hilo linatarajia kutimua vumbi zake hivi karibuni katika mikoa mbalimbali,ambapo katika tamasha hilo mdhamini mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake Serengeti Premium Lager,Kampuni ya mafuta ya Gapco pamoja na Push Mobile.Kauli mbiu ya tamasha hilo ni "MUONEKANO MPYA-BURUDANI ILELE-BAAAS"!
Sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ikiwemo Magari aina ya Toyota Vitz kila moja yenye thamani ya shilingi milioni nane,Piki piki a.k.a Boda Boda 14 kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na nus na zawadi nyingine zikiwemo simu aina ya blackberry,Nokia.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya lidaz Club,jijini dar.
Mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa umakini na kuweka misisitizo kwa Wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha hilo.
Sebastian Maganga kutoka Clouds Media Group akiwatambulisha Wadhamini wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kutoka kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya mafuta ya Gapco,Ben Temu,Meneja wa kinywaji cha Serengeti kutoka SBL,Allan Chonjo pamoja na muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile,Bw.Rodney
Meneja wa bia ya Serengeti kutoka kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012,Allan Chonjo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa wakiwemo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,uliofanyika leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,jijin Dar.
Bw.Rodney ambaye ni muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile akionesha moja ya namba zitakazotumika kutoa taarifa mbalimbali za tamasha hilo litakaloanza kutimua vumbi zake kuanzia hapo kesho katika mikoa ya Arusha na Mbeya na baadaye mikoa mingine.
Pichani shoto ni Meneja mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bw.Iman Lwinga akiwa sambamba na baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wageni waalikwa wakiwemo wasanii kadhaa bia walifika kushudia tukio hilo kubwa la kihistoria katiak tasnia ya burudani hapa nchini.
Wakifuatilia kwa umakini zaidi.
Kwa mshangao mkubwa wakishuhudia uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Lidaz Club.
Wadau wakifuatilia uzinduzi huo,akiwemo Shaffih Dauda mzee wa sports bar.
Meneja wa vinywaji vikali wa SBL,Bw.Emillian Rwejuna akizungumza na Meneja wea kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mwasiti kuhusiana na tamasha la fiesta kwa ujmla.
Wadadazi nao walikuwepo kunogesha uzinduzi huo wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

Msanii wa Uganda, Jose Chameleone (pichani juu) jana alikamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa Taifa mpya, jijini Dar es salaam, siku ya sabasaba baada ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, kutia timu Entebe jana. Pichani juu ni Chameleone akijigamba kufanya shoo na akisaini mkataba wa mwisho huku akishuhudiwa na meneja wake. Chameleone ametoa onyo kwa Diamond kuwa atamchakaza na Valuvalu!

Monday, June 25, 2012


KALALA JUNIA NDANI YA EXTRA BONGO

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky(kulia) akiimba sambamba na waimbaji wake wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam

Wacheza shoo wakicheza

Rapa Mkuu wa Bendi ya Extra Bongo, Frank Kabatano akiimba wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam

Mpiga Rythm, Mfaume Zablon akilichakaza Gitaa wakati wa onyesho hilo

Mpiga Tumba, Salum Chakuku akiwajibika wakati wa onyesho hilo.

Wacheza shoo wakicheza
Mpiga Solo, Adam Hassan akiwajibika katika kutua burudani

Chocky na waimbaji wake wakiimba

Mpiga Drums,Martine Kibosho akiwajibika wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam

Ally Chocky na wadau wa muziki,kutoka kulia ni Kalala Junia,Ndanda Kossovo
Wacheza shoo wakicheza
Mwalimu wa Waalimuni,Banza Stone akiimba
Wakicheza staili ya Katelelo


Wakicheza
Mtaalamu wa kila chombo cha muziki, Sebastian Ngosha akilichalaza Bass
 
Kiongozi wa wacheza shoo wa kike, Otilia Boniphace akionyesha manjonjo

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...