Saturday, June 30, 2012

UZINDUZI WA SOBBING SOUND NA WATOTO YATIMA

Source: Ray The Greatest

Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuizindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio, Kwanini nimeamua kufanya hivi wadau ni kwa sababu nimeguswa na jinsi wanayoishi watoto yatima katika mazingira magumu ili ni jukumu la Watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini. wadau sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba unaambiwa kuwa kama utoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho...Hivi ni baadhi ya vitu nilivyowapelekea watoto wa kituo hicho wadau kutoa si utajiri bali ni moyo na nimeamua kila sinema yangu inapotoka basi lazima nirudishe shukrani zangu kwa Watanzania wa hali ya chini nitaanzia Dar es salaa na baadaye mikoani wadau ..Watoto wa kituo hicho wakiwa wametulia kufuatilia kinachoendelea..Waandishi wa habari kutoka vituo tofauti walikuwepo kuchukua habari kama kawaida ya wanahabari panapokuwa kuna tukio.Pritesh toka Steps kampuni ya usambazaji hapa nchini alikuwepo kunipa tafu katika jambo ili la kuwasaidia watoto yatima..The Greatest(Ray) nikiwa nimewasili katika kituo cha watoto yatima cha Maunga nikimsikiliza mama mlezi wa kituo hicho.

Mama mlezi wa kituo hicho akiongea machache pamoja na kunishukuru.


Nami nilipata fursa ya kuongea ya kwangu.Zoezi la makabhiano yalianza kama ifuatavyo, hapa nikimkabidhi Mama mlezi kiroba cha unga..Mambo yakiendelea...Nikiendelea na taratibu za kutoa msaada.Niliweza kutembelea maeneo wanapolala ndugu zangu na kama mnavyoona wadau tunahitaji kujitoa kuwasaidia ndugu zetu..
Na hichi ndio choo chao embu angalieni jamani hii n hatari sana kama utakuwa na chochote ama umeguswa kusaidia basi tunaweza kuwasiliana.

Baada ya matukio yote nilipewa nafasi nyingine ya kusaini kitabu cha wageni.


Niliweza kupata picha ya pamoja na watoto hao.


Hapa nikiongea na vyombo vya habari..


Nikipokea shukurani yao.
`Nilifurahi sana kwa kupata nafasi kubwa ya kufika katika kituo cha watoto yatima na hapa wakinisindikiza.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...