Tuesday, August 12, 2014

HUDDAH MONROE NA PICHA ZAKE ZA UTUPU INSTAGRAM

MREMBO kutoka nchini Kenya Huddah Monroe, ameendelea kutupia picha zake za 'utupu' kupitia mtandao wa Instagram kama kawaida yake.Staa huyo ambaye kwa sasa yupo Abuja nchini Nigeria ametupia picha zake akijiachia na mavazi ya kuogelea huku nyingine akiwa na mwenzake.


MCHEKESHAJI MAARUFU WA MAREKANI AJIUA

Muigizaji na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams amejiua. Mwili wake umekutwa nyumbani kwake California, Marekani Jumatatu Agosti 11, 2014.
Muigizaji na mchekeshaji maaarufu wa Marekani, Robin Williams enzi za uhai wake.
Robin Williams akiwa na mke wake wa tatu, Susan Schneider.
Maua na ujumbe wa kumkumbuka Robin Williams.
Imeelezwa kuwa kwa siku za hivi karibuni Williams ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 63 alikuwa akipambana na sonona.
Muigizaji huyo alikuwa hajitambui na hakuwa anapumua na hivyo kubainika kuwa alijiua kwa kukosa hewa. Williams alionekana nyumbani kwake mara ya mwisho mida ya nne usiku siku ya Jumapili.
Robin alipelekwa rehab mwezi uliopita kujizuia kunywa pombe. Alikuwa akihangaika kuacha kutumia cocaine na pombe katika miaka ya 80 lakini hakuwahi kunywa kwa miaka 20.

WAPAKISTANI WALIO KAMATWA NA UNGA DAR WATOROKA

Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa  wakiwa  na  Watanzania  wanaotuhumiwa kwa kukutwa  na  madawa ya kulevya wametoroka nchini.
 Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.
Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2,  Mbezi Beach  maeneo ya  Jogoo  jijini Dar sa Salaam.
Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi  hiyo  inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa  kwa  watuhumiwa  hao.
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa  na  kikosi  kazi  cha  kuzuia na kupambana na madawa  ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Mtuhumiwa Shahbaz Malk.
Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia.
Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani  hapo.
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa hao yenye thamani ya shilingi  bilioni 6.2.
Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.
Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...