Friday, August 19, 2016

KESSY ARUHUSIWA KUKIPIGA YANGA RASMI!Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji imepitisha usajili wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha jina la mchezaji Hassan Kessy kuichezea Young Africans. Hii ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas. 
Kessy alikuwa katika mgogoto mzito kutokana na kile kilichodaiwa kusajiliwa na Yanga kabla hajamalizana na Simba, hali ambayo ilifanya Simba kukataa kutoa barua ya uthibitisho kuwa imemalizana na Kessy.
Kitendo cha Simba kutoandikiwa barua hiyo kimesababisha akose mechi za kimataifa licha ya kuwa katika kikosi cha Yanga kwa wiki kadhaa.

Jumatano iliyopita alicheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kitendo ambacho kililalamikiwa na baadhi ya wadau wa Simba na Azam ambao walidai kuwa inakuwaje TFF inamruhusu kucheza wakati usajili wake haujakamilika.

Kuruhusiwa kwa Kessy sasa kutamfanya mchezji huyo kuwa huru kuitumikia Yanga katika msimu mpya wa 2016/17 unaotarajiwa kuanza wikiendi hii.


Habari ya Kessy kuruhusiwa kuichezea Yanga ni neema kubwa kwa kocha wake, Hans van Pluijm ambaye amekuwa akihitaji huduma yake lakini alikuw akiikosa kutokana na mgogoro huo

Thursday, August 18, 2016

SIMBA SC. YAWEKA SOKONI MAJI YAKE!

Maji mapya  ya simba simba ambayo yanaandaliwa kwaajili ya kuwafanya mashabiki waichangie timu yao.

Wednesday, August 17, 2016

AZAM FC ILIVYOITOA NISHAI YANGA NA KUTWAA NGAO YA JAMII


Azam FC wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Jamii kwa uifunga Yanga kwa penati 4-1, leo kwenye Uwanja wa Taifa baada ya timu hizo kumaliza kwa sare ya mabao 2-2.

Yanga ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata mabaop yake kupitia kwa Donald Ngoma ambapo mpaka dakika 45 zinakamilika matokeo yalikuwa 2-0 lakini kipindi cha pili hali ilibadilika na Azam kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shomari Kapombe na John Bocco.

Hivi sasa msimu wa 2016/17 umefunguliwa rasmi ambapo mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarakiwa kuanza wikiendi ijayo katika viwanja tofauti.

 


Tuesday, August 16, 2016

BASATA YAFAFANUA KUHUSU NAY WA MITEGO KUTOKA KIFUNGONI


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungulia Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego kuendelea na shughuli za Sanaa baada ya kuwa ametekeleza adhabu (maagizo) zote alizopewa kama masharti ya kumfungulia.

Aidha, BASATA kama mlezi wa wasanii linamfungulia kufuatia yeye mwenyewe (Nay wa Mitego) kujutia na kukiri kwamba amejifunza na yuko tayari kubadilika na kwamba hatarudia makosa aliyoyafanya.

Hata hivyo, pamoja na kumfungulia kuendelea na shughuli za Sanaa Baraza linamweka kwenye uangalizi maalum msanii huyo kama sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za Sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu sambamba na kuzingatia maadili katika kazi zake.

Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/07/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:

1.      Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na  kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa

2.      Kulipa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000/-)

3.      Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari na kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii

4.      Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’  ili ubebe maudhui yenye maadili.

Msanii Nay wa Mitego ametekeleza adhabu zote tajwa hapo juu. Leo hii tunamkabidhi rasmi cheti chake cha usajili na kibali cha BASATA. 

Hata hivyo, pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekebisho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huu hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili.
 Katika kikao na Msanii Nay wa Mitego cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa adhabu yake kilichofanyika tarehe 12/08/2016 Ofisi za BASATA ameagizwa kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado anaona anauhitaji.

Baraza linatoa maelekezo kwa vyombo vya habari na watanzania kwa ujumla kuacha kuucheza wimbo huo hadi hapo itakapoelekezwa vinginevyo. Hatua na adhabu za kisheria zitachukuliwa kwa chombo chochote cha habari kitakachokiuka agizo hili.

Aidha, katika kikao hicho cha tathimini ilibainika kwamba Msanii Nay wa Mitego kwa taarifa potofu alizopewa alipanda Jukwaani kwenye tamasha la Mwendo Kasi la tarehe 30/07/2016 akiwa katika adhabu.

Kwa kosa hili ameandika barua ya kuomba radhi na Baraza linafikiria hatua za kuchukua kwa waandaaji wa tamasha hili.
   


Baraza linatoa wito kwa wasanii kuendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji shughuli za Sanaa sambamba na kuhakikisha wanazingatia maadili katika kila kazi wanazobuni ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima ambayo yanaathiri kazi zao kwa kiasi kikubwa sana.

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

MBUNGE MAHAMOOD MGIMWA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASIKAZINI


Na Fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu  za Jimbo hilo huku akitaka michezo yote kuendelezwa.

Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni  kutokana na ahadi yake  yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku  baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa.

Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
  
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikagua baadhi ya maeneo ambapo michezo hiyo itafanyika.

Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo.


Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.

Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi  na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.

Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...