Friday, March 29, 2013

HIVI NDIVYO GHOROFA LILIVYOANGUKA POSTA JIJINI DAR.


Hiki ndicho kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15.

LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi Watanzania wameingia kwenye vilio baada ya jengo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam, kuanguka na kuwafunika watu waliokuwa eneo hilo na kusababisha wengine kupoteza maisha. Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani yake, ila watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa.

Winchi likiokoa mabaki ya moja ya gari lililoangukiwa na kifusi.

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiangalia hali ya uokoaji inavyoendelea.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuondoa kifusi eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) akifuatilia shughuli ya uokoaji.
Watu mbalimbali wakiondoa kifusi.
Askari aliyejuu ya farasi akihakikisha usalama eneo hilo.
Baadhi ya watu wakilisukuma gari ambalo pia lilikuwa kwenye ajali hiyo.
Mama Salma Kikwete (kulia) na Rais Kikwete wakiangalia kifusi.
Kijana aliyenusurika katika ajali hiyo akinywa kahawa.

Thursday, March 28, 2013

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefarikizishiMbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa ma zinafanyika.

ROSE GODWIN KUTOKA ARUSHA ATWAA TUZO YA SJMC MISS TOURISM TANZANIA 2012/13-MEDIA AWARD,AZAWADIWA KUSOMA CHUO KIKUU.Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya Tatu Baby Juma kutoka mkoa wa Mtwara Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye 

Fainali za Utalii Tanzania zimeendelea kushika kasi kwa warembo kushindania Tuzo mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Jamii na za Kuichumi. Jana lilifanyika Shindano la kumpata Mshindi wa Tuzo ya Habari (Media Award) , Shindano ambalo liloifanyika katika Viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma (SJMC) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo.

Katika Shindano hilo la Miss Utalii Tanzania 2012/13 Media Award zaidi ya Warembo 30 walipanda jukwaani kwa kuelezea mada ya vivutio vya Mikoa wanayo wakirisha na kisha Majaji wa Shindano hilo kutoka Shule Kuu ya Waandishi wa Habari na mawasiliano ya Umma walitangaza warembo Sita walioingia katika Sita Bora na Baadae waliulizwa Maswali kila mmoja na swali lake na pia swali la pili lilikuwa ni Swali la Jumla ambapo wote waliulizwa. Washiriki wote walijibu kwa umahili na baadae wakapatikana washindi watatu ambapo Mshindi wa kwanza alikuwa ni Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin, Mshindi wa Pili alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi na Mshindi wa tatu alikuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara Baby Juma.

Mshindi wa Tuzo hiyo ya Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award kutoka Mkoa wa Arusha Rose Godwin Alipata zawadi ya Udhamini wa kusomeshwa katika Shule Kuu hiyo ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kutoa Tuzo, Rais wa Miss Utalii Tanzania Aliwashukuru Wadhamini wakuu wa Tuzo hiyo ya SJMC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Awards, ambao ni Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma kwa kutoa Heshima kubwa ya Kumsomesha Mshindi wa Tuzo hiyo katika chuo hicho na kuongeza kuwa Elimu ndio Ufunguo wa Maisha na Hilo ni Jambo muhimu katika Taifa letu la Tanzania ambapo Wasomi zaidi wanahitajika ili Kujenga Taifa na Kukuza Uchumi wa nchi yetu. 


Mshindi wa SMJC Miss Tourism Tanzania 2012/13 Media Award nafasi ya pili kutoka Mkoa wa Rukwa Neema Kafanunzi Akikabidhiwa Zawadi ya Ua na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye

Mshindi wa Tuzo ya Media ya Awards kutoka mkoa wa Arusha(katikati) akiwa na wenzake baada ya kutangazwa mrembo wa Vyombo vya Habari vya SJMC Radio, Tv na Magazeti, hafla ambayo imefanyika kwenye ofisi za Chuo Kijitonyama jijini Dar es salaam. Fainali za Miss Utalii zitafanyika tarhe 6/4/2012/13 katika Viwanja vya Makumbusho.

Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye (wa pili kulia), akiwa na Washindi wa watatu wa Tuzo ya Media Awards ya chuo hicho, katikati ni mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka katika Mkoa wa Arusha.

Rais wa Miss Utalii Tanzania wa Kwanza kutoka upande wa kushoto Ndugu Erasto G. Chipungahelo Akiwa Na washindi watatu pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye.

Meneja vyombo vya habari vya Mlimani-Mama Edda Sanga(kati) Susanne Mbise(kushoto)na Afisa Masoko wa SJMC Sophia Ndibalema(kulia) wakiwa na Mshindi wa Miss Utalii Tanzania-Tuzo ya Media Awards kutoka mkoa wa Arusha, muda Mfupi baada ya kutangazwa katika Hafla iliyofanyika katika Chuo cha SJMC.

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya kutangazwa kwa Mshindi wa tuzo ya SJMC Media Award

Jopo la majaji wakiwa katika Picha ya Pamoja

Rais wa Miss Utalii Tanzania Ndugu Erasto G. Chipungahelo akitoa neno la Shukurani kwa Mwalimu Mkuu wa Shule kuu ya Chuo Cha Uhandishi wa Habari SJMC, Drk. Herbert Makoye ofisini kwake

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakitumbuiza Ngoma za asili wakati wa utoaji wa Tuzo hiyo.

Washindi sita wakiwa katika Picha ya Pamoja

"RAYUU ANENA MAKUBWA KUHUSU SINTAH!


 Rayuu 
Katika kile kinachoonekana kuwa ni mwendelezo wa ugomvi wa Sintah na Rayuu, wasanii hawa wameendelea kurushiana matusi ya nguoni na kuumbuana kila siku......

Sintah aliwahi mtuhumu Rayuu kuwa ni kahaba mwenye kiwango na aliyeshindikana.Tuhuma hizo zilikuja baada ya picha za uchi za msanii Rayuu kuvuja mtandaoni zikionesha makalio na matiti yake.....


Sintah

Baada ya tuhumu hizo, Rayuu naye ameendelea kufichua mambo mengi kuhusiana na Sintah kwa kudai kuwa Sintah ni kahaba na haoni aibu maana umri wake umeenda....


Rayuu anadai kuwa ukahaba ulimfanya Sintah aachwe na Juma Nature.Msanii huyu ameenda mbali zaidi baada ya kudai kuwa amewahi muona Sintah kwa macho yake akijiuza maeneo ya Manzese.....


Wednesday, March 27, 2013

MEYA WA ILALA MH.JERRY SILAA AZINDUA ZIARA YA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA KIHISTORIA NDANI YA MANISPAA YAKEMmoja wa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 , kutoka Kanda Maalum ya Zanzibar akitoa Shukurani kwa niaba ya Warembo wenzake.

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika Picha ya pamoja na Muheshimiwa Meya wa Manispaa Jerry Silaa

Washiriki wa Miss Utalii Taifa 2012/13 wakiwa na Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Ilala Bi. Shani wa kwanza kushoto, ambaye ndiye alikuwa anatoa maelezo yote ya kina kuhusiana na eneo hilo Muhimu kwa Taifa la Tanzania

LOWASA AONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI MAZISHI YA NYITI ARUSHAMh Lowassa akiongoza viongozi kwenda kwenda kuweka udongo kaburini,nyuma yake ni Waziri wa mambo ya nje Mh Bernard Membe.

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakati wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kanda maarufu wa CCM Mkoani Arusha Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha.


Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine waliyoudhuria Ni pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe,Naibu Waziri wa maliasili na utaalii Lazaro Nyalandu,mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr Reginald Mengi,Mkuu wa mkoa wa Arusha, mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.


Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa pia alikwenda kutoa pole katika msiba wa Moja wa wazee maarufu eneo la Mto wa Mbu, mzee Athman.

Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akiweka udongo

Mh Lowassa akisalimiana na Mh Mbowe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akiweka shada la maua

TID ASIKITISHWA NA UGOMVI WA CHID BENZ NA NGWAIR


Mashabiki wa Bongo Flava wiki hii walisikitishwa na taarifa za Chidi Benz kumpiga mshikaji wake Ngwair. Katika tukio hilo lililotokea Ambassador Lounge jijini Dar es Salaam, Ngwair alidaiwa kujeruhiwa na chupa.

Tukio hilo lilimsikitisha pia mshkaji wao mwingine, Khalid Mohamed aka TID ambaye kwa mujibu wa U Heard ya Clouds FM, alipiga kioo cha gari yake kwa hasira.

“Hawa jamaa wanapigana pigana tu, me wananiudhi unajua kwanini , kwanini wao wanapigana pigana kila saa tu, huyu mara kampiga huyu and we all spend time together, at the end of the day wao wanaanza kupigana, mimi wananiconfuse, wananipotezea concentration ya kazi,” alisema TID.

“Hakuna sababu ya msingi watu wanapigana tu, watu wanongea saa zote tupo wote halafu baadae unaona watu wanaanza kupigana, unauliza sababu eti huyu kanambia mi dogo.. come on man. Mi nimewamind wote wanaopigana na ku disturb peace kwenye concentration ya kazi, violence inaonyesha sisi ni wajinga.”

Hata hivyo Chidi Benz aliendelea kusisitiza kuwa hakumpiga Ngwair. “Nani anaeamini Ngwea kapigwa? Y nimpige na ni mtu niko nae kila siiiku mabatani, tumefanya kazi nyiingi na tuna mipango,tafadhali usishabikie kitu na ukajiona mjinga mwishoni,” aliandika Chidi kwenye akaunti yake ya Facebook.

“Kuhusu swala la Ugomvi kati ya mimi na Mangwea naomba lisikuzwe ikaonekana ni sababu najua wabaya wangu watavyoweza kulikuza hili.hatuna Ubaya na ngwea na ni boonge la mshkaji..tusameheane haya Maisha tunatafuta.Peace, no lie.”

HUYU NDIYE MKE ANAYELALAMIKA KUIBIWA MUME NA 'JACK CHUZ' ALIYEFUNGA NDOA HIVI KARIBUNI


ZENGWE limeanza! saa 48 baada ya Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na jamaa aitwaye Gadna Dibibi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Omary ameibuka na kudai muoaji ni baba mtoto wake wa miezi minne hivyo anamuomba msanii huyo amwachie mumewe.


Mariam Omary anayedai Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kamchukulia baba watoto wake akiwa na mwanaye.

Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya kuenea kwa habari za Jack Chuz kufunga ndoa na kijana huyo wikiendi iliyopita, ndipo ilipogundulika kuwa ana mwanamke ambaye wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani miaka mitatu na wana mtoto huyo mmoja wa kiume.

Baada ya ripota wetu kuidaka ishu hiyo aliingia mzigoni kutafuta ukweli wa jambo hilo ndipo akakutana na mwanamke huyo aishie Kigogo, Dar ambapo alikutwa akiwa anambembeleza mtoto huyo anayeitwa Price Laden.

Akifunguka mbele ya mwandishi wetu, Mariam alidai kwamba siku ambayo mwanaume huyo alifunga ndoa (Ijumaa), alimuaga anasafiri kwenda Morogoro hivyo hatakuwepo Dar lakini wanusaji wa mambo ya watu walishampa ‘infomesheni’ kwamba anafunga ndoa na Jack Chuz.


“Unajua mtu atakunyima ugali ila siyo maneno, nilishajua na nilikuwa namwangalia tu nione atasemaje,” alisema.

Mariam aliendelea kutiririka kwamba anamjua vizuri Jack Chuz linapokuja suala la wanaume wa wenzake lakini kwake atachemsha kwa kuwa msanii huyo anajua kila kitu juu ya uhusiano wake na mwanaume huyo ambaye ni halali yake.

“Hakuna asichokijua kati yangu na Dibibi, kwa usalama wake Jack aniachie mume wangu,” alilalama mwanamke huyo.

Baada ya kuzungumza na Mariam, mwandishi wetu alimvutia waya mume wa Jack na kusomewa mashitaka yake ambapo alisema kuwa baba wa mtoto anayemjua ni mama peke yake na isitoshe kuzaa naye isiwe sababu kwani yeye hakumuoa.

“Alikuwa demu wangu na kuzaa mtoto isiwe sababu. Hata hivyo, ukweli wa baba wa mtoto anayejua ni mama. Sikumtolea mahari wala kumvalisha pete ‘so’ hana kizuizi na ndoa yangu,” alisema jamaa huyo kisha akakata simu.

CHADEMA WAPOKEA MSAADA WA MILIONI 400Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kutoka Chama cha Upinzani nchini Denmark cha Conservative People’s Party (CPP), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. WILBROAD SLAA amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanachama wake kupitia Baraza la Vijana la Chama hicho, (BAVICHA), pamoja na lile la Wanawake (BAWACHA), inatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Conservative People’s Party (CPP), ROLF AAGAARD, anaelezea lengo la chama hicho kutoa msaada huo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), JOHN HECHE amesema msaada huo utawawezesha kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Baraza hilo katika mikoa mbalimbali nchini.

Chama cha Conservative People’s Party (CPP), kilianzishwa mwaka 1915 na kimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu hadi kiliposhindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini.

ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA AFIKISHWA MAHAKAMANIMtuhumiwa akiwasili mahakamani
 
Jackson Simbo anayedaiwa kumgonga kwa gari marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar ss Salaam amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huuAkiteta jambo na Issa Mnally ndani ya mahakama kabla ya hakimu kuwasili.


Monday, March 25, 2013

CHID BENZ " AMTANDIKA MAKOFI " NGWAIR


Mkali wa vina na mashairi kutoka pande za Ilala anayefahamika kwa jina maarufu la 'Chid Benz' ameanza kupata sifa mbaya baada ya kumpiga mwanamuziki mwenzake 'Ngwea' nje ya ukumbi wa Ambassador Lounge ulioko kwenye jengo la Benjamini Mkapa tower Posta usiku wa kuamkia Machi 22.

Kupigwa kwa 'Ngwea' kulikuja baada ya 'Chid' kumzingua 'Dully' alipokua akiingia ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.

Alipoondoka 'Dully', 'Ngwea' akamuuliza inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo 'Chid' alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza 'Ngwea', inasemekana 'Ngwea' aliamua kukaa kimya lakini 'Chid' aliendelea kungea kwa hasira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia 'Ngwea'.

'Ngwea' aliamua kuondoka kwenye ukumbi huo lakini alipofika chini ya ghorofa ndipo 'Chid' alipomfuata na kuanza kumshambulia mwanamuziki mwenzake huyo na baadaye kumjeruhi kwa chupa mkononi.


Lakini baada ya hapo 'Ngwea' aliweza kufika hospitali na kuweza kupatiwa matibabu ya jeraha hilo la chupa.

WEMA SEPETU AJITOLEA KUTOA MILIONI 13 KUMUOKOA KAJALA ALIEHUKUMIWA MIAKA MITANO ....

Leo imesomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mcheza filamu za Kitanzania anayefahamika kwa jina la 'Kajala Masanja' na mumewe mbele ya Hakimu 'Sundi Fimbo' kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam.


Katika hukumu hiyo 'Kajala' amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe 'Faraji Agustino' kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo kutolea mahakamani hapa, mwanadada mwenye michejo mingi hapa Bongo anayefahamika kwa jina la Wema Sepetu' aliweza kujitolea yeye mwenyewe kiasi cha Tsh. milioni 13 kutoka mfukoni mwake kwa ajili ya kumlipia msanii mwenzake wa filamu 'Kajala' asiweze kutumikia adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 jela.Hii ni mara ya pili kwa msanii 'Wema Sepetu' kujitolea kiasi kikubwa cha fedha kusaidia msanii mwenzake.!

Thursday, March 21, 2013

NEY WA MITEGO AMNYESHEA MVUA YA MATUSI KWA NIKKI MBISHI


Katika kile kinachoonesha bifu ya Ney wa Mitego na Nikki Mbishi kufikia pabaya, Ney amemmwagia matusi ya nguoni rapper huyo wa ‘Kill Yo Self’ kupitia BBM.

 Bifu la wasanii hao lilianza baada ya Nikki kudaiwa kurekodi wimbo uitwao Ney wa Mitego ambayo anamzungumzia msichana mwenye jina hilo na ambaye ana tabia za ukicheche.
“Nikki Mbishi acha us***ge k***m*yako utaf***a siku si nyingi kwa ambao huyu shoga ni rafiki yao BBM mtajua kwanini naongea hivi. Serious Nikki utaf**ika muda si mrefu unatambia za kike we m***nge nimekuvumilia sana kumbe una tabia sawa na dada yako …!! Jipange,” ameandika Ney.

HUU NDIYO MUONEKANO MPYA WA AGNES MASOGANGE


Mwanadada ambaye ni Video Queen wa bongo na alifanya poa sana katika video ya Belle 9 ya Masogage,na kupewa jina la Agnes Masogange,
huu ndiyo muonekano wake mpya kwa sasa.... check picha zake akiwa katika pozi tofauti tofauti.Angnes katika poziiii
Agnes Maso gange katika pozi.

MWANAMKE ACHINJWA KAMA MBUZI HUKO KAHAMAMarehemu Martha Charles baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake. 
 
HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Asack Nzolela (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.

Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.

Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.


Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.
 
Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.

Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana.

Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.


Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.

Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19).

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na mwandishi wetu alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzolela katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzolela amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.

Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...