Friday, August 31, 2012

WA5 WATINGA FAINALI YA SHINDANO LA MISS KANDA YA MASHARIKI TALENT, KUUMANA KESHO MORO


Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.

Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.

Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.

Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.

Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall.

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.

Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini wengine ni pamoja na mtandano  wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd'd, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.

Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.

Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.

Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.

Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea.

Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo.

Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.

Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora .

Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone.

Thursday, August 30, 2012

TWITE ATUA YANGA, MAMIA WAMLAKI, SIMBA HAWAKUONEKANA


Twite baada ya kutua Uwanja wa ndege akiwa na viongozi wa Yanga

BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite ametua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo, kabla ya kupakiwa kwenye gari kuelekea makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Hakuna kiongozi yeyote wa Simba wala askari polisi aliyemsogelea kama ambavyo kulikuwa kuna tishio kwamba akitua tu beki huyo wa kimataifa wa Rwanda, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watamkamata kwa tuhuma za kuwatapeli dola za Kimarekani 30,000.
Inadaiwa, kabla ya kusaini Yanga, Twite aliyekuwa akichezea APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.
Hata hivyo, baadaye mchezaji huyo alighairi na kuamua kwenda Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, ambazo zilikuwa zinammiliki kwa pamoja mchezaji huyo.
Lakini viongozi wa Simba waligoma kupokea fedha hizo ingawa viongozi wa APR na Lupopo walifika hadi ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kuzikabidhi fedha hizo, ili Simba wakazichukulie hapo.
Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha kuhama kwake rasmi na kuja kuanza maisha mapya Dar es Salaam,
Lakini upande wa pili, Simba SC waliamini beki huyo amekwepa kukamatwa kufuatia kuvuja kwa habari za mpango wa kumtegea akitua nchini wamkamate.
Ametua na amekwenda Jangwani, maana yake jaribio la kumkamata akitua limefeli na sasa tusubiri kama Simba watamuwekea mtego mwingine.
Shabiki wa Yanga Babu Ally, akiwa na jezi ya Rage na4
Twite akizungumza na Waandishi huku amevaa jezi namba 4 yenye jina Rage


Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya Yanga, Francis Kifukwe kushoto akiwa Uwanja wa Ndege na kigogo wa Usajili, Seif Ahmad 'Magari'


MISS KANDA YA MASHARIKI WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI MORO

Meneja Mkuu wa Abood Media, Julius Nyaisangah (Uncle J) akitoa ufafanuzi kwa warembo hao walipokuwa ndani ya Radio Abood na Abood Television.

WAREMBO 12 wanaowania taji la Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2012 linalotarajiwa kushindaniwa Septemba 1 ndani ya Hoteli ya Nashera, jana jioni walitembelea baadhi vyombo vya habari vya mkoani Morogoro.
Warembo hao kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na wenyeji Morogoro, walitembelea vyombo vya Abood Media vilivyo eneo la Msamvu, na kujionea jinsi vinavyoendeshwa.
Mratibu wa shindano la Redds Miss Kanda ya Mashariki 2012, kutoka Kampuni ya Nepa Production & Events, Alexandra Nikitasi akiwaongoza warembo hao katika ofisi za Abood Media.
Warembo hao wakiwa katika pozi kwenye ofisi za Abood Media.


Stv kufanya mabadiliko katika vipindi vyake kuanzia Oktoba mosi

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Barbara Kambogi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya mabadiliko ya Chanel za DStv yatakayoanza tarehe 1 Oktoba mwaka huu, hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Ving’amuzi ya DStv Francis Senguji akizungumza katika hafla hiyo na kuelezea mambo mbalimbali yanayohusi mabadiliko hayo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo
Kutoka kulia ni KK, Shelmasi Ngahemela na Rehema Ahmed wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Benny Kisaka kutoka Jambo Leo, Gerald Hando kutoka Clouds na Sebbo wakiwa katika hafla hiyo.
William Malecela na wadau wengine wa Multichoice wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Mamaa Shamimu wa Zeze kutoka 8020fashionblog akiwa na mzee wa Mtaa kwa Mtaa Othman Michuzi na mzee wa www.fullshangweblog.com Bw. John Bukuku.
Kutoka kushoto ni Mdau Zaunul kutoka Mo Blog , Andrew Chale kutoka Tanzania Daima na Mwesa kutoka Mhariri mkuu wa Jambo leo.

DC wa zamani Hawa Ngulume afariki dunia; JK atuma salamu za pole kwa familia

Marehemu Mama Hawa Ngulume (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) na John Guninita ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam. 


Taarifa tulizozipata  ni kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kibaha, Bagamoyo na Mbarali kwa vipindi tofauti Bibi Hawa Ngulume amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatoilewa baadaye.

Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu .

wakati huo huo... Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kwa Familia ya aliyepata kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mama Hawa Ngulume kufuatia taarifa za kifo chake kilichotokea katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani. Mama Hawa Ngulume amefariki leo tarehe 30 Agosti, 2012.


Katika Salamu zake hizo, Rais Kikwete amesema Marehemu Hawa Ngulume, enzi za uhai wake, alikuwa kiongozi shupavu aliyesimamia maamuzi yake katika majukumu muhimu ya kitaifa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo katika sehemu zote alizotumikia akiwa Mtumishi wa Umma, na baadaye alipopewa wadhifa wa Mkuu wa Wilaya alioutumikia katika Wilaya za Singida Mjini katika Mkoa wa Singida, Kinondoni Mkoani Dar es Salaam na mara ya mwisho katika Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya.


“Nilimfahamu Marehemu, enzi za uhai wake, kama Kiongozi Mwanamke shupavu aliyesimamia kikamilifu maamuzi yake, na hivyo kuthibitisha ukweli kwamba wanawake wakipewa fursa wanaweza”, amesema Rais Kikwete katika kuomboleza kifo chake.


“Kutokana na msiba huo mkubwa, natuma Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa Familia ya Marehemu, Mama Hawa Ngulume kwa kuondokewa na Mhimili muhimu na Kiongozi wa Familia. Natambua machungu mliyo nayo hivi sasa kwa kumpoteza Mama wa Familia, lakini nawahakikishia kuwa niko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa”, ameongeza kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.


Rais Kikwete amewataka wanafamilia ya Marehemu wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri wakati huu wanapoomboleza msiba wa mpendwa wao kwani yote ni Mapenzi yake Mola. Amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Mama Hawa Ngulume, Amina.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Agosti, 2012
Gadna G Habash aibukia Times FM


Aliyewahi kuwa mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Gadna G Habash ametambulishwa rasmi leo mbele ya wafanyakazi wenzake wakiwemo na wanahabari wengine waalikwa kupitia kituo kingine cha redio,Times FM ya hapa jijini Dar es Salaam .Gadna ataanza kusikika katika kituo hicho kupitia kipindi chake kitakachoitwa Maskani kuanzia Jumatatu Ijayo mnamo saa kumi mpaka kumi namoja jioni.

Wednesday, August 29, 2012

MISS MWANZA 2012 NI MTIKISIKO IJUMAAFAINALI za Miss Mwanza 2012, zinatarajiwa kulitikisa Jiji la Mwanza Ijumaa hii.
Shindano hilo mwaka huu, limeonesha kuwa na msisimko wa hali ya juu kutokana na hali halisi kujionesha kwamba warembo
wa shindano hilo mwaka huu ni tishio hata kwa Miss Tanzania.
Tathmini ya mashindano ngazi mbalimbali kuelekea Miss Tanzania mwaka huu, inaonesha kuwa mrembo atakayeshinda Miss
Mwanza mwaka huu, anayo nafasi kubwa ya kuchukua taji.
Wasichana hao wazuri, wanaostahili sifa ya kuitwa warembo, ndiyo watakaopanda jukwaani kesho (Agosti 31, 2012) kwenye
Ukumbi wa Yacht Club, Mwanza, kuwania la Taji la Miss Mwanza 2012.
Warembo hao, tayari wapo kambini ndani ya Isamilo Lodge, wakijiandaa na mtifuano mkali.
Mratibu wa shindano hilo, Peter Omar, amesema: “Kila kitu kipo sawa, maandalizi ni mazuri. Kusema ukweli kambi ya Miss
Mwanza mwaka huu ni matawi ya juu. Warembo wapo vizuri na huduma pia ni za kiwango kizuri. Kimsingi kambi ya mwaka huu imepandisha hadhi ya shindano letu.”
Kwa upande mwingine, Omar alisema, wakongwe wa Taarab nchini, Malkia Khadija Kopa na gwiji Mwanahawa Ali, wanarajiwa
kuoneshana mkali wa vijembe vya mwambao kwenye shindano la Miss Mwanza 2012-2013.
Kopa na Mwanahawa ambao ndiyo waimbaji wakongwe walio juu kwa sasa kwenye muziki wa Taarab, wanarajiwa kutoa shoo
kali siku hiyo kisha mashabiki wenyewe ndiyo watapima nani mkali wa mipasho.
“Miss Mwanza ya mwaka huu ni funga kazi. Watakaokuja Yacht Club, watashuhudia shoo kali ambayo haijawahi kutokea.
Kwanza kabisa tuna warembo wazuri. Hii ina maana kwamba Miss Tanzania wa mwaka huu, atatokea Mwanza.
“Tuna timu nzuri ya wanamuziki watakaotumbuiza. Mpambano wa Khadija Kopa na Mwanahawa Ali, haujawahi kutokea
Mwanza. Kuna wanamuziki wengine wakali watakuwepo akiwemo Bob Haisa (Haisa Mbyula) ambaye kwa zaidi ya miaka 14,
amebaki kuwa mmoja wa mabalozi bora kabisa wa Kanda ya Ziwa kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.”Warembo Redds Miss Mwanza 2012/13 wakiwa kambini katika Hoteli ya Isamilo Lodge, ambapo warembo 18 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mwanza, watashiriki shindano hilo, linalotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 31/08/2012 ndani ya Yatch Club jijini Mwanza.

KAMPUNI YA PUSH MOBILE YAKABIDHI PIKIPIKI ZA WASHINDI WA TANGA WA SHINDA BODA BODA NA SERENGETI FIESTA 2012


Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney akimkabidhi pikipiki aina ya TOYO, Rashid Juma Ramadhan ambaye ni mkazi wa Tanga aliyejishindia pikipiki hiyo baada ya kucheza bahati nasibu ya Serengeti Fiesta 2012.

Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi pikipiki aina ya TOYO, Alima Salim Omari ambaye ni mkazi wa Tanga aliyejishindia pikipiki hiyo baada ya kucheza bahati nasibu ya Serengeti Fiesta 2012.

  

WATAALAMU WA MAMBO YA AFYA KUTOKA NCHINI INDIA WAJA TANZANIA KWA ZIARA YA UTALII WA AFYA


Mshauri wa Ubalozi wa India, Kunal Roy akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ziara ya kitalii ‘’ Utalii wa Afya‘’ itakoyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 30 na 31 Augusti. Moja ya lengo ikiwa ni kujuana kwa wasomi na kuelimishana na kuboresha huduma.

Mkurugenzi wa Shirikisho Kanda ya India Chemba ya Biashara na Viwanda (FICCI), Lt. Vivek Kodikal (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ubalozi wa India uliopo jijini Dar es Salaam jana kuhusu ziara ya kitalii ‘’ Utalii wa Afya‘’ itakoyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia tarehe 30 na 31 Augusti. Moja ya lengo ikiwa ni kujuana kwa wasomi na kuelimishana na kuboresha huduma.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

Tuesday, August 28, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TANO KCMC‏


Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza na Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kushoto} Profesa Raimos Olomi na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akina mama Dkt Gileard Masenga (kulia) mara baada ya kutoa msaada wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo. 
 
Benki ya ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa shilingi milioni tano (5m) kusadia ununuzi wa vifaa katika wodi ya akina mama katika hospitali ya rufaa KCMC ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina mama wajawazito,
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo uliofanyika hospitali hapo jana, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau alisema kuwa msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa msaada ambao benki hiyo iliutoa mwaka jana.
Mwaka jana tulikarabati chumba cha akina mama wagonjwa hatuti kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni kumi na moja. Nilipofamishwa kuwa chumba kilikuwa tayari lakini hakuna vifaa niliona kuna umuhimu kutoa msaada wa kununulia vifaa ili pesa iliyotolewa kwanza isiwe imepotea bure,” alieleza
Meneja huyo wa tawi alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa msaada huo kwa kutambua umuhimu wa kusaidia serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhakikisha kuwa malengo ya millennia ya kuhakikisha kuwa vifo vya akina mama na mtoto vinakwisha kufikia mwaka 2015.
Akipokea msaada huo, Kaimu mkurunzi wa hospital ya KCMC Profesa Raimos Olomi alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika hospitali hiyo kutokana.
Vifo vya akina mama na watoto hapa nchini bado ni vingi. Jitihada kubwa zinahitajika kuvipunguza. Kupitia misaada ya wadau mbalimbali kama huu wa Benki ya KCB lengo linaweza kufikiwa. Tunaishukuru sana Benki ya KCB kwa msaada huu muhimu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake hospitalini hapo Dr Gileard Masenga alisema kuwa hospitali hiyo haikuwa na wodi ya akina mama mahututi na kuongeza kuwa msaada huo utasadia kuokoa maisha ya akina mama na watoto.
Mwanzoni tulikuwa tunalazimika kuwapeleka akina mama kwenye hodi za wagonjwa hahututi ambazo wagonjwa wote wanatibiwa. Tunaamini msaada huo utasaidia kuboresha hali na hivyo kuokoa wakina mama wengi zaidi. Tunaishukuru Benki ya KCB kwa kuwekeza katika afya ya mama na mtoto,” alifafanua.

Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya makabidiano ya hundi yenye thamani ya shilingi 5m/- kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- kwa Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya KCMC {kulia} Profesa Raimos Olomi kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga. Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali. Katika kati ni Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC Profesa Raimos Olomi
Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC rofesa Raimos Olomi akiifurahia hundi ya shilingi 5m/-iliyotolewa na Benki ya KCB kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kushoto ni Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau.
Mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga akitoa maelezo kwa Emmanuel Grayson ambaye ni mkuu wa masuala ya kijamii wa Benki ya KCB tawi la moshi juu ya wodi iliyokarabatiwa na benki hiyo mwaka jana mara baada ya kutoa msaada wa wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...