Tuesday, September 23, 2014

MSAMA AWAPIGA TAFU YATIMA DAR


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda. Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika tamasha la Pasaka na Krismasi.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.

Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.

Watoto wa kituo cha Maunga cha Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Rashid Mpinda (mwenye kofia).

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.

Msama akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha Tovichodo cha Temeke.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda. Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika tamasha la Pasaka na Krismasi.Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda akimshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa misaada aliyotoa.


Msama akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga.

Watoto wakimshukuru Msama baada ya kuwapatia msaada wa vyakula mbalimbali.

Mkurugenzi wa Kituo cha Tovichodo cha Temeke, Honoratha Michael akipokea sehemu ya msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.


KAMPUNI ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, juzi ilitoa misaada ya vitu kwa vituo vitatu vya kulea yatima vya wilayani Kinondoni na Temeke.
Msaada huo ambao ni utekelezaji wa programu ya kampuni hiyo kama moja ya kurejesha sehemu ya faida itokanayo na uratibu wa matamasha ya muziki wa injili kwa jamii.
 
  Msama Promotions Ltd ambayo pia ni waratibu wa tamasha la muziki wa injili la Pasaka na Krismas, si mara ya kwanza kwao kutoa misaada ya aina hiyo kwa vituo vua yatima na watu wengine wenye mahitaji kama wajane na wazee.

Vikundi vilivyonufaika na msaada huo Jumapili, ni kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Maunga pia cha Kinondoni.

Aidha, misada hiyo imewafariji watoto yatima wa kituo cha Tovichido cha Wilayani Temeke akisema amefanya hivyo baada ya kuguswa na hali halisi inayowakabili.

Msama alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa watu wenye uwezo, makampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.


Kwa upande wa misaada iliyokabidhiwa kwa vituo hivyo, ni mchele, sukari, unga, mafuta ya kula, chumvi, unga wa ngano na vingine vingi kwa ajili ya matumizi ya kila siku nyumbani, vyote vikiwa na thamani ya shilingi mil 7.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa Kituo cha Maunga, Rashid Mpinda alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo na kuwasihi wengine waige mfano huo wa kusaidia makundi maalum.

Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mpinda alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma hadi kufukuzwa kwa kukosa karo, hivyo kushindwa kupata elimu.

Msama kwa upande wake alisema jukumu la karo za wanafunzi hao analibeba yeye pamoja na sare kutokana na kuguswa kwake na kilio cha watoto hao.

TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI YA WAREMBO WA MISS TANZANIA HUKO BABATI
Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi watano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam.

Msanii wa Bongo Fleva, Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.


Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.

Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo.
Kila aina ya staili za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani.

Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.

Wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.

Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.

Friday, September 12, 2014

Mike Tyson amporomoshea matusi mtangazaji wa kipindi cha TV kilichoruka LIVE

Bingwa wa zamani wa dunia katika mchezo wa masumbwi Mike Tyson alishindwa kuvumilia swali aliloulizwa na mtangazaji wa Canada wa kipindi cha Television kilichokuwa kinaruka Live na kumporomeshea matusi mfululizo.

Mtangazaji huyo, Nathan Downer alikuwa akifanya mahojiano na Mike na alikuwa kwenye kipengele kuhusu mkutano wake na mgombea wa kiti cha Mayor, Rob Ford anaemuunga mkono.

Baada ya maswali mawili matatu, mtangazaji huyo alimuuliza Mike Tyson swali kuhusu sakata lake la kufungwa kwa kosa la ubakaji na hapo ndipo mambo yalipobadilika.

“Baadhi ya wakosoaji wako wanaweza kusema, ‘hizi ni mbio za kuwania kiti cha mayor, tunajua wewe ni mfungwa wa kesi ya ubakaji, hii inaweza kuiumiza kampeni yake (Rob Ford). Utalijibu vipi hilo?” Aliuliza Downer.

Kwanza Tyson alianza kwa kumwambia kuwa hamjui mtu mwingine anaesema hivyo na kwamba amemsikia yeye peke yake akisema hivyo.

“It’s so interesting because you come across as a nice guy but you’re really a piece of shit…“F*ck you.” Alisikika Tyson.

Baada ya sekunde chache aliongeza tena kwa msisitizo hata baada ya kukumbushwa kuwa yuko kwenye kipindi kinachoruka moja kwa moja, “No because you’re a piece a shit, you really are. F*ck you.”
Mtangazaji alijitahidi kuyapotezea yaliyotokea na kuendelea na maswali mengine lakini mambo hayakuwa sawa kabisa.

Baada ya mahojiano hayo, Downer alitweet kuwaomba radhi watazamaji na kwamba kwa upande wake binafsi hana tatizo na alichofanya Tyson.

“No ill will toward Mike Tyson. He lashed out at me and that's okay. Not taking it personally.” Alitweet.

“I'm okay everybody. Unfortuantlely my question hurt Mike Tyson's feelings. That was not my intentions. My apolgies for the language” Inasomeka tweet nyingine ya Downer.

Tyson yuko Canada kwa ajili ya kufanya onesho lake la ‘Mike Tyson: Undisputed Truth’.

Mwanaume augua kama mwanamke mjamzito


Harry Ashby ameripotiwa kuwa na dalili za ujauzito kama mchumba wake

Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza nchini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito.

amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa Itv news umeeleza.

habari zinasema mwanaume huyo mwenye miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi ,amesema ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili ya aliye mjamzito na kudai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa na hamu ya baadhi ya vyakula.

Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa mchumba wake ni mjamzito.

Harry amekuwa akipatiwa dawa na inasemekana anaweza kudai mafao wakati akiwa katika mapumziko hayo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...