Friday, June 28, 2013

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA


Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.

Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.
Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.

MAITI AFUFULIWA HUKO MKURANGA PWANI.... MILIONI 15 ZAHITAJIKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUMRUDISHA KATIKA HALI YA KAWAIDABinti Nuru Omari aliyeibuliwa.
BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu.
Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha Kalole, Tarafa ya Kisiju, walayani humo.

Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’.

Kijumba alimokuwa Nuru.
Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.


Ndugu na majirani waliofika kumtazama Nuru.
Mzee huyo alisema ilibidi aondoke licha ya mwanaye kumtaka alale lakini kwa vile yeye ni mwanaume isingewezekana kulala hospitalini hapo.

“Kesho yake nilipewa taarifa kuwa mwanangu amefariki dunia usiku. Tulianza taratibu za mazishi na kumzika kwenye Makaburi ya Kichangani, Mbagala, Dar kutokana na kukosa fedha za kuusafirisha mwili hadi Mkuranga,” alisema mzazi huyo

Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Said Ali Ngaora ‘Dr. Lamba’ anayeishi Mbagala Rangi Tatu, Dar alifika katika kijiji hicho cha Kalole mwaka huu na kuwaambia wananchi kuwa kijijini hapo pana mtu anaonekana alikufa na kuzikwa lakini bado yupo hai na amewekwa sehemu na kutaja gharama za kumtoa ni shilingi milioni tatu.


Mganga aliyemuibua Nuru.
Akielezea tukio zima Dr. Lamba alisema wananchi walimruhusu akaanza kazi kwa kushirikiana na wataalamu wenzake.


Dr. Lamba na timu yake walifanikiwa kumuibua msichana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 12-15 kwenye mji ambao hakuna mtu anayeishi akiwa ndani ya banda la kuku huku kukiwa na chungu chenye damu, asali na udongo ambavyo vilikuwa ndivyo vyakula vyake akiwa na muonekano wa kutisha kwa kuwa na nywele ndefu na chafu na kucha zikiwa ndefu mithili ya jini.

Baada ya kumtoa alipelekwa katika uwanja wa mpira kijijini hapo na kuogeshwa pamoja na kukatwa kucha kisha akapelekwa katika nyumba aliyofikia mganga huyo, hata hivyo hakuweza kuongea vizuri.

Kwa mujibu wa mashuhuda ulimi wa Nuru ulikuwa mzito na mpaka sasa anazungumza kwa vitendo kama bubu huku chakula ambacho ameanza kula vikiwa ni ugali na kuku, uji na juisi ya embe.

Mbali na shilingi milioni tatu za kutoa, mganga huyo anataka milioni 15 kutokana na dawa anazompa kwa ajili ya matibabu ili arudi katika hali ya kibinadamu .

Hata hivyo, baadhi ya ndugu wanaopinga kuwa Nuru siyo mtoto wao lakini baba mzazi anasema ni mwanaye kutokana na alama zilizopo mgongoni mwake na anafanana sana na mdogo wake.

Makamu Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ali Hassan Ndeko alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa wanakijiji wanaendelea kumiminika kwa ajili ya kumuona mtoto huyo akiwa chini ya uangalizi maalumu wa mganga huyo huku wakijitolea vyakula.

SOMA PIA ANGALIA PICHA NAMNA WEMA SEPETU ALIVYOWAFANYIA WAFANYAKAZI WAKE WA NDANIWema Isaac Sepetu akiwa amefura kwa hasira.

STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi, Amani linakuletea kisa na mkasa.
Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.

ILIKUWAJE?
Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo.

Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.
Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.
Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.

...Akimmwagia maji mlinzi.

APANDWA NA HASIRA
Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele yake.

MITUSI MIZITO
Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni isiyoandikika gazeti kutokana na ukali wake.


“My friend ninyi ni mabogasi kabisa, nawaambia mtaozea Segerea, mnafanya nini hapa ninyi wa…(tusi) au mna…(tusi kali).
“Ninyi ni …(tusi kubwa likihusisha mama zao), mnakaakaa tu hapa wa…(tusi tena), mnajua bei ya power window? Mnadhani hili ni Toyota? Kwa taarifa yenu hili ni Lexus …(tusi) zenu,” alisikika Wema akitumia lugha ya matusi ambayo asilimia kubwa hayaandikiki kwa namna yoyote kutokana na kupitiliza.
Wema aliendelea kuwakimbiza ndani ya fensi akiwapiga huku sauti ya Martin Kadinda (yule meneja wake) ikisikika, ‘Mwache ataruka ukuta, nenda karipoti polisi’.

...Mlinzi akiwa hoi baada ya mshikemshike.

AMGEUKIA FIONA
Huku akiwa mbogo, Wema alimgeukia mmoja wa mbwa wake aitwaye Fiona na kumuwashia moto huku akimmwagia mitusi:
“Na wewe Fiona unakaa hapo hapo unamuuzia nani sura badala ya kulinda mlinzi, sipendi mambo ya ki… (tusi).
NI HUJUMA?
Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kufyatua filamu ya Endless Fame Production alikwenda mbali na kuwatuhumu wafanyakazi hao kuwa kuna uwezekano wanatumiwa kumhujumu akiahidi kuwakomesha.
“Mnatumwa mnapewa pesa ili mnifanyie hivi…gari litaibiwaje power window likiwa ndani na ninyi mkiwepo? Wa…(tusi) sana ninyi,” alisikika msanii huyo.

 
...Wema akiporomosha matusi.

Katika hali ya kushangaza, badala ya kumuwashia moto mlinzi anayehusika na usalama nyumbani hapo, Wema ‘alidili’ na wafanyakazi wa ndani tu huku mlinzi naye akishindwa kumuamulia na kubaki kumtazama tu namna alivyokuwa akikimbizana na wafanyakazi hao.

NENO LA MAJIRANI
Kwa upande wao majirani walikuwa wakila chabo na kusikitishwa na mvua ya matusi aliyokuwa akiitoa msanii huyo ambaye ni kioo cha jamii.

...Akiliangalia gari lake.

“Jamani jamani, hivi hajui tuna watoto wadogo ambao hawastahili kusikia matusi makubwa kama anayomwaga?
“Ukweli Wema anatusikitisha sana kwa sababu watoto wanajifunza nini kutoka kwake?” alihoji mmoja wa majirani hao aliyeomba hifadhi ya jina ili na yeye asije akawashiwa moto na msanii huyo.

AMANI LAFUNGASHA VIRAGO
Hadi Amani linafungasha virago maeneo hayo mwanadada huyo alikuwa akijiandaa kwenda kuripoti tukio hilo polisi hivyo tunaendelea kufuatilia kilichojiri. 
sorce:global publishers

Thursday, June 27, 2013

MASHUJAA BANDI YATAMBULISHA WANENGUAJI WAPYA

    Wanenguaji wapya wa Mashujaa Band wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakitambulishwa leo.

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Mashujaa imezidi kujiimarisha baada ya kuwatwaa wanenguaji wapya toka nchini Kongo. Wanenguaji hao ambao wametambulishwa leo kwa waandishi wa habari wanaonekana moto wa kuotea mbali.
Mmoja wa wanamuziki hao akijitambulisha kwa wanahabari (hawapo pichani).
   
Mmoja wa wanenguaji hao akionyesha staili yake ya nywele.
   
Benny Kinyaiya (kulia) akiwa na mmoja wa wapenzi wa bendi hiyo.
Wanenguaji hao wakionyesha umahili wao wa kunengua.
Afisa habari wa Mashujaa Band, Asha Kigungula akiwa na Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter. 

USIKU WA TUDD THOMAS KUACHA HISTORIA DAR LIVE J'PILI HII

REDD'S MISS TEMEKE KUFANYIKA JULAI 5 2013

Wednesday, June 26, 2013

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERASerikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.

Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.

Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.

Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.

Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria.

Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.

Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.

Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”

Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.

“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.

“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).

Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.

Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.
“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.

Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.

Sala zetu kwa Mzee Madiba
Pamoja na mkutano huo, wanafamilia hao walifanya mazungumzo na machifu wa eneo hilo, wakiongozwa na Chifu Bhovulengwe wa Baraza la Kifalme la Abathembu.

Johannesburg. Familia ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela imesema haitaruhusu kusitishwa kwa matibabu anayoendelea kuyapata na kwamba itaendelea kufanya juhudi za kurefusha uhai wake hadi Mungu atakapoamua kumchukua.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mwanawe mkubwa, Makaziwe Mandela huku kukiwa na taarifa kwamba kiongozi huyo hajitambui na anasaidiwa kuendelea kuishi kwa mashine tangu alipofikishwa hospitalini huko Pretoria wiki mbili zilizopita.

Alisema kwamba familia haiwezi kuacha kumhudumia kwa shinikizo la watu wa pembeni wanaodai kwamba inatakiwa imruhusu akapumzike kwa amani na kwamba kwa mujibu wa mila za Wathembu, watafanya hivyo endapo tu mhusika mwenyewe (Madiba), atakapotamka.

Juzi, kwa mara ya kwanza, Rais Jacob Zuma alikiri hadharani kwamba hali ya shujaa huyo wa Afrika Kusini ni mbaya na anahitaji maombezi. Alisema hayo baada ya kumtembelea na kuzungumza na mkewe, Graca Machel-Mandela.

Hata hivyo, taarifa zilieleza kwamba hajaweza kuzungumza tangu alipofikishwa hospitali, bali alifungua macho kwa shida mara kadhaa.

Mandela anayesumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu alifikishwa katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo ya Medi-Clinic, Pretoria Juni 8 na tangu wakati huo, taarifa zimeeleza kwamba hajaweza kuzungumza lolote.

Taarifa zikieleza kwamba hali yake ilizidi kuwa mbaya Jumapili iliyopita na baadhi ya wanafamilia tayari wameshatangulia kijijini kwake, Qunu.

Gazeti la Mail&Guardian la Afrika Kusini lilieleza jana kwamba wanafamilia hao walifanya kikao maalumu nyumbani kwa Mandela, kisha kutembelea na kufanya ukaguzi katika eneo la makaburi ya familia, sehemu ambayo kiongozi huyo pia anaweza kuzikwa.

Makaburi hayo yako jirani na nyumba ya mdogo wake, Morris na haikuwekwa wazi kuhusu uamuzi wa wanafamilia hao kufika eneo hilo la makaburi, lakini kwa mujibu wa mila na desturi za watu wa Kabila la Xosa, familia hutembelea eneo hilo wanapobaini kwamba mmoja wa wanafamilia yuko mbioni kuungana na waliotangulia mbele za haki, au kuomba sala maalumu kwa ajili ya kupata ridhaa ya kurefusha maisha ya mhusika.

Pamoja na mkutano huo, wanafamilia hao walifanya mazungumzo na machifu wa eneo hilo, wakiongozwa na Chifu Bhovulengwe wa Baraza la Kifalme la Abathembu.

Wanafamilia waliofika na kuhudhuria kikao hicho cha jana ni pamoja na mkewe wa zamani, Winnie Madikizela-Mandela na Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala, Lindiwe Sisulu pamoja na Kiongozi wa Chama cha United Democratic Movement, Bantu Holomisa.

Iliarifiwa kwamba kikao hicho kilifanyika kutokana na simu ya dharura iliyopigwa kwa wanandugu na wanawe, Mandla, Thanduxolo, Ndaba na Ndileka Mandela ambao tayari walishawasili kijijini hapo tangu Jumapili na kujumuika na wanafamilia wengine.

Ulinzi wa Obama haujawahi kutokea Afrika
Tayari baadhi ya wanajeshi wa Marekani wamewasili Dar es Salaam na kuweka mitambo ya mawasiliano maeneo yote ambayo atapita au kukagua.

Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.

Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.

Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.

Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.

Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.

Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.

Tuesday, June 25, 2013

"LAZIMA NIFE KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 40"...AUNT EZEKIEL


WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka na kudai kuwa hawezi kuishi miaka mingi na atakufa mapema kuliko watu wanavyodhani.

Aunt Ezekiel alifunguka hayo juzikati alipokuwa akipiga stori na mwandishi wetu jijini Dar ambapo alibainisha kuwa akijitazama mustakabali wa maisha yake basi anaona kabisa kuwa hawezi kufikisha hata miaka 40 kabla hajafa.

“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.

MBUNGE WA CHADEMA SUGU AKANA KUMUOMBA RADHI WAZI MKUU KWA KUMUITA "MPUMBAVU"Juzi, mbunge wa mbeya mjini alitoa tusi zito kwa waziri mkuu wa Tanzania na kudai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbuvu kama yeye...

Kupitia account yake ya facebook, Sugu, ambaye ni mbunge wa mbeya amezidi kusisitiza kuwa hawezi kuomba msamaha wala kuifuta kauli yake....

Hii ni post yake facebook:

"...naskia kuwa watu wanasema kwamba eti nimefuta kauli yangu kuhusu waziri mkuu na amri yake kwa polisi kupiga wananchi?!...


Sina sababu ya kufuta wala kuomba radhi, na nasimamia kauli yangu to the end...kwanza 'upumbavu' sio tusi,upumbavu kwa kiingereza ni stupidity-which is lack of knowledge and understanding...

So hata uwe na cheo gani kama ukishindwa kuwa na 'understanding' juu ya madhara ya kauli zako kwa taifa then u r 'stupid'...ambapo kwa kiswahili ndio 'mpumbavu'..."


BAADA YA KURUSHIWA CHUPA AKIWA STEJINI OMMY DIMPOZ AOMBA MSAMAHA KWA MARA YA PILI.


Ommy Dimpoz kwa mara nyingine ameamua kupaaza sauti yake na kuwaomba watanzania wamsamehe kwa kauli zake mbaya kuhusu marehemu Ngwea....

Sambamba na msamaha huo,Ommy anadai kuwa amejifunza kutokana na kosa lake na kwamba hatarudia tena...

Uamuzi wa kuomba msamaha kwa mara ya pili umekuja baada ya msanii huyu kupigwa mawe mjini Dodoma hivi juzi


Hii ni kauli yake kupitia ukurasa wake wa facebook:

MTANGAZAJI JOYCE KIRIA AOMBA AFAHAMISHWE ALIPO MUMEWE HENRY KILEO .

Mtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao jana jijini dar es salaam.

Monday, June 24, 2013

HIVI NDIYO UMATI WA WATU ULIVYOJITOKEZA KATIKA MAZISHI YA MAMA WA WANAMZIKI BARNABA

Barnaba akiagana na Mama ake kwa mara ya mwisho.....!!

Madee akiwa na Lady Naa......!!Joh Makini baada ya Kuaga Mwili.....!!

Baadhi ya wanakikundi wanaounda Tanzania House of Talent (T.H.T)
Hapa mwili ukiwa umewasili makaburini tayari kabisa kwa maziko...!

Barnaba akitupa mchanga wa mwisho kwenye kaburi la marehemu mama yakeMume wa Bi Mariamu Arubeth akiweka mchanga kaburini...!!

Jeneza likiwa ndani ya kaburi tayari kwa kuanza kufukia na mchanga.....!

Hyper Man HK alikuwepo pembeni na mwanamuziki Shilole...!!

Producer Lamar wa Fishacrab Studio alikuwepo pia...!

Hali ile ya uchungu na kulia sana ilipelekea Barnaba kukosa
nguvu na kuzimia kwa dakika kadhaa...

Baada ya kuzinduka akisaidiwa kuingia kwenye gari kuwaishwa
Hospital kutokana na kupoteza nguvu kabisa...!!


Mume wa Marehemu akisimika msalaba kaburini

Msemaji wa familia akisoma historia fupi ya
marehemu Mariamu Arubeth...!!
Msemai wa Familia akitoa maelekezo kwa waombolezaji mara
baada ya kumaliza shuguli a maziko...!!

Umati wa waombolezaji wakitawanyika makaburini baada
ya shuguli ya mazishi kukamilika...!!

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...