Saturday, July 25, 2015

Hii ni tweet ya Martin Kadinda baada ya Wema Sepetu kushindwa viti maalumu Singida

Wema Sepetu bahati imekuwa sio yake, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa viti maalumu katika mkoa wa Singida.
wemaa-na-kadinda
Meneja wa Wema sepetu ameandika kuhusu kushindwa kwa Wema Sepetu katika uchaguzi huo…Katika Mtandao wa Twitter Martin Kadinda ameandika “Haikuwa vile tulivyotarajia… Hongera Aysharose Mattembe”.

Utata mpya mtoto wa Diamond!

Diamond-Platnumz-na-Zari
Staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  akiwa katika pozi na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
MUSA MATEJA
Utata mpya umeibuka wakati mama kijacho wa staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,  akitarajiwa kujifungua muda wowote kutoka sasa, ishu ni juu ya uraia wa mtoto atakayezaliwa.
TUJIUNGE NA MTU WA NDANI
Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia hiyo zilidai kwamba, utata umezidi kuigubika familia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ndugu wa pande zote kuendelea kuvutana juu ya Zari ajifungulie nchi gani kati ya Tanzania, Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’.
DIAMONDZARI.jpg
Utata huo umevuja wakati paparazi wetu akiwa katika mishemishe za kutaka kujua Zari alipo kwa sasa na atajifungulia katika hospitali ipi ndipo alipopenyezewa ‘ubuyu’ kwamba hadi sasa kuna utata mkubwa katika familia hiyo.
MABISHANO YA URAIA
Chanzo kilimweleza mwanahabari wetu kuwa, kikubwa ni mabishano ya uraia na sehemu sahihi ya kujifungulia mtoto huyo.
Kilidai kwamba, suala hilo limekuja kufuatia ndugu wa Zari kutaka ajifungulie Sauz jambo ambalo Diamond na familia yake wamekuwa wakilipinga vikali.
ZARINADIAMOND4.jpg
ZARI NJIA PANDA
Ilisemekana kwamba, kwa upande wake Zari amekuwa njia panda kutokana na shinikizo hilo huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye akisisitiza kuwa lazima Zari ajifungulie Bongo ili amuhudumie mkwe wake huyo.
“Yaani ndugu wa Zari wanampa Diamond wakati mgumu sana kutokana na kuendelea kung’ang’ania Zari akajifungulie kwao (Sauz ambako kuna ndugu wengi) wakati furaha ya Diamond ni kuona mtoto akizaliwa Bongo.
DIAMOND ACHACHAMAA
“Unaambiwa Diamond amechachamaa vibaya, alipoona hawezi kutumia nguvu ikabidi atumie ushawishi kwa ndugu wa Zari ili wakubali ajifungulie Bongo lakini wale ndugu wanasema wako tayari kumtumia hata ndege kwa sababu yupo Bongo, arudi Sauz ambako kuna daktari wao wa familia.
HUYU HAPA DIAMOND
Paparazi wetu baada ya kunyaka utata huo alimtafuta laivu Diamond kwa kujiridhisha zaidi juu ya hilo ambapo baada ya kumpata alifunguka kwamba, kipindi hiki kuna mambo kibao yanaibuka kila kukicha jambo linalomshangaza.
zari
Alisema kuwa utata huo alishamalizana nao ndiyo maana hadi muda huu Zari yupo Dar kwa ajili ya kujifungua.
“Ninachoweza kusema kwenye maisha ya kawaida huwezi kuwazuia watu kuongea jambo wanaloliwaza wao.
“Hayo mambo ya utata nimeshayamaliza ndiyo maana kwa sasa Zari yupo White House (nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Madale jijini Dar) akisubiria saa ya kujifungua.
“Kwangu namuomba Mungu ajifungue salama maana mtoto ni miongoni mwa vitu nilivyotamani kitambo,” alisema Diamond huku akiwashukuru Watanzania wote wanaoendelea kumuunga mkono kwenye muziki wake.

Nkurunziza karudi madarakani Burundi? Haya ndio matokeo ya Uchaguzi..


NKURUZINZA
Uchaguzi Mkuu wa Rais Burundi umefanyika tayari japo kulikuwa na mvutano mkubwa sana kutokana na ishu ya kuonekana Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu ilikuwa ni kwenda kinyume na kanuni za nchi hiyo.
Matokeo yametolewa July 24 2015 na matokeo yameonesha Rais Nkurunziza ameshinda tena Uchaguzi huo kwa kupata 69.4% ya kura na kumshinda mpinzani wake wa karibu Agothon Ruwasa aliyepata 18.9 %. 
Kulikuwa na jumla ya Wagombea nane kwenye nafasi hiyo lakini Wagombea wengine walijitoa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo.

Wednesday, July 22, 2015

Wema, Aunt wakutana wapigana vikumbo!

shostMafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’.
Imelda Mtema
MAFAHARI wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.
wemasepetuWema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliusoma ‘mchezo’ mwanzo mwisho, Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao walifika na kukaa meza nyingine.
auntezekiel1Aunt Ezekiel.
Habari zinazidi kudai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt tangu ajifungue.
“Yaani kwa kweli hakuna hata mmoja aliyeamini kilichotokea pale kwa kuwa watu wengi wanajua ni marafiki wa damu lakini kiliwashangaza watu, hata kupeana salamu kweli? Kila mmoja aliendelea kufanya kilichompeleka,” kilisema chanzo chetu.

Diamond: Aibu yao!

MSHTUKO! Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka siri nzito kwa mashabiki waliokuwa wakimpigia kampeni katika mitandao mbalimbali ili ashindwe kwenye Tuzo za MTV Africa Music (Mama) 2015, zilizofanyika usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita huko Durban, Afrika Kusini  baada ya kushinda tuzo moja na kudai kuwa ni aibu kwa waliokuwa wakifanya kampeni asishinde.
Diamond-MTVBase-Red-Carpet-03Diamond akiwa katika red carpet ya tuzo hizo.
DIAMOND MTUMBUIZAJI BORA AFRIKA
Diamond alitwaa Tuzo ya Best Live Act (Mtumbuizaji Bora Afrika) ambapo alijikuta akifurahi kupindukia huku akiwakejeli wale waliokuwa wakimpigia kampeni ashindwe kwamba bado ataendelea kuwakalisha vibaya.
WAMEBAKI NA AIBU
“Nina furaha sana kupata tuzo tena, wale waliokuwa wakipiga kampeni kwenye mitandao kwamba nisipigiwe kura naona wamebaki na aibu yaani nimewaumbua, hapa bado ninaongeza nguvu zaidi na nina mpango wa kufanya kazi na mastaa wakubwa wa Marekani, ila ninawashukuru wale walionipigia kura,” alisema Diamond.
JOKATE ALALAMIKA KUDHALILISHWA
Wakati Diamond akisherehekea ushindi huo, mwanadada aliyewahi kuwa mpenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amelalamika kudhalilishwa mtandaoni na mwanamuziki huyo baada ya kuweka video akiwa anacheza wimbo wa jamaa huyo wa Mdogo Mdogo na kuambatanisha na maneno yaliyosomeka: “Mbona bado. Mtanyooka tu.”
kateJokate.
“Sijapenda na sijawahi kuona mwanaume mswahili kama Diamond, anatafuta kiki za ajabu tu mjini hapa kwani hiyo video ni ya zamani tena nilipigwa nikiwa studio lakini nimeshangazwa sana na kitendo chake cha kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na maneno ya kunidhalilisha,” alisema Jokate akiwa amepaniki.
Diamond alipata mapokezi ya kifalme  baada ya kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa Ndege wa Julius Nyerere, Dar, Jumapili iliyopita ambapo kundi kubwa la watu lilijitokeza kumpokea pamoja na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa muda mrefu alikuwa mgonjwa lakini alionekana akimfurahia mwanaye uwanjani hapo.
Baada ya kutua Bongo, Diamond alifikishiwa malalamiko ya Jokate kwamba alikuwa amemdhalilisha yeye na wanawake wengine ambapo aliyafungukia:
“Unajua, kwanza nimecheka alafu nimesikitishwa kwa sababu nimeambiwa sijasoma, nimeambiwa kuna posti ameandika (Jokate), amezungumzia vitu vingi…Yeye kacheza kama fan wa nyimbo zangu na mimi nilimposti kama fan wangu.
“Hakuna mahali nilimuandika jina, kwa nini achukulie vibaya?
“Ukiona mtu anajishuku ujue kuna namna nyuma. Mbona mimi naposti watu wengi tu, tena naandika caption zangu za vitukovituko maana yake mimi nina caption za vituko.
“Ni kweli mimi ni mswahili, nimezaliwa Tandale, nimekulia Tandale na Tandale ndiyo kumenifanya leo niwe hapa nilipo…
“Kwa hiyo nina caption zangu za uswahili kwa sababu uswahili ndiyo umenikuza…siziachi kuziandika, huwa naziandika nyingi ..kwa nini ya kwake yeye tu aione tatizo?
kiba6060000000
Ali kiba.
“Kwani kuna ubaya gani mimi kuandika mtanyooka tu kama yeye haimhusu ina maana labda kuna kitu kinamhusu.
“Nimeambiwa pia amezungumza kwamba ndiyo maana wanaogopa kuwasapoti wasanii Watanzania kwa sababu wakiwasapoti wanadhalilishwa, yeye mimi mpaka nimeenda kuchukua tuzo alinisapoti nini?
“Aliposti hata posti moja kusema mpigieni kura Diamond? Sasa hivi anajishaua eti kanisapoti. Amesapoti nini? Eti ametoa hongera, mimi nimeshinda tuzo, eti ooh hongera kwa tuzo by the way, angeposti kuhamasisha watu wapige kura ili ushindi uje nyumbani.

Yanga: Lazima tuwachinje

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli.
Waandishi Wetu, Dar es Salaam
YANGA leo inatarajiwa kujitupa Uwanja wa Taifa kuvaana na Telecom FC ya Djibouti katika mchezo wa pili wa Kombe la Kagame. Ni lazima wawachinje .
Yanga wanatakiwa kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huu baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Gor Mahia na kama wakipoteza na huu, basi watakuwa wamejiweka kwenye mazingira magumu sana.

Saturday, July 18, 2015

GLOBAL TV ONLINE: MAHOJIANO YA MWISHO YA GLOBAL TV NA BANZA STONE, HALI ILIVYO KATIKA MSIBA WAKE

HATIMAYE WEMA AMWANGUKIA KAJALA

wema (8)
Staa wa filamu za bongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
Musa mateja
HAKUNA mwanzo usiyokuwa na mwisho! Huu ni usemi pekee ambao umejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Endless Fame Production na mbunge mtarajiwa wa Viti Maalum mkoani Singida kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu baada ya kumwangukia aliyekuwa shostito wake, Kajala Masanja ‘Kay’.
MWISHO WA MATUSI?
Wema na Kajala wamekuwa na bifu zito lililokuwa likichukua sura mpya kila kukicha kufuatia wawili hao kutokusameheana, kutukanana na kukashifiana ambapo Wema alifikia hatua ya kumwita mwenzake ‘bogasi’ na yeye (Kajala) akamwita chizi.
Tukio la Wema kujishusha na kutoa kauli ya kusema yuko tayari kumsamehe Kajala aliitoa mbele ya mwandishi wetu, Julai 15, mwaka huu ndani ya Ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
masanja1Kajala Masanja ‘Kay’.
WEMA AFUNGUKA
Wema alifunguka hayo baada ya kuulizwa hatima ya bifu lake na Kajala  ambapo alisema kwa sasa yupo tayari kabisa kumsamehe Kajala ambapo aliapa kwamba hata ikitokea wakutane popote hawezi kumuonyeshea kinyongo cha aina yoyote.
Alisema pamoja na kushindwa kukutana na Kajala kwa muda mrefu lakini nafsi yake imeshamsamehe na imemuongoza kufanya hivyo.
Wema alisema kuwa kila jambo lina mwisho wake, hivyo amekaa chini na kufikia uamuzi huo ambao anaamini kabisa hapa duniani hakuna mtu asiyekuwa na moyo wa huruma.
Aliongeza kuwa pamoja na yote yaliyotokea awali, hana budi kuyapuuzia kwa sasa, hivyo yuko tayari kukutana na kukaa na Kajala  kwani moyoni hana kinyongo chochote.
wemanakajalaKajala na Wema wakipozi pamoja.
SINA TATIZO NA KAJALA
“Kiukweli kabisa nimeshamsamehe Kajala, sina tatizo naye, hivyo muda wowote akinihitaji kwa lolote sina kinyongo kabisa.
“Nimefikiria kwa kina, nikaona sina sababu ya kuendelea kuwa na chuki naye na kupitia hilo namuomba Mungu aendelee kuniongoza ili nifute kabisa hilo wazo la chuki moyoni.
“Nipo radhi kukutana naye mahali popote pale endapo atanihitaji au mimi nitakapomuhitaji nitamtafuta,” alifunguka staa huyo na kuongeza:

MFANYAKAZI CLOUDS MBARONI

IMG-20150714-WA0001-1
Cynthia Maximillian ambaye alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Clouds Media Group anayedaiwa kutiwa mbaloni kwa utapeli.
Musa Mateja
MREMBO aliyetajwa kwa jina la Cynthia Maximillian ambaye alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya Clouds Media Group  amejikuta akitiwa mbaroni kwa madai ya kutapeli mamilioni ya shilingi ya wafanyakazi wenzake na marafiki aliosoma nao.
Taarifa zilizotua kwenye gazeti hili zinadai kuwa, Cynthia alitiwa rumande katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar Julai 13, mwaka huu.
IMG-20150714-WA0003-1Ilidaiwa kuwa, mrembo huyo ambaye kwa sasa ameachishwa kazi kwenye kampuni hiyo aliwakusanya marafiki zake na kuwapa mchongo kuwa, kuna viwanja vinapatikana huko Bagamoyo kwa shilingi mil1.5 kupitia Chama cha Mazingira Fukayosi.
“Baada ya kuona fursa tulijikusanya na kumpa Cythia pesa, kila mmoja alitoa milioni moja na nusu, na tulikuwa watu kama mia hivi akiwemo bosi Ruge Mutahaba. Cha ajabu baada ya kukamata mshiko huo akaleta usanii,” alidai mmoja wa wafanyakazi waliolizwa aliyeomba hifadhi ya jina lake.
IMG-20150714-WA0002-1Kufuatia utapeli huo, Cynthia alisakwa na kufikishwa polisi kisha kufunguliwa jalada la kesi lenye namba; OB/IR/6025/2015 KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu aliongea na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba ambaye alikiri kuwa miongoni mwa waliolizwa wamo wafanyakazi wa Clouds akiwemo yeye.
“Ni kweli hata mimi Cynthia ameniingiza mjini na tumepata taarifa za kutiwa kwake mbaroni ila watu wajue kwamba kwa sasa siyo mfanyakazi wetu maana tayari alikuwa ameshaachishwa kazi. Wananchi wajue kwamba sisi kama Clouds hatuhusiki na utapeli huo bali ni waathirika,” alisema Ruge.

Thursday, July 16, 2015

MKUBWA FELA KUWANIA UDIWANI MBAGALA KWA TIKETI YA CCM

Fela (kulia) akikabidhiwa fomu za kugombea udiwani 
MKURUGENZI wa kundi la Yamoto Band, Said Fela leo amechukua fomu za kuwania udiwani katika Kata ya Kilungule, Mbagala, Temeke, Dar es Salaam.
Fela ambaye pia ni mwasisi wa kundi la TMK Wanaume Family na Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe kinachosimamia bendi ya vijana machachari wa Yamoto, ameamua kuchukua fomu hiyo na kugombea nafasi hiyo ili aweze kutatua kero za wakazi wa kata ya Kilungule na kuleta maendeleo katika Kata hiyo.
"Nimeamua kuchukua nafasi hii ili kutatua kero za kata yangu, hapa kuna shida ya maji na barara naamini nikiwa Diwana nitaweza kuonana na wakubwa wa nchi uso kwa uso,"amesema.
Mkubwa Fela akijaza fomu za kuwania Udiwani

Wednesday, July 15, 2015

SAIDI FELLA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KATA YA KILUNGULE
Meneja wa kundi la Wanaume Famili pamoja na Yamoto Bendi Saidi Fella akiwa katika picha na baadhi ya wajumbe wa Kata ya Kilungule muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea katika nafasi ya Udiwani.
HAYA ndiyo maneno yake aliyoongea mara tu baada ya kuchukua fomu hiyo: Na shukulu MUNGU Leo nimethubutu kuchukua fomu ya udiwani kata mpya ya Mbagara Kilungule wadau naomba dua zenu", MANENO YAKE HAYO.


BOSI WA MABASI YA J4 AWAPIGA KWA RISASI WATU WAWILI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Charles Mkumbo.

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya J4 Express Juma Mahende mkazi wa Nyakato jijini Mwanza kwa tuhuma za kuwaua wakazi wawili wa jijini humo kwa kutumia bastola usiku wa kuamkia leo katika eneo la Nyakato sokoni. Marehemu hao wawili wametambuliwa kuwa ni Ally Mohamed Abeid mkazi wa Igoma na Claude Sikalwanda mkazi wa Nyasaka. Wakizungumzia mauaji hayo kwa masikitiko makubwa huku wakibubujikwa na machozi, kaka wa marehemu Ally Mohamed Abeid aitwaye Ramadhan Mohamed Abeid pamoja na dada wa marehemu Claude, Bi. Aziza Steven Sikalwanda wamevitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinatenda haki katika uchunguzi wa suala hilo. Mjane wa marehemu Ally Mohamed Abeid, Bi. Dominata Gabriel pamoja na mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi marehemu Ally Mohamed Abeid iliyoko eneo la Igoma Bw. Roger Rwegasira wanaeleza walivyopokea taarifa za kuuawa kwa watu hao. Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo ameeleza mazingira ya vifo vya watu hao ambao wameuawa kwa kupigwa risasi kifuani huku pia akiwaonya baadhi ya wamiliki wa silaha kuacha tabia ya kuzitumia ovyo kinyume na sheria na utaratibu.

Thursday, July 9, 2015

BARAKAH DA PRINCE & RUBY - NIVUMILIE

DIAMOND, ZARI KIMENUKA

OHOOO! Wakati penzi lao likitarajia matunda ya kupata kijacho miezi kadhaa ijayo, uhusiano wa Nasibu Abdul ‘Diamond na staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ umedaiwa kutibuka baada ya Diamond kufunguka kuwa anampenda mwigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde, Amani linakupa mchapo.Mkali wa Bongo fleva Nasibu Abdul ‘Diamond.
Diamond aliitoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Lagos alipokuwa akihojiwa redioni ambapo alipoulizwa ni wasanii gani maarufu anavutiwa nao kimapenzi, bila hiyana, mkali huyo kutoka Tandale-Dar, alisema ni Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.
WAMBEA WASHIKIA BANGO
Mara baada ya Diamond kutamka kauli hiyo na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, ‘wambea’ walilivalia njuga suala hilo na kumfikishia maneno Zari, ambaye naye anadaiwa kuyaamini na kumcharukia Diamond.

BELLA KOMBO AAMUA KUOKOKA!


Mshiriki wa Bongo Star Search (BSS), mwaka 2010/2011, Bella Kombo.
Shani ramadhani
MSHIRIKI wa Bongo Star Search (BSS), mwaka 2010/2011, Bella Kombo ameweka wazi kuwa sasa hivi ameamua kumtumikia Mungu na kuachana na muziki wa kidunia aliokuwa akiufanya awali.
Akipiga stori na Amani, Bella alisema baada ya Shindano la BSS alikuwa anaimba katika bendi na pia ameshafanya kolabo na wasanii kama Hemed Phd, Tunda Man, Kala Jeremiah, Steve RnB, lakini mwaka jana aliamua kurudi rasmi kwenye nyimbo za Injili.
“Nimekulia kwenye familia ya watu waliookoka kwa hiyo sijaanza kuokoka hivi karibuni ni malezi ambayo nimekuwa nayo tangu nimezaliwa na ninayaendeleza mpaka sasa, niko kwenye maandalizi ya kutoa albamu yangu ya nyimbo za Injili,” alisema Bella.

Wednesday, July 8, 2015

MENEJA: KAJALA AMEPONA


Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
Gladness Mallya
MIEZI michache baada ya Kajala Masanja kugundulika kuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye kizazi, meneja wa msanii huyo, Leah Richard amesema hivi sasa yupo sawa kufuatia upasuaji wa mafanikio aliofanyiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Kajala kwa sasa yupo fiti na tatizo la uzazi limeisha, hivyo mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kabisa kwani atarejea kazini kuendelea kuwapa burudani,” alisema meneja huyo baada ya simu ya msanii huyo kukosekana hewani.
Kajala, mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri katika Bongo Movie, alipatwa na wasiwasi baada ya kugunduliwa kwa uvimbe huo tumboni akihofu kutozaa tena, lakini kwa mujibu wa meneja wake, mafanikio hayo yamempa faraja kubwa na kumshukuru Mungu.

NAPE: HAKUNA NAFASI YA KUKATA RUFAA MAJINA YAKIKATWA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama  cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye. 
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama  wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.
Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari  wakati  akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.

Kikao hicho kitaongozwa  na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.
Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.

“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.
Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Aidha amebainisha  kuwa  hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.
Kwa mujibu wa ratiba  ya kikao,Kamati Kuu itakutana tarehe tisa  na kutoa wagombea watano kabla ya Halmashauri Kuu kukutana  tarehe 10mwezi huu, ambapo majina matatu ya wagombea yatateuliwa kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu tarehe 11 ili kumpata mgombea mmoja atakaepeperusha  bendera ya chama hicho.

ALIYEZAA NA NAY ANASWA NA KIDUME UGANDA

Gladness Mallya KABAANG! Zilipendwa wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amezua gumzo la aina yake baada ya kunaswa na ‘kidume’ kingine nchini Uganda.
Zilipendwa wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichowafuatilia wawili hao hatua kwa hatua, mpango mzima ulianzia jijini Mwanza ambapo Siwema alionekana akiwa na mwanaume huyo (jina halikupatikana mara moja) wakipeana kampani utadhani ni wapenzi.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, wawili hao walipanda basi la Friends jijini Mwanza ambapo Siwema na mwanaume huyo walikuwa beneti nje na ndani ya gari.
Siwema akiwa na kidume hicho.
Kilieleza kuwa, wakiwa mpakani Mtukula wawili hao walikuwa wakipiga stori, kula chakula na vinywaji pamoja ambapo walipofika Kampala, Uganda walikatiza mitaani na kufikia kwenye Hoteli ya HBT.

WEMA AGUNDULIKA NA GONJWA LA AJABU

Musa Mateja
Habari mbaya ikufikie kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame Films Productions ambaye yupo kwenye harakati za kuwania Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Wema Isaac Sepetu amegundulika kuwa na gonjwa la ajabu linalomsababishia kukosa raha ambalo linakua kadiri siku zinavyosonga.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu.
Gonjwa hilo limegundulika hivi karibuni machoni mwa paparazi wetu baada ya kumuona mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006 akiwa na bonge la nundu nyuma ya shingo, jambo lililomfanya paparazi ashindwe kujizuia na kuamua kumuuliza Wema.
MIAKA 26 MWILINI
Bila kupepesa macho Wema alisema kuwa ‘uvimbe’ huo upo mwilini mwake kwa zaidi ya miaka 26 sasa na umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.
Wema alilazimika kufunguka zaidi baada ya paparazi wetu kumuona sehemu hiyo ikiwa imemvimba bila kujua kama ni tatizo lake la miaka yote.
Sehemu ya shingo iliyoonekana kuvimba.
HATA MAMA YAKE?
Wema alitolea ufafanuzi jambo hilo kwa kusema kuwa huo si uvimbe bali ni nundu ambayo amekuwa nayo tangu mwaka mmoja baada ya kuzaliwa na hata mama yake mzazi, Miriam Sepetu pia yuko hivyo.“Huu siyo uvimbe mpya, ujue mimi niko hivi na hii nundu ipo siku nyingi, sema imekuwa ikiongezeka kadiri siku zinavyosonga.
LAMKOSESHA RAHA
“Kweli tatizo hili linanikosesha raha. Nimekuwa nikisuka nywele ndefu na mara nyingine mawigi yangu ni marefu hivyo watu huwa hawanigundui.“Nadhani hili ni tatizo la kifamilia maana mama yangu pia yuko hivihivi isipokuwa mimi linaonekana kuwa kubwa sana,” alisema Wema.
MTU WA KARIBU
Paparazi wetu aliendelea kuchimba kwa watu wa karibu wa Wema ili kujua kama ni kweli hiyo nundu ipo siku zote au alipata ajali, jambo ambalo lilikuwa hivyo kutokana na majibu ya Petit Man ambaye alisema kuwa wao hata hawamshangai tena Wema maana hiyo nundu ipo kitambo na kuna muda huwa wanamtania kwa kumuita jina la Kinundu.
“Haaa! Wewe ulikuwa hujui kama Wema ana nundu, mbona ipo siku nyingi tu, sema huwa anaifunika na nywele na ndiyo maana haionekani sana, muda mwingi watu wamekuwa hawaigundui kwa kuwa ipo nyuma ya shingo, labda ingekuwa mbele au pembeni nadhani kila mtu angekuwa anaiona,” alisema Petit Man.
DAKTARI AFAFANUA
Akizungumza na gazeti hili, daktari maarufu jijini Dar, Godfrey Chale ‘Dokta Chale’ alifafanua kwamba ugonjwa huo kitaalam unajulikana kwa jina la Lipoma na huwa ni mkusanyiko wa nyama ya mafuta kwa ndani hivyo ukubwa wake ukizidi huwa ni gumu.
“Uvimbe huo ukishakuwa na ugumu huo unaotokana na kuwa kubwa husababisha mishipa ya damu kugandamizwa, hali inayomsababisha mgonjwa kuumwa na kichwa kwa upande wa nyuma.
“Pia huaribu muonekano wa kawaida wa mtu,” alisema Dk. Chale na kuongeza:
“Inabidi Wema amuone daktari kwa vipimo na upasuaji ili kuondoa uvimbe huo.”

Monday, July 6, 2015

NI VIDEO GANI KALI KATI YA NANA Vs CHEKETUA

UKAWA wajitoa rasmi Bungeni, waondoka Dodoma leo

Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika vyama vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa hawajaadhibiwa.
Umoja huo pia umemtaka Rais Kikwete kutotia saini muswada hiyo kwa kuwa imepitishwa kinyume cha taratibu.
Mbowe amesema kuwa endapo Rais Kikwete atalazimisha kuisaini miswada hiyo, umoja huo utaishitaki serikali kwa wananchi.
Wabunge wote kutoka UKAWA wameazimia kuondoka kabisa leo kutoka mjini Dodoma, na wanataraji kukutana jijini Dar es salaam siku ya Jumatano kwa hatua zaidi.

Wakati huo huo bunge limepitisha muswada wa usimamizi wa mapato yatokanayo na mafuta na gesi, na muswada mwingine wa uwazi na uwajibikaji katika uchimbaji wa madini, gesi na mafuta, hiyo ikiwa ni miswada miwli kati ya mitatu ambayo imekuwa ikipingwa na wabunge kutoka UKAWA.
Muswada mwingine ni ule wa sheria ya Petroli ambao ulipitishwa jana bila ya ushiriki wa wabunge hao.
EATV imefanya mahojiano na Mh. Tundu Lissu mara baada ya kutangazwa kwa msimamo huo wa UKAWA, na hapa anaeleza zaidi:-

JIDE ALA BATA CHINA!

GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini Hong Kong, China akila bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.
Staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.
Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.
Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.
Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.
Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.

BANZA TUMWACHIE MUNGU!

Ugua pole! Hali ya mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ni ya kumwachia Mungu kwani bado ni tete na watu wamekuwa wakimiminika kwa ajili ya kumuona katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar alikolazwa.
Mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ akiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar alikolazwa.
Ijumaa Wikienda lilitia maguu kwenye hospitali hiyo na kufanikiwa kumuona Banza ambaye kwa wakati huo alikuwa amezungukwa na watu mbalimbali, wakiwemo wanamuziki wenzake wa dansi wengi wakiwa ni wale wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
Akipewa kikombe cha uji.
“Yaani inahuzunisha kwani huyu siyo yule Banza tuliyemzoea, hali yake hii ni ya kumwachia Mungu tu kwani ndiye anayejua kila tatizo linalomtokea binadamu litaondokaje, kikubwa ni kuendelea kumuombea tu maana hatua aliyopo siyo nzuri, ni Mungu tu aweke mkono wake,” alisema mmoja wa wanamuziki ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini.
Naye kaka wa Banza, Hamis Masanja alisema waliamua kumpeleka hospitali kutokana na hali yake kuwa mbaya ambapo Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka akiwa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) walifika nyumbani kwa ajili ya kumjulia hali ndipo wakaafikiana kumpeleka hospitali.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.

Banza akiwa na afya yake jukwaani.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linaungana na Watanzania kumuombea Banza Mungu amponye kwa neno lake kutoka kwenye Kitabu cha Yeremia 30:17 linalosema: “Kwa maana nitakurudishia afya nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana kwa sababu wamekuita mwenye kutupwa wakisema ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.”

Thursday, July 2, 2015

DIAMOND AKIRI KUMPENDA OMOTOLA

Mwandishi wetu
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde, Ijumaa lina stori kamili.
King wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza katika vyombo vya habari.

OMOTOLA_NdaniTV_Daniel-Sync-PHOTOS-13-Edited-1Staa wa Nollywood nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde ‘Omotola’.
“Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.
“Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.
Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.
“Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.Diamond hakupatikana ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.

LULU AMWAGA MINOTI KWENYE PATI!

Waandishi wetu
ULE msemo wa ‘pata pesa tuone tabia yako’ huenda ni kweli, kufuatia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ambaye siku hizi anaitwa ‘tajiri mtoto’ kutokana na kuwa na fedha na kumwaga ‘minoti’ (pesa) kwenye pati, Ijumaa ‘Kubwa’ lilikuwepo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, ishu nzima ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye pati ya ‘bethidei’ ya mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mastaa na mapedeshee kibao wa ‘mujini’ walihudhuria.
LULU AMWAGA MINOTI
Ilielezwa kwamba, Lulu alifanya ‘kufuru’ hiyo baada ya waalikwa wa pati hiyo kumaliza kula na kunywa ambapo ikafika wakati ratiba ikaelekeza watu kutoa zawadi kwa kadiri watakavyojisikia au kujaliwa nacho.
Ndipo Lulu ambaye siku hizi amekuwa hapendi kujitokeza kwenye shughuli, alipita mbele na kuanza kumpa noti nyekundu ‘Msimbazi’ aliyekuwa akizikusanya kwa niaba ya Kalala Junior kwa staili ya moja-moja.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akihesabu minoti.
Shuhuda wetu alidadavua kuwa, kila aliponyoosha mkono kutoa Msimbazi mmoja, watu walimkodolea macho wakiamini hawezi kufika ‘kilo moja’ (Sh. 100,000).
MANENO YA WATU
“Lulu bwana, anajitutumua tu. Hawezi kumpa laki moja Kalala Junior. Kwanza sidhani kama siku hizi ana pesa za kufanyia fujo,” alisema mwalikwa mmoja, mwenzake akampinga.“Wee! Lulu siku hizi ana pesa. Wenzake wanamuita tajiri mtoto. Ndiyo maana ana jeuri ile,” alisema mwingine miongoni mwa waalikwa hao.
Hata hivyo, Ijumaa halikuweza kufuatilia noti hizo katika mtiririko wa kutoka ili kujua ni shilingi ngapi bali baada ya kumaliza, lilimfuata Lulu ili kumuuliza ambapo hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Mtu wa karibu na Lulu ambaye aliomba jina lihifadhiwe, aliliambia Ijumaa kuwa, Lulu siku hiyo alitenga shilingi milioni moja na laki nne (1,400,000) kwa ajili ya kumtuza Kalala Junior tu.“Hawezi kusema, lakini mimi ninavyojua alitenga milioni moja na laki nne. Lulu kwa sasa yuko vizuri kipesa,” alisema mtu huyo na kuachana na Ijumaa.
KWA NINI LULU ALITOA KIASI HICHO CHA PESA KWA KALALA JUNIOR?
Habari za ndani zinasema kuwa, Lulu aliamua kumwaga mkwanja huo kwa vile, mwanamuziki huyo kwa sasa ni mpenzi wa shoga kipenzi wa Lulu, Rose Alphonce ‘Muna’.
Wakati wa matatizo ya Lulu kuswekwa Magereza ya Segerea, Dar kwa madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Muna ndiye aliyebeba jukumu la kumpelekea chakula mahabusu huyo kila siku.
Lakini pia, Lulu alipotoka gerezani kwa dhamana, alikwenda kuishi kwa muda nyumbani kwa Muna, Mwananyamala jijini Dar.
MAPEDESHEE NAO
Baada ya Lulu kumaliza kutuza minoti yake, mapedeshee waliokuwa ukumbini humo nao walicharuka ambapo walichomoa minoti yao na kuimwaga kwenye maboksi mawili na kutolewa ukumbini hapo na wapambe.
KUMBE KALALA ALIFANYIWA SAPRAIZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya ukumbi huo, Kalala Junior akiwa hajui chochote, mpenzi wake huyo ambaye pia ni msanii wa filamu, alimtaka watoke kwa ajili ya kupata chakula cha jioni ambapo walikwenda kwenye hoteli hiyo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Kalala Hamza ‘Kalala Junior’.
Baada ya kufika, Kalala alipokelewa na watu waliokuwa ukumbini hapo huku wakimmwagia maji, bia na soda hadi akawa chapachapa huku wakimwimbia nyimbo za ‘hepi bethidei tu yuuu…’ jambo ambalo hakulitegemea.
Kutokana na kulowa chapachapa, Muna alimchukua hadi kwenye chumba alichochukua mapema ndani ya hoteli hiyo ambapo alimbadilisha nguo.
Muna alimvalisha Kalala suti yenye gharama ya shilingi 2,800,000, viatu vya shilingi 800,000 (inadaiwa ni vya kutoka Italia), vyote hivyo alivinunua mwanadada huyo ikiwa ni zawadi kwa mpenzi wake.
Wawili hao walirudi ukumbini ambako walipokelewa kwa shangwe huku mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ akiwa ni mshehereshaji (MC) wa shughuli hiyo ambayo kwa kuangalia tu iligharimu mamilioni ya shilingi.
KALALA AMFUNGUKIA MUNA
Kufuatia mbwembwe hizo za Muna, Kalala alitumia nafasi hiyo kumtambulisha rasmi kwamba ndiye mchumba’ke wa sasa na kumshukuru kwa kumwandalia sherehe kubwa na ya gharama kwani hakuwahi kufanyiwa hapo awali.
MAIMARTHA ATIA NENO
Naye mshereheshaji wa shughuli hiyo, Maimatha aliliambia gazeti hili kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ya aina yake na yeye alilipwa zaidi ya shilingi milioni moja.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...