Saturday, July 18, 2015

HATIMAYE WEMA AMWANGUKIA KAJALA

wema (8)
Staa wa filamu za bongo, Wema Sepetu ‘Madam’.
Musa mateja
HAKUNA mwanzo usiyokuwa na mwisho! Huu ni usemi pekee ambao umejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Endless Fame Production na mbunge mtarajiwa wa Viti Maalum mkoani Singida kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu baada ya kumwangukia aliyekuwa shostito wake, Kajala Masanja ‘Kay’.
MWISHO WA MATUSI?
Wema na Kajala wamekuwa na bifu zito lililokuwa likichukua sura mpya kila kukicha kufuatia wawili hao kutokusameheana, kutukanana na kukashifiana ambapo Wema alifikia hatua ya kumwita mwenzake ‘bogasi’ na yeye (Kajala) akamwita chizi.
Tukio la Wema kujishusha na kutoa kauli ya kusema yuko tayari kumsamehe Kajala aliitoa mbele ya mwandishi wetu, Julai 15, mwaka huu ndani ya Ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
masanja1Kajala Masanja ‘Kay’.
WEMA AFUNGUKA
Wema alifunguka hayo baada ya kuulizwa hatima ya bifu lake na Kajala  ambapo alisema kwa sasa yupo tayari kabisa kumsamehe Kajala ambapo aliapa kwamba hata ikitokea wakutane popote hawezi kumuonyeshea kinyongo cha aina yoyote.
Alisema pamoja na kushindwa kukutana na Kajala kwa muda mrefu lakini nafsi yake imeshamsamehe na imemuongoza kufanya hivyo.
Wema alisema kuwa kila jambo lina mwisho wake, hivyo amekaa chini na kufikia uamuzi huo ambao anaamini kabisa hapa duniani hakuna mtu asiyekuwa na moyo wa huruma.
Aliongeza kuwa pamoja na yote yaliyotokea awali, hana budi kuyapuuzia kwa sasa, hivyo yuko tayari kukutana na kukaa na Kajala  kwani moyoni hana kinyongo chochote.
wemanakajalaKajala na Wema wakipozi pamoja.
SINA TATIZO NA KAJALA
“Kiukweli kabisa nimeshamsamehe Kajala, sina tatizo naye, hivyo muda wowote akinihitaji kwa lolote sina kinyongo kabisa.
“Nimefikiria kwa kina, nikaona sina sababu ya kuendelea kuwa na chuki naye na kupitia hilo namuomba Mungu aendelee kuniongoza ili nifute kabisa hilo wazo la chuki moyoni.
“Nipo radhi kukutana naye mahali popote pale endapo atanihitaji au mimi nitakapomuhitaji nitamtafuta,” alifunguka staa huyo na kuongeza:

KUTOKA MOYONI
“Najua itakuwa ngumu sana kwa watu kuniamini kwa sababu hapo nyuma kulikuwa na mambo mengi kati yetu, naendelea kuwatoa wasiwasi kwa kuwaambia tena kuwa tayari moyo wangu umeshamsamehe Kajala na nimejishusha kwa kila hali kwake.
“Nipo radhi kukutana naye mahali popote tukaongee ili wale wanaohisi sijamsamehe waamini hilo.”
Baada ya paparazi wetu kuhakikishiwa taarifa hiyo na Wema kwa kauli za kumsamehe zaidi ya mara moja huku akionyesha unyenyekevu na kujishusha kwa asilimia mia, alimtafuta Kajala ili kujua moyoni mwake ana nini juu  ya Wema.
KAJALA ROHO KWATU
“Kwanza nashukuru kusikia hivyo, binafsi sina tatizo na hilo, kikubwa namshukuru maana nimekuwa nikimuomba Wema kupitia sehemu mbalimbali ili tumalize tofauti zetu lakini alikuwa akikataa, ila kama mwenyewe anasema yupo tayari tuyamalize, kwangu ni furaha.
“Nimekuwa nikipigania hilo kila kukicha, sasa naamini Mungu atakuwa amesikia kilio changu kwa mara nyingine, napenda kusema sina tatizo lolote katika hilo,” alisema Kajala.
WEMA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE
Msamaha huo umekuja siku moja kabla ya Wema kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Mjini kupitia CCM ambapo juzi Julai 15, mwaka huu alichukua fomu na anatarajia kuirejesha kesho Jumapili.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...