Sunday, March 30, 2014

MSHINDI WA TUZO YA MWANAMKE BORA WA MWAKA TZ,AKIBIDHIWA TUZO YAKE NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

 Dk. Maria Kamm ametwaa tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 iliyotolewa na Global Publishers akiwashinda Dk. Migiro, Prof. Tibaijuka na Anne Kilango,tukio hilo lilifanyika jana mjini Dodoma.

WAZIRI MKUU AJUMUIKA KWENYE MAZIKO YA MKUU WA MKOA WA MARA MAREHEMU JOHN TUPA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, kwenye mazishi yaliyofanyika nyumbanikwa marehemu, Kilosa Machi 29, 2014.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu, Kilosa, Machi 29, 2014.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimfariji Mzee Gabriel Tupa baba mzazi wa aliyekuwaMkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kilosa achi 29, 2014.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA UDOM WAAHIDI KUJIUNGA NA PPFMeneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.


Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, John Mwalisu, akitoa mada kwenye semina ya siku mbili, iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada.
WANAFUNZI wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameridhishwa na mada mbalimbali zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, na wameahidi kujiunga kwa wingi na Mfuko huo, kwani wengi wao wanatarajia kujiajiri, hivyo itakuwa fursa nzuri kwao kuandaa maisha yao ya baadaye watakapostafu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti chuoni hapo jana mara baada ya semina iliyoandaliwa na PPF kwa wahitimu wa elimu ya juu, walisema awali walidhani kwamba Mfuko wa Pensheni wa PPF ni kwa ajili ya wafanyakazi walioajiriwa tu, lakini sasa wamefahamu kuwa milango iko wazi hata kwa wale ambao wamejiari ili mradi tu wawe na umri wa kuanzia 18.

Mmoja wa wanafunzi hao, Oneck Mwalongo, alisema kwa muda wote ambao amekuwa chuoni alikuwa hajawahi kuona maofisa wa mifuko inayojihusisha na masuala ya hifadhi ya jamii wakifika kwa ajili ya kuwapa semina kuhusiana na fursa zinazotolewa, lakini PPF imekuwa ya kwanza kuwapa elimu hiyo.

"Lakini leo hii tunashukuru PPF wametufumbua macho kwani tulikuwa tunajua ili uwe mwanachama ni lazima uwe umeajiriwa, kwangu mimi nitajiunga na PPF kwa sababu kozi yangu ya sayansi ya kompyuta si lazima niajiriwe nitajiajiri mwenyewe," alisema Mwalongo.

Alisema mfumo wa uwekaji amana wa hiari ulioanzishwa na PPF utasaidia vijana wengi watakaokuwa wamejiajiri kujiwekea akiba.

Pia alisema amefurahishwa na mpango wa baadaye wa PPF wa kuanza kukopesha wanachama wake viwanja, kwani nyumba ndiyo jambo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Mwalongo, alisema wakati akiingia kwenye semina hiyo alikuwa hafahamu kama maisha ya kesho huanza kuandaliwa leo, hivyo atakapoondoka chuoni hapo ataanza kujiwekea akiba ili asikumbane na msemo wa fainali uzeeni.

"Nilikuwa sifahamu kama maisha ya kesho yanaandaliwa leo wamenionesha njia sasa naanza kuandaa maisha ya uzeeni," alisema.

Kwa upande wake, Elizaberth Elibarick, alisema PPF ni mfuko wa kujiunga nao hasa kwa kuzingatia mfuko huo una mfumo wa uwekaji amana wa hiari na unatoa fao la elimu kwa watoto wa mwanachama anapofariki akiwa bado kazini.

Alisema si jambo la mchezo Mfuko kumsomesha mtoto au watoto wa wanachama ambao wamefariki kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita na kizuri zaidi wanalipa mafao kwa wakati.

Naye Leonard Mgeja, alisema kupitia semina hiyo yeye na wanafunzi wenzake wameweza kufahamu vitu vya msingi ambavyo walikuwa hawafahamu kuhusiana na Mfuko wa PPF.

"Leo tumefahamu umuhimu wa maandalizi ya maisha ya baadaye tukiwa na umri mdogo ili kufanya mambo sahihi kabla ya kufikia uzeeni," alisema na kuongeza kwamba;

"Hivi sasa ambapo tunakaribia kwenda makazini tunaenda na mwanzo mzuri kwani hatutegemei kuajiriwa tu, bali na kujiajiri hivyo tutajiunga na uchangiaji wa hiari kama hatutakuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira."

Awali Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko huo, Lulu Mengele, aliwaasa wanafunzi hao wa mwaka wa mwisho zaidi ya 500 waliohudhuria semina hiyo, kujiunga na PPF kupitia Mfumo wa asili wa Pensheni au ule wa uwekezaji amana pale ambapo wataamua kujiajiri wenyewe.

“Mfumo wa uwekezaji amana, unaandikisha watu kutoka sekta isiyo rasmi, kama wakulima, wafugaji, machinga na mama lishe”. Alifafanua.

Katika mada ya uwekezaji amana, Lulu alisisitiza umuhimu wa kuweka akiba kwani matayarisho ya maisha ya kesho yanaanza sasa.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Pesnheni wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati, inayojumuisha Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, John Mwalisu, alisema PPF imeandaa semina hiyo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa chuo hicho kwa kuwa wao ndiyo wanaingia kwenye soko la ajira.

Alisema kutokana na wao kuwa na nguvu ya kuajiriwa au kujiajiri wameona ni vema kuwaelimisha namna nzuri ya kutunza akiba ili iwasaidie watakapokuwa fikia hatua ya kustaafu.

Thursday, March 27, 2014

INASIKITISHA WATOTO WATEKETEA KWA MOTO WAKIWA WAMELALA TABORA

Watoto hao walipokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambao chanzo chake inadhaniwa kuwa ni hitilafu za umeme.

Miili ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8)na mdogo wake Emmanuel Paul(3) ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani majira ya saa moja asubuhi peke yao huko eneo la mtaa wa Rufita Mwanza road Tabora mjini.HATIMAYE COLONEL MUSTAPHA AWAOMBA RADHI WANAWAKE WA AFRIKA MASHARIKI


Baada ya Nyota Ndogo wiki iliyopita kufanya maandamano na wanawake wengine mjini Mombasa Kenya kupinga kile walichokiita ‘udhalilishaji dhidi yao’ uliofanywa na rapper Colonel Mustafa na kumtaka awaombe radhi, mkali huyo wa ‘Lenga Stress’ amekuwa mpole na kuomba radhi

Mustafa ameliambia gazeti la The Star la Kenya:

“Wana sababu za msingi kama wanawake. Nawaomba radhi wanawake wote wa Afrika Mashariki waliochukizwa na picha lakini ningependa kusema kuwa, wanawake kwenye picha hizo hawakulazimishwa kupose. Siku hizi uanamitindo umeingia kwenye kugeuza mwili kuwa sanaa.”

Picha zilizoleta utata ni zile alizopiga Huddah Monroe.

Tuesday, March 25, 2014

WOLPER, HUSNA WAMGOMBEA MKONGO


 KUCHAMBANA, kutoleana lugha chafu ndiyo ishu iliyopo kwa sasa kati ya nyota wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011 iliyomtoa mlimbwende Salha Israel, Husna Maulid kufuatia madai kwamba, wanamgombea mwanamume Mkongo aliyejulikana kwa jina moja la Mwami.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Husna ndiye aliyeanza kuwa na uhusiano na Mkongo huyo mwaka jana na kila anapofika nchini hutanua naye kwenye ‘viwanja’ mbalimbali.

“Husna ndiye mwenye mwanaume, akija Bongo wako wote, lakini hivi karibuni ghafla tu, jamaa kaja na kuwa na Wolper, Husna kapigwa chini, sijui Wolper alimpatia wapi?” kilisema chanzo hicho.

Jumamosi iliyopita,mwandishi wetu alimtafuta Husna na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka kwa kusema:
“Ni kweli kabisa, Wolper amenichukulia mwanaume wangu. Mi nimemshangaa sana. Halafu eti ananitumia meseji za ajabu ajabu mimi, eti anasema hajanichukulia bali ni bwana ‘ake siku nyingi (huku akionesha meseji hizo).

Baadhi ya meseji hizo zinaonesha Husna akijibu mapigo upande wa pili huku akishambulia kwa maneno makali kufuatia madai kwamba anatembea na Mkongo wake.

“Jana (Ijumaa) alikwenda naye hoteli…(anaitaja jina) iliyopo Masaki (Dar), wakala chakula kisha wakaenda kulala hoteli… (pia anaitaja jina). Mimi najua kila kitu,” alisema Husna akionesha hasira.
Kwa mujibu wa Husna, awali siku hiyo alitaka kwenda kumfumania Wolper na Mkongo huyo kwenye hoteli waliyokuwa wakila chakula lakini machale kama yalimcheza wakaondoka.

Baada ya kuzungumza ana kwa ana na Husna, mwandishi wetu alimsaka Wolper kwa njia ya simu ili kumuuliza lakini hakupokea. Wakati mwingine simu yake ilipopigwa ilionekana kuwa bize.

Hata hivyo, ili kumpa nafasi zaidi ya kujieleza, Wolper alitumiwa meseji saa 5:05 asubuhi ikiwa na mashitaka yote ambapo ‘ilideliva’ kwenye simu yake, lakini pia hakuijibu.

Monday, March 24, 2014

ROSE MUHANDO SASA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA UPENDO HAPA BONGOTangazo limetegenezwa na Rumafrica +255 715851523

MUIGIZAJI JAQUE PENTZEL AWASHANGAZA WADAU KWA KUFANYA HIKI WAZI WAZI


Star wa bongo movie Jacque Steven Pentzel amewashangaza watu wengi kwa kutimiza mwaka mmoja wa ndoa yake ikiwa ni tofauti na mtazamo wa watu waliokua wakidhani ndoa iyo aitodumu ata miez mitatu, hatimae Tarehe 22 mwezi huu Jacque Pentzel ametimiza mwaka mmoja (Annivesarry) ya ndoa yake na mumewe Gadner Dibibi.
Jacque aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa "Namshukuru Allah kwa kuniwezesha kufikisha mwaka mmoja wa ndoa yangu na mume wangu kipenzi Bw. Gadner Dibibi, tumepitia mengi lakini Inshallah tunavumiliana"
Jacque alifunga ndoa mwaka jana Tarehe 22, March kwenye msikiti wa Magomeni Makuti na kubadili dini kuwa Muislam na hivi sasa anatambulika kwa jina la Kauthar Dibibi.Jacque Pentzel akiwa na Mumewe Gadner Dibibi siku walipofunga ndoa

KIGOGO MAGEREZA LA UKONGA ATESWA, AUAWA NA MWILI WAKE WATUPWA CHOONI...MKEWE AHUSISHWA


KIGOGO wa cheo cha juu katika Jeshi la Magereza Tanzania, SP Barnabas Nkuba (56) ameuawa kikatili kisha mwili wake kuburuzwa na kutupwa kwenye choo cha nje cha nyumba yake, Uwazi limeichimba.
Jeneza lenye mwili wa marehemu, SP Barnabas Nkuba (56) likiwa limebebwa na maofisa wa Jeshi la Magereza Tanzania.

Tukio hilo lililoacha maswali mengi lakini majibu kiduchu huku jeshi la polisi likihaha kuwanasa wauaji, lilijiri Machi 20, mwaka huu nyumbani kwake, Kitunda -Machimbo, Ilala jijini Dar es Salaam.

MAZINGIRA YA KUUAWA
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka Jeshi la Magereza, Ukonga, Dar alikokuwa anafanyia kazi mpaka kifo chake, huenda marehemu alitekwa kwanza, kisha akateswa na baadaye kuuawa kikatili.
“Ukiangalia mazingira yanaonesha bosi (marehemu) alitekwa kwanza, akateswa sana na baadaye kuuawa,” kilisema chanzo hicho huku kikiangua kilio cha utu uzima.

MWILI WAKUTWA CHOONI
Habari zaidi zinadai kuwa baada ya kumuua, watu hao waliuburuza mwili hadi kwenye choo cha nje ambako waliutupa ndani yake.
Ndugu na jamaa wa marehemu wakiomboleza msiba wa kigogo huyo.

Wengine walipingana na kauli hiyo, wakisema kuwa huenda afande huyo alipotekwa aliteswa kwanza kisha akaburuzwa hadi chooni akiwa hajiwezi ambako aliuawa.
“Mimi napingana na madai kwamba aliuawa kisha mwili wakautupa chooni kwa sababu, mwili ulikutwa chooni ndiyo lakini pembeni yake kulikuwa na vipande viwili vya matofali ambavyo huenda vilitumika kumpigia marehemu hadi kufa, maana mwili wake ulikutwa na jeraha usoni,” kilisema chanzo kingine.

KUNYONGWA KWATAJWA
Taarifa zingine zilidai kuwa marehemu ni kama alinyongwa kwanza kisha kupigwa na tofali hali iliyosababisha kifo chake cha kimyakimya bila kupiga kelele kwa vile matofali yaliyokutwa chooni hayakuwa na ukubwa wa kutumika kumpigia mtu hadi kufa.

Marehemu, SP Barnabas Nkuba enzi za uhai wake.

SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Vyanzo vingine vya habari vilisema kwamba siku ya tukio, marehemu alipotoka kazini alipitia dukani na kununua soda mbili ambazo polisi walizikuta mezani sebuleni zikiwa zimenywewa nusu.

MKEWE AHUSISHWA, AKAMATWA, KWA NINI?
Habari zaidi zilisema kwamba marehemu Nkuba alikuwa akiishi na mkewe, Cheula tu kwani watoto wao walikuwa masomoni.
Inasemekana kwamba marehemu alikuwa na mazoea ya kutangulia kufika nyumbani kabla ya mke wake kwa vile mwanamke huyo anafanya biashara ya kuuza chakula Ukonga-Mazizini, Dar na hurudi nyumbani usiku mwingi.

Ikadaiwa kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo aliwahi kurudi akiwa amepanda bodaboda.
“Mkewe ambaye ni mdogo, maana alimuoa baada ya mke mkubwa kufariki dunia, alipokaribia kwake na bodaboda inadaiwa alimwambia dereva kuwa asifike nyumbani kabisa kwa vile hali si shwari.
“Tunasikia kwamba aliposhuka alikwenda mwenyewe nyumbani kwake na kukuta mlango uko wazi. Akaingiwa na hofu.

“Basi, akaenda baa ya jirani na kuwaambia anaowajua kwamba amefika nyumbani na kukuta mlango uko wazi na kila akiipiga simu ya mumewe, haipatikani.
“Ndipo majirani hao na mwanamke huyo wakaenda nyumbani hapo na kuingia. hawakukuta mtu, hata walipoita Nkuba, Nkuba, wapi! Kimya!
“Walikwenda uani ambako walikuta alama za mburuziko wa kitu, wakazifuata hadi chooni ambako waliukuta mwili wa kigogo huyo akiwa ameshafariki dunia na ndipo polisi walipopewa taarifa.
“Mwili wake ulipelekwa Hospitali ya Amana, baadaye wakauhamishia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” kilisema chanzo.

Polisi walipofika, habari zinadai kuwa walimkamata mwanamke huyo kutokana na mazingira yenye utata.
“Tunasikia polisi walishangaa kama yeye ndiyo mwenye nyumba iweje akute mlango wazi ahofie kuingia wakati wanaishi wawili tu? Kwa nini asiingie na kumuita mumewe, pengine alipitiwa na usingizi?
“Halafu kingine, ni kwa nini alimwambia dereva wa bodaboda asimfikishe nyumbani hali si shwari? Ni hali gani hiyo ambayo haikuwa shwari wakati alikuwa hajaingia ndani?” kilihoji chanzo hicho.
Kwa cheo cha marehemu, angekuwa JWTZ nafasi yake ni meja, kwa jeshi la polisi angekuwa kamanda wa polisi wa wilaya (OCD).

Mwili wa marehemu Nkuba ulisafirishwa Machi 22, mwaka huu kupelekwa Shinyanga kwa mazishi. Ameacha watoto wanne. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

SHOPRITE IMEUZWA WAFANYA KAZI WAGOMA NA KUANDAMANA MLIMANI CITY


Jana mida ya Jioni pale mlimani City nimeshuhudia wafanya kazi wa Duka Kubwa la Shoprite wakiwa wamegoma wakizua watu wasiingie kwenye duka hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa duka hilo limeuzwa bila wao kupewa mafao yao …Habari zilizopo ni kuwa duka hilo limenunuliwa na Super Market Ingine kubwa Nchini Kenya Ambayo inakuja kupanua biashara zake hapa Dar …..

CHAKULA CHA UBONGO: BUNGE LA KATIBA LICHUNGULIE ZANZIBAR


Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.

Na Luqman Maloto
KICHWA kinauma kutokana na kufikiria jinsi Bunge Maalum la Katiba litakavyokuwa na kazi kubwa ya kuandika Katiba Mpya ya Tanzania huku kukiwa na vifungu katika Katiba ya Zanzibar ambavyo vinaashiria mambo mazito.

Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.

Moja ya vifungu hivyo ni katika Sura ya kwanza kifungu cha 1 cha katiba hiyo kinachosema kuwa Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka ambavyo kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanziabar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kifungu hicho ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema Tanzania ni Jamhurri ya Muungano na eneo lake la ardhi ni kuanzia Tanzania Bara hadi Zanzibar.

Hakuna ubishi kwamba kifungu hicho cha sheria ndicho kilichofanya kesi ya uhaini ya Zanzibar ambayo iliwahusisha viongozi wengi wa Chama Cha wananchi (CUF), akiwemo Maalim Seif Sharif Hamadi (pichani) kuachiwa huru na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania

baada ya kuonekana kuwa hakuwezi kufanyika Zanzibar uhaini kwa sababu eneo hilo siyo la nchi dola inayoweza kupinduliwa nje ya Tanzania.

Lakini Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ilisema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano, kwa maana hiyo katiba ya sasa ya Zanzibar inakana muungano kwa kuweka mipaka yake na kujitenga na Tanzania Bara.

Ibara ya 2(A) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka bayana kuwa pale rais anapotaka kuigawa Zanzibar, atashirikiana na Rais wa Tanzania Zanzibar, sasa sijui kama Baraza la Wawakilishi baada ya kupitisha sheria hiyo na kumkabidhi rais wa Zanzibar kabla ya kutia sahihi aliwasiliana na rais wa jamhuri?

Kama hakuwasiliana naye na tayari ameweka mipaka ya visiwa hivyo ni wazi Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amemkosea Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete kwani kwa maneno mengine mabadiliko hayo yamekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakika hayo ndiyo mambo ya kujadili wakati wa kupitisha vifungu hivyo vinavyohusu mipaka ya nchi. Kuna matatizo mengi sana ya kujadili na kupatia ufumbuzi lakini hili la muungano ndilo linalogonga vichwa vya watu wengi.

Ukweli ni kwamba nchi hii waasisi wetu walikuwa na nia ya kuifanya nchi moja na ndiyo maana walipoanza tu aliyekuwa Rais wa Zanzibar akawa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wazanzibar walikasirika baada ya cheo hicho kunyang’anywa rais wao na wakawa wanahoji, atakapokuwa anakuja katika baraza la mawaziri la Tanzania atakuja kama nani? Mjumbe tu wa kawaida? Hatukusikia jibu hadi leo.

Watu wa Unguja na Pemba baada ya kuona hivyo wakaamua kutengeneza katiba yao kama ilivyo sasa na wakatengeneza bendera yao na wimbo wao wa taifa. Haya yote wakati wa kuandikwa katiba mpya yaangaliwe kwa kina kwa sababu kulipua kunaweza kuzusha machafuko siku za usoni. Kazi kwenu wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

ZA KUAMBIWA NA JK, WARIOBA TUCHANGANYE NA ZETU


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa iliyopita alilizindua rasmi Bunge Maalum la Katiba kwa kutoa hotuba iliyokigawa chombo hicho muhimu kwa taifa kwa sasa, baada ya wajumbe wake kutofautiana misimamo.
Hotuba hiyo ya Rais, ilikuja siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya katiba hiyo mbele ya wajumbe hao hao.
Akiwasilisha rasimu hiyo huku akishangiliwa na wajumbe wengi, Jaji Warioba alisema suala la serikali tatu haliepukiki, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuunusuru Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hasa kwa vile tayari upande mmoja umeshavunja katiba ya sasa, kwa kujitangaza nchi kamili, haki ambayo inapaswa pia kutolewa kwa upande wa pili.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Lakini katika hotuba yake ya uzinduzi wa bunge hilo, Rais Kikwete, naye huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wajumbe, alisema mfumo wa serikali mbili ndiyo pekee unaopaswa kufuatwa, kwa sababu serikali ya tatu, siyo tu haitakuwa na chanzo cha uhakika cha mapato, bali pia inaweza kusababisha machafuko, hasa kama itashindwa kusimamia vizuri vyombo vya ulinzi na usalama.
Wakati Warioba aliwasilisha rasimu kama maoni ya wananchi yaliyoratibiwa na tume yake, Rais Kikwete alisema alichokisema ni maoni yake binafsi, licha ya ukweli kwamba msimamo huo unafanana na ule wa chama chake cha CCM.
Wote wawili, kila mmoja alipopata nafasi ya kusimama mbele ya wajumbe na taifa kwa jumla, walitoa sababu zinazounga mkono misimamo yao, kwa nini serikali tatu ni muhimu na jinsi gani serikali mbili zinavyoweza kudumisha umoja na mshikamano kama taifa.
Katika moja ya hotuba zake nyingi kwa taifa, Rais Kikwete aliwahi kutoa kauli moja ya msingi sana, kwamba akili ya kuambiwa, changanya na yako.
Huu ndiyo unaoweza kuwa ujumbe wangu kwa wajumbe wa bunge hili, ambao wataipitia, kuijadili na hatimaye kutupatia katiba mpya ya Tanzania ili wananchi tuweze kupiga kura ya maoni.
Nimezisikia hotuba zote mbili na ni lazima niwe mkweli kwamba maelezo ya kila upande yana ushawishi wa aina yake kwangu. Ni wazi kwamba kutakuwa na mvutano mkubwa wa mawazo wakati wa mjadala wa rasimu hii, ingawa zipo dalili kwamba mchakato mzima unaweza kutekwa na itikadi za kimakundi badala ya kuiweka nchi mbele.
Nionavyo, kwa jinsi hali ilivyo, ili tutembee katika maneno ya Rais Kikwete, ni lazima Zanzibar ikubali kuiondoa katiba yake, ili tubaki na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wapo baadhi ya watu wanaodai serikali tatu kwa sababu ya chuki tu, lakini hawana hoja yoyote vichwani mwao.
Na chuki hii inakuja kwa vile wanajiuliza mbona wenzao wa Zanzibar wana Katiba yao, inayoitambua kama nchi kamili, yenye wimbo wake wa taifa, yenye bendera yake na bunge lake, lakini Tanganyika ikiwa haina vitu vyote hivyo?
Wanaotetea muungano wa serikali mbili lazima wawe na jibu la kutosheleza maswali kama haya. Haitoshi tu kusema tutavunja muungano bila kupata muarobaini wa hili.
Na hata serikali tatu nazo zina maswali yanayohitaji majibu, kama chanzo chake cha mapato ni kipi na jukumu lake kama serikali ni lipi. Maana isije ikafikia wakati tunatengeneza serikali ya heshima (Ceremonial Government) isiyo na kazi ya maana ya kufanya.
Ndiyo maana tukasema katika suala la katiba ya nchi, ni jambo la hekima sana kila mmoja kuchanganya akili zake na zile za kuambiwa, tulizoletewa na Rais Kikwete pamoja na Jaji Warioba.
Wote kama taifa, ni lazima tukubali kwamba nchi yetu inahitaji mabadiliko ya kimfumo, vinginevyo taifa litaendelea kudumaa kiuchumi na kimaendeleo, licha ya rasilimali nyingi zilizopo ambazo wakati mwingine wanaofaidika nazo ni wachache kwa sababu ya ufisadi.
Ili hili lifanikiwe, ni lazima akili ya makundi tuiache. Tujadili na kupitisha vifungu bila kujali kama wewe ni Mpemba au Mtanganyika, bila kuhusisha chama chako cha siasa wala masilahi ya kundi unalowakilisha. Tunachohitaji ni katiba itakayowafaa Watanzania.
Asiwepo Mtanzania anayedhani yeye au kundi lake ni bora kuliko katiba tunayotaka kuitengeneza inayolenga kutumika sasa na vizazi vijavyo!

JB, TIMU YA EATV NIRVANA WAUVAMIA MJI WA LUSHOTO

Alfajiri ya Machi 6, timu ya Nirvana, Grow, pamoja na JB walielekea soko kuu la Lushoto ambapo walikutana na wakulima ili kusikia hadithi zao za mafanikio pamoja na changamoto. Nirvana na Kampeni ya GROW wanahamasisha lifestyle njema! Lakini tunavyokula vyakula bora, vyenye virutubisho tunajua vinatoka wapi!

Akizungumza kutoka katika sehemu yake ya biashara, Zinira Ally (kushoto aliyekaa) alishuhudia jinsi ambavyo anasomesha watoto na kulisha familia yake kwa pesa inayotokana na biashara yake ya uuzaji wa mbogamboga na matunda.

"Nzenze"... Salaam na wapenzi wa filamu zikiendelea.

JB, Lotus na Deo wakitizama mazao mbalimbali katika soko kuu la Lushoto.

Veronica Joseph ambaye ni muuzaji wa mboga mboga sokoni Lushoto anasema angependa kuona mabadiliko katika miundombinu ya soko ili kulinda ubora wa mazao, “soko halina ubora, watu wananunua vyakula hivi hivi kwa bei ghali kwenye supermarket kwa sababu ya ubora, sie tunauza tu bora tunauza, tunaogopa vyakula kuoza, tungekuwa na mafriji ya kuhifadhia mboga mboga na sisi tungeweza kuuza bei sawa na supermarket.”Akiendelea kutaja changamoto, Veronica ambaye ni mama wa watoto wawili, alionyesha kusikitishwa kwake na maisha duni wanayoishi wakulima, “mkulima analima chakula ambacho wengine wanakula hadi kutupa lakini yeye hawezi hata kula mlo kamili kwa sababu kipato anachopata ni kidogo” Veronica anaamini kama, “masoko yangeboreshwa, tungeuza bidhaa kwa bei nzuri ili na sisi tusomeshe watoto wetu na kujikimu kimaisha.”

Uvuvi unalipa..??

Ugeni umefika katika meza ya Asha Paulo (Kushoto) na Shakira Rashid (kulia), hawa ni wauzaji wa samaki katika soko kuu la Lushoto. Asha na Shakira wanaelezea jinsi ambavyo mikopo kwa wakulima na wafugaji isivyokuwa rafiki. Asha anasema, “mikopo ina masharti makali sana, sidhani kama inamlenga mtu wa hali ya chini kwani makato ni makubwa sana.”

Watangazaji wa kipindi cha Nirvana, Lotus na Deo walishangaa kuona apple zinazolimwa Tanzania. Kisado kimoja ambacho kwa wastani kina ma-apple ishirini (20) kinauzwa kwa Tshs. 2000 wakati kwa wastani apple moja jijini Dar es salaam linauzwa hadi Tshs. 1000. Baada ya kuonja, Deo anashangaa kuona ladha haipishani sana na ile ya matunda hayo yanayoagizwa kutoka nje. Ukweli ni kwamba miundo mbinu, technolojia, sera na mifumo iliyopo imewaangusha wakulima hapa Tanzania! Fikiria kwamba ni rahisi na kuna faida zaidi kusafirisha apple kutoka nje ya nchi kuliko hapa hapa Lushoto Tanzania!

Paulina Isaya (mwenye nguo nyeusi), muuzaji wa matunda apple katika soko kuu la Lushoto anasema, “kama wakulima wangepewa mafunzo sahihi, mbegu bora na kuhakikishiwa masoko, hakika matunda hayo yangekuwa na kiwango kama hayo yanayoagizwa kutoka nje”.

Taswira ya soko kuu la Lushoto kwa nje.

JB akiangalia kabichi zilizowekwa pembezoni mwa barabara. (Haikujulikana mara moja kama zilikuwa zinasubiri kusafirishwa ama la)

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani,iliyoadhimishwa Duniani kote mnamo Machi 5, kampeni ya Grow ikiongozana na mmoja wa mabalozi wake muigizaji Jacob Stephen ‘JB’ iliungana na kipindi cha EATV Nirvana na kuutembelea mji wa Lushoto,Jijini Tanga.

Kampeni ya GROW, inayoendeshwa na Oxfam, inahamasisha mabadiliko kwenye mifumo iliyopo ili iwafanufaishe wakulima na wafugaji/wavuvi wadogo wadogo hususani wanawake wawe na maisha endelevu! Inawasherekea kwa mchango wao mkubwa wa kulisha nchi huku wakipambana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa masoko, pembejeo na miundo mbinu. Katika harakati hizi, mnamo mwaka 2011, shindano la "Mama Shujaa wa Chakula " lilizinduliwa rasmi hapa nchini. Lengo la tuzo hii ni kutambua mchango wa wanawake hasa waishio vijijini.

OBAMA TO VISIT SAUDI ARABIA AFTER EUROPE TOURU.S. President Barack Obama (R) salutes as he boards Marine One to begin his travel to Europe from the White House in Washington March 23, 2014. ( U.S. President Barack Obama departed Washington on Sunday night for the Netherlands, his first stop on a four-nation trip that will include visits to Belgium, Italy and Saudi Arabia.

Obama is expected to arrive in Riyadh on Thursday and meet with King Abdullah to discuss a range of security issues in the Middle East that have caused some strains in the bilateral relationship.
“As part of regular consultations between our two countries, President Obama will travel to the Kingdom of Saudi Arabia in March 2014 to meet with His Majesty King Abdullah bin Abdulaziz al-Saud,” the White House said in a statement last month.

While his visit to the European countries will likely be dominated by Ukraine, his trip to the Gulf kingdom will include discussions about “Gulf and regional security, peace in the Middle East, countering violent extremism, and other issues of prosperity and security,” the statement added.


The last meeting between Obama (R) and King Abdullah was in 2010. (Reuters)
“The President looks forward to discussing with King Abdullah the enduring and strategic ties between the United States and Saudi Arabia as well as ongoing cooperation to advance a range of common,” the White House said.

The United States and Saudi Arabia have been allies since the kingdom was formed in 1932, giving Riyadh a powerful military protector and Washington secure oil supplies.
In recent months, both countries have been strained by regional crises and concerns.
In October, Saudi Arabia turned down a seat on the United Nations Security Council, in a display of anger at the failure of the international community to end the war in Syria.
It was then that Saudi Arabia’s intelligence chief said the kingdom was looking at making a “major shift” in relations with the United States.

In November, King Abdullah met Secretary of State John Kerry and discussed concerns about the unwillingness of the United State to intervene in Syria and recent overtures to its arch-rival, Iran.
Europe trip

Meanwhile, Obama will be taking his hard line on Russia to Europe and will see how far European allies are willing to go to stop Moscow from moving deeper into Ukraine after annexing Crimea.
In talks on Monday at The Hague with fellow leaders of the Group of Seven industrial democracies, Obama faces a test on whether he can bring along European allies to increase the pressure on Russia.
He has threatened U.S. sanctions against key sectors of the Russian economy. European allies have far closer economic ties to Russia than the United States and their still-fragile economies could face a backlash by getting tough with Moscow.

Russia provides almost a third of the EU's gas needs and some 40 percent of the gas is shipped through Ukraine.
"Europeans are committed to do something," said Jeffrey Mankoff, a Russian analyst at the Center for Strategic International Studies. "I think it'll be difficult to convince them to go anywhere near where the United States would like to go."
Russia's abrupt annexation of the Crimea region of southern Ukraine has presented Obama with an urgent foreign policy challenge, one that figures to weigh heavily on a second term that he prefers to devote to domestic affairs.


Source: english.alarabiya.net

ROSE MUHANDO KUFANYA TAMASHA LA UPENDO

Rose Muhando ambaye anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji anatarajia kufanya tamasha la UPENDO katika ukumbi wa wa kanisa la Baptist Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 06/04/2014, tamasha litaanza saa 7:00 mchana na kuendelea.
http://3.bp.blogspot.com/-uVpFLAt2Bmk/T4zS9Z9QIAI/AAAAAAAADFU/2p-ToGCMP3c/s1600/IMG_6572.JPG

 Lengo zima la kuandaa tamasha hili ni kukisaidia kituo cha watoto yatima cha HOCET kilichopo  Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam.  Kabla ya tamasha Rose Muhando atakwenda kukitembelea kituo hicho kwaajili wa kuwafariji na kuwatia moyo watoto hawa ambao wametoka katika mazingira magumu baada ya wazazi wao kutoweka dunia. Rose Muhando amesema atatoa msaada wake kama vile Mungu alivyomjalia. Kutakuwa na wasindikizaji watakaomuunga mkono malikia huyo wa muziki wa injili Tanzania Rose Muhando ni  waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania,  Stella Joel, Elizabeth Ngaiza na Janeth Mrema. |

Kuna nafasi ya kutosha kwako wewe ya kuweza kuungana na baraka hizi na kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Rose Muhando kwa kutoa kile ulichonacho ili watoto hawa ambao ni yatima waweze kujiona kama kuna watu wanaowajali na kuwatunza. Watoto hawa wanauhitaji wa vitu vingi kama vile mavazi, chakula, vifaa vya shule, matibabu na mengine mengi. Mungu amekujali kuwa na kidogo ulichonacho, ni vizuri ukashirikiana na hawa watoto wenye uhitaji ili Mungu aweze kufanya jambo katika maisha yako na kufungua milango iliyofungwa na adui yako kimafanikio.
Katika tamasha hili kutakuwa hakuna kiingilio, ila ni wewe kuja na sadaka au mchango wako kwaajili ya kuwasaidia hawa watoto yatima. Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama vile Stella Joel, Elizabeth Ngaiza, Julieth Dougras, Janeth Mrema, Christopher Malango, Tuamini Njole, Sifa John, Faraja Ntaboba, Kwaya ya Baptist  Magomeni, Kwaya ya Ukombozi, Subi Mwamezi, Christina Matai, John Shabani, Ado Novemba, Gideon Mutalemwa na Petro Mwampashi. Waimbaji hawa wameamua kujitolea kwa lengo la kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele. Watamtumikia Mungu siku hiyo na watachochea IMANI yako kuzidi kukua na kumtumainia Mungu wetu.

Bwana Yesu Kristo amehimiza sana katika kitabu kitakatifu (BIBLIA) juu ya upendo. Mimi na wewe tutakiwa sasa kuonyesha upendo  wetu kwa hawa yatima ambao ni walengwa wa siku hiyo. Na uppendo huu utakaouonyesha siku hiyo ukazidi kufanyika na kwa watu wengine.

Kama umeguswa basi unaweza kuwasilisha mchango wako katika ofisi za RUMAFRICA zilizopo Sinza Afrikasana eneo la soko la mbogamboga na matunda  au wasiliana na Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Elizabeth Ngaiza kwa simu +255 0714 294076 au 
Stella Joel +255 0756 846166

WATAKAO MUUNGA MKONO ROSE MUHANDO KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WANAOTOKA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
http://4.bp.blogspot.com/-d7R5tn4LwFE/ULD1Ig84iVI/AAAAAAAAANA/Zn3HYOhxi_Y/s1600/DSC_0134.JPG
Janet Mrema
http://3.bp.blogspot.com/-5TRvCOoRd7Q/UYFbSh6shnI/AAAAAAAAJSA/xgfRdd1T64w/s640/DSCN9611.JPG
Stella Joel
http://4.bp.blogspot.com/-5lD3n4nN4iU/UuNo9BG1nrI/AAAAAAAAVgc/X5rZZIh4Ha4/s1600/16.jpg
Elizabeth Ngaiza

KUTOA NI MOYO

Friday, March 21, 2014

BATULI AJIWEKA KWA CHIEF KIUMBEStaa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amedaiwa kujiweka kwa Pedeshee Chifu Kiumbe baada ya siku kadhaa zilizopita kumfuata na kumtaka amsaidie katika project ya filamu yake .
Staa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya msanii huyo kupewa sapoti ikiwa ni pamoja na gari la kushutia, mdada huyo amekuwa akijionesha kuwa pedeshee huyo ni mtu wake.

“Alipopewa sapoti hiyo akaona ndiyo ajiweke kabisa bila kujua kuwa Chifu Kiumbe alikuwa akimsaidia tu na wala hakuwa na wazo la kumtaka,” alidai sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
 
Pedeshee Chifu Kiumbe.
Baada ya habari hizi kunaswa, mapaparazi wetu walimtafuta pedeshehe huyo ambaye alisema: “Hata mimi nashangaa kusikia watu wakisema natoka na yule dada, ukweli sijawahi kuwa mpenzi wake alikuja kuniomba msaada wa project yake nikamsaidia hata gari nilimpatia lakini nimesikia eti ananiita bebi kwenye mitandao ya kijamii, siyo kweli kabisa.”
Batuli.
Batuli naye anasemaje? Huyu hapa: “Mh! Watu wananisema mengi sana, waache waseme, mimi naongea na Chifu kawaida tu, hata jana nilimfuata anisaidie kama wasanii wengine.”

URAFIKI WA WEMA,KAJALA CHALIKimenuka upyaaa! Wale mashostito wawili katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja ambao walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana, wanadaiwa kuvunja rasmi ushosti wao, Ijumaa limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki wa mastaa hao, hivi sasa hali ni tete huku sababu mbalimbali zikidaiwa kuwa chanzo cha yote.
WEMA KARUDI KWA SNURA?
Chanzo hicho kilidai kuwa kila mmoja kwa sasa amechukua hamsini zake huku Wema akidaiwa kurudi kwa shostito wake wa zamani, mamaa wa Majanga, Snura Mushi.
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa chanzo kikubwa ni kuwa mashosti hao walikutana katika saluni moja maarufu iliyopo Kinondoni, Dar ambapo Kajala alikuwa akitokea kwenye ‘shutingi’ ya filamu yake.
Ilidaiwa kuwa Kajala alifika saluni hapo akiendesha baiskeli iliyosababisha akaloa jasho sehemu kubwa ya mwili wake.

Ilisemekana kwamba Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini Kajala alimkwepa kwa sababu mwili wake ulikuwa na jasho jingi, jambo lililomfedhehesha Wema na kununa.
“Yaani baada ya Kajala kukwepa kukumbatiwa, Wema aliumia sana.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo hicho.


KISA CHA NYUMBANI
Hata hivyo, chanzo kingine kilicholonga na Ijumaa kilidai kwamba kuna siku Kei alikwenda nyumbani kwa Wema, Kijitonyama Dar kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia sinema).

DIAMOND ANANYIMA FURSA?
Ikadaiwa kuwa Kajala alipofika nyumbani hapo aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo amelala na Diamond na huwa hawaamshwi.

Chanzo hicho kilidai kwamba Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu na akamwambia asubiri ambapo msanii huyo alisubiri kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.
Pia chanzo hicho kilitiririka kwamba ushosti wa Wema na Kajala ulianza kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond mara baada ya kurudiana na Wema.

KIVIPI?
Chanzo hicho kilinyetisha madai kwamba eti Kajala hampendi Diamond kwani jamaa huyo amekuwa akitumia muda mwingi kuwa na Wema hivyo kubana fursa ya mashosti hao kujiachia.

“Unajua kabla Diamond hajarudiana na Wema, Kajala alikuwa anaweza kufika pale kwa Wema na kuingia hadi chumbani kwa shosti wake lakini sasa inashindikana kwa sababu anakuwepo Diamond,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Ndiyo maana Kajala ameona kama mbwai, mbwai tu! Kila mtu afe kivyake.”
HUYU HAPA KAJALA
Kwa upande wake Kajala alipopatikana, awali hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai kuwa hana tatizo na Wema na kwamba sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.
Alipotafutwa Wema na kusimuliwa mkasa mzima alisema kwa kifupi: “Mimi niko sawa, hakuna kitu na muda si mrefu watu watatuona tena pamoja,” alisema Wema.

SI MARA YA KWANZA
Wema na Kajala wamekuwa mashosti wa muda tangu Wema alipomlipia mwenzake faini ya Shilingi Mil. 13 mahakamani na kumuepusha kwenda jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kutibuana kwani mwaka jana waligombana lakini baadaye wakapatana.

RIDHIWANI AOMBA KULA KATA YA UBENAMgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete, akihutubia mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Visakazi, katika kata ya Ubena jana.
Wananchi wa kijiji cha Visakazi wakinyoosha mikono kuonyesha kumuuunga mkono Ridhiwani wakati wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlai akimpa ushauri Ridhiwani, kabla ua kumpa nafasi ya kuomba kura kwa wananchi wa kijiji cha Visakazi katika kaya hiyo jana.


Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Pwani, akimnadi Ridhiwani katika mkutano wa kampeni uliofanyika Visakazi katika kaya hiyo


Watoto wakijaribu kutumia simu ya mkononi kupata picha ya Ridhiwani wakati wakihutubia Kijiji cha Visakazi


Mzee Hemedi Ali akiongoza kutumbuiza ngoma ya kumlaki Ridhiwani katika kijiji cha Mwidu kata ya Ubena.


Ridhiwani akiwasalimia wapigakura alipokwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Mwidu.

Ridhiwani akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Ubena Zomozi alipokwenda kuhutubia mkutano wa kampeni.

Ridhiwani akionyesha furaha yake.

Sam wa Ukweli akitumbuiza Ubena Zomozi kwenye mkutano wa kampeni wa Ridhiwani.
 
Picha zote na (Bashir Nkoromo)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...