Sunday, July 13, 2014

DIAMOND ASHIRIKI UZINDUZI WA FILAMU YA THINK LIKE A MANMsanii Diamond Platnumz akihojiwa wakati wa uzinduzi wa filamu ya THINK LIKE A MEN.


Msanii Diamond,pamoja na wageni alioambatana nao akiwemo Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba wakati wakiwasili katika uzinduzi huo.


Terrence akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ambayo naye ameshiriki kuanza.


Diamond akisalimiana na baadhi ya mashabiki baada ya uzinduzi.

SHAKIRA, WYCLEF JEAN KUTUMBUIZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA USIKU


Shakira atapanda sejini kuimba wimbo wa "La la la (Brazil 2014)".

WANAMUZIKI Shakira na Wyclef Jean, usiku wa leo wataongoza burudani katika fainali za Kombe la Dunia 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.
Staa wa Hip Hop kutoka Haiti, Wyclef Jean naye atakuwepo kutoa kburudani usiku huu.

Mastaa wengine watakaoangusha burudani usiku wa leo ni pamoja na mpiga gitaa mahiri wa Mexico, Carlos Santana, Ivete Sangalo, Alexandre Pires wa Brazil na wanamuziki kutoka Shule ya Samba nchini Brazil.
Burudani hizo zitaanza saa 2:30 usiku ikiwa ni saa moja na nusu kabla ya mtanange wa fainali kuanza katika Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, Brazil.
Mpiga gitaa mahiri wa Mexico, Carlos Santana naye ndani.
Shakira ambaye anafanya shoo yake ya tatu katika Kombe la Dunia, atapanda stejini kuimba wimbo wake wa "La la la (Brazil 2014)" huku staa wa Hip Hop kutoka Haiti, Wyclef Jean na Alexandre Pires wakiimba wimbo "Dar um Jeito (We Will Find A Way)" wakati mashabiki wakiingia uwanjani.

Katika fainali za 2010, Afrika Kusini, Shakira aliimba wimbo wa "Waka Waka" huku 2006 nchini Ujerumani akiimba "Hips Don't Lie".
Shakira.
Kombe litakabidhiwa kwa mabingwa na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.

Kabla ya mechi, aliyekuwa beki wa Barcelona, Carles Puyol na modo wa Brazil, Gisele Bundchen wataliingiza kombe hilo uwanjani.

Ulinzi umeimarishwa katika fainali ya leo ambapo askari 26,000 watakuwa mitaani kudumisha ulinzi.

RAY C ACHEZEA KICHAPO CHA CHID BENZNa Musa Mateja
Uonevu! Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.
Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’.

TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.
Mwanaisha aliyepigwa na Chidi Benz hapo awali.

CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C Changanyikeni.

UNGA WATAJWA
Sosi wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C, wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.
KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.
“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.
RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio kwa kipigo kikali walichopokea.
RAY C AVUJA DAMU
“Ray C aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.
RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.

“Alinipiga vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo ambalo lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu hadi kuja kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye nilitoka naye ofisini kwangu.

“Ujue jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na Mariam, sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.

“Huko nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada ya kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za kuondoa sumu.

“Tumeendelea kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna baadhi ya kazi nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu. Pia alishawahi kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa alikataa na kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai mimi ndiyo namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.

“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”

SOO LIPO POLISI
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.

Juhudi za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi anaweza kutupigia.

CHID BENZ NI TATIZO?
Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.

Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.

Thursday, July 3, 2014

DIAMOND AENDELEZA MAKAMUZI MAREKANI SASA AJIACHIA NA MBWA

Msanii wa Bongo Fleva nchini Diamond, juzikati alinaswa kwenye moja ya viwanja nchini Marekani akiwa ameshikilia mbwa aliyekuwa na mmoja wa marafiki zake,wakati akiwa katika moja ya mizunguko na kujirusha kabla hajaanza safari ya kurudi Bongo.

Wednesday, July 2, 2014

ANGALIA RAHA ALIZOPATA DIAMOND AKIWA MAREKANI KWENYE TUZO ZA BETDiamond Platnumz akipita kwenye Red Carpet ya BET mbele ya mapaparazi zaidi ya 200. Mwanamuziki huyu alionekana kuwavutia watu wengi na suti yake iliyokuwa imemkaa kisawasawa ambayo Waingereza wanasema "Well Tailored Suit" By Designer Sheria Ngowi .

Mapaparazi zaidi ya 200 walichukua every step and moments za Red Carpet wakati Diamond akipita.

Mwana Muziki Ne-Yo alimwita Diamond wakati akipita na kumwambia 'congratulation' jambo ambalo lilitushangaza kuona kumbe hata wanamuziki wa Marekani wamefuatilia sana habari za wanamuziki waliokuwa nominated kutoka mataifa ya Afrika.

Mwanamuziki Nelly alitushangaza pale alipomvuta koti Diamond kwa nyuma na kumwita kwa jina, tulishangaa sana kuona kumbe wanamuziki wa Marekani nao wanafuatilia habari za African Nominees.

Picha iliyotamba kwenye Blogs za Marekani jana -Diamond katika pozi la Kisheria Ngowi.

Hap Diamond aligeuka nakukuta aliyemvuta koti ni Nelly ambaye alimwambia congratulations.

Ndani kwenye award show Diamond na USA Manager wake DMK wakipata ukodaki.

Behind The Scene Diamond akiwa na Super Designer aliyedesign suti yake, Sheria Ngowi.

Picha hii ilipigwa kutoka angani vile.

Diamond akiwa na USA Tour Manager wake DMK akifanyiwa wakati akifanyiwa mahojiano kwenye Red
Behind the scene Diamond akihojiwa na Factory 78 ya UK.

Behind the Scene Diamond katika picha ya pamoja na DMK ambaye ndiye USA Tour Manager wake.

Diamond akihojiwa na Karrueche Tran Kwenye Red Carpet (Karrueche ni Girlfriend wa Chris Brown),

Faith Evans ambaye ni Mke wa Marehemu BIG alipata nafasi yakupiga picha na Diamond.

Camrea yetu ilimpata Platnumz katika pozi hili.

Diamond akihojiwa na XXL Magazine kwenye Red Carpet pembeni yake ni USA Manager DMK.

Mtangazaji wa Fox Entertainment akimuhoji Diamond kwenye Red Carpet.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...