Sunday, May 31, 2015

DUNIA IMEKWISHA! WANAFUNZI DAR WAFANYA MAPENZI NA MBWA

NI kweli kabisa dunia imekwisha! Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar lililo chini ya Mchungaji Benson Shirima limegeuzwa danguro la kufanyia ‘usodoma’ kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Benaco waliotoroka majumbani mwao na kukacha masomo wakiwa ndani ya Kanisa la Maombezi la Ebenezer Deliverance la Mbezi ya Salasala jijini Dar.
WAZAZI, WASAMARIA WEMA
Kufuatia kushamiri kwa vitendo hivyo kwenye kanisa hilo, wazazi wa wanafunzi hao na wasamaria wema walikwenda kutoa taarifa kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kilimahewa, Kata ya Wazo, Mbezi Salasala na kuweka bayana kila kitu.
Wanafunzi hao wakiwa katika katika pozi baada ya kunaswa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.
KISA CHA KUTOA TAARIFA
Awali ilidaiwa kuwa, baadhi ya wanafunzi kwenye eneo hilo walikuwa wakisakwa na wazazi wao kwani waliondoka majumbani wiki kadhaa kwenda shuleni lakini hawakurudi na shuleni hawakuwepo.
“Hata walimu walisema wanafunzi hao hawafiki shuleni na majumbani hawapo. Ndiyo tuliposikia kuna kanisa limefanywa geto tukaamua kwenda serikalini kutoa taarifa ili uongozi wa serikali ujipange tukavamie,” alisema mtu mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Godoro ambalo watoto hao walikua wakilitumia.
UAMUZI WA SERIKALI YA MTAA
Maelezo ni kwamba, baada ya taarifa hiyo kufikishwa ofisini hapo, wajumbe wa ofisi hiyo na vijana wa ulinzi shirikishi wakiongozwa na mwenyekiti wa ofisi hiyo, Kulthum Juma walikwenda kulivamia geto hilo kwa lengo la kulisambaratisha.

KALIO LA MASOGANGE LALETA AJALI!

Makubwa! Lile kalio la haja la muuza nyago maarufu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Agness Gerald ‘Masogange’ limesababisha ajali kati ya bodaboda na Bajaj maeneo ya Sinza-Mori baada ya mrembo huyo kushuka kwenye gari akielekea saluni.
Agness Gerald ‘Masogange’ akiwa katika pozi.
Shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa bodaboda ilikuwa ikitokea upande wa Baa ya Meeda na Bajaj ilikuwa ikitokea upande mwingine ambapo muendesha bodaboda alitumia muda mwingi akimtazama Masogange aliyekuwa akikatiza huku akilitingisha wowowo ndipo jamaa huyo akasababisha ajali.
Agness Gerald ‘Masogange’ akionyesha jinsi alivyoumbika.
“Yaani aliposhuka Masogange tu kwenye gari yule mwendesha bodaboda hakuwa anaangalia mbele kabisa wakati Bajaj ilikuwa ikija kwa kasi hivyo akashindwa kuikwepa akaivaa na kumrusha dereva wa bodaboda upande mwingine kwa kishindo,” alisema shuhuda.
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa baada ya ajali hiyo kutokea, watu walikusanyika kitendo ambacho hata Masogange kilimshtua na kumfanya asimame kuangali tukio hilo.
Hata hivyo, shuhuda huyo alisema madereva hao walielewana na kuyamaliza palepale.
Baada ya gazeti hili kupata ‘ubuyu’ huo, lilimtafuta Masogange ambapo alikiri kutokea kwa ajali hiyo lakini mwanzo hakujua kama yeye alikuwa chanzo cha ajali hiyo.
“Unajua mimi nilivyosikia kishindo na watu wakipiga makelele sikujua kama  nilikuwa chanzo hadi niliposikia watu wanaanza kunong’ona maana hata mimi nilikuwa nashangaa na kujikuta nikicheka tu kwani sikujua wowowo langu lilisababisha shida,” alisema.ge.

Saturday, May 30, 2015

VIDEO MPYA: DIAMOND PLATNUMZ FT MR FLAVOUR - NANA

CHIKOKA ANASWA NA ‘KIBURUDISHO’

 
Msanii wa filamu category ya ‘siriaz komedi’, Juma Chikoka ‘Chopa’ akiwa na dada huyo.
Brighton Masalu MSANII wa filamu category ya ‘siriaz komedi’, Juma Chikoka ‘Chopa’ amenaswa ‘laivu’ akiwa na mrembo huku akionesha hali ya kutojiamini na kutoa tafsiri hasi miongoni mwa baadhi ya watu.
Mwanahabari wetu alimnasa msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Jengo la Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar,  kulikokuwa na sherehe za utoaji Tuzo za TAFA huku akimchimba mkwara mwandishi wetu akimtaka kusitisha zoezi la ‘kuwafotoa’ picha.
Awali, mwandishi wetu alimshuhudia Chikoka akiingia ukumbini humo na kuketi mkao wa ‘ kusikiliza misa’ kabla mrembo huyo hajatinga ndani na kumfanya msanii huyo asahau ghafla maana ya msamiati utulivu jambo lililowafanya baadhi ya watu kugeuza shingo mara kwa mara kuwatazama.“Oyaa, achana na mambo ya picha bwana hebu tupe uhuru wa kufurahia kilichotuleta hapa,” alisema Chikoka.

WEMA, IDRIS NUSU WAZICHAPE

Musa mateja MALKIA anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa kimapenzi ukitajwa.
Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar ambapo kwa pamoja walikuwa wamehudhuria sherehe ya utoaji Tuzo za Watu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tafrani ya wawili hao kutaka kukunjana ilitokea baada ya kumalizika kwa shuguli hiyo ambapo Idris alimpora Wema tuzo yake aliyoshinda na kwenda nayo kwenye gari lake.
Ugomvi huo ulipamba moto na kusababisha watu waliokuwa wakiwashuhudia kutaharuki ambapo Wema alikwenda kwenye gari lake lililokuwa likiendeshwa na Petit Man lakini Idris alimfuata akionekana kumuonea wivu na kumtaka apande gari lake waondoka jambo ambalo Wema alilitolea nje na kumfungia kioo.
Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15, Idris Sultan.
Baada ya kuona Wema amemtolea nje, Idris alikwenda kwenye gari lake na kuliegesha mbele ya gari la Wema ‘kum-block’ ili asiondoke ambapo alishuka na kumwambia Petit Man ahakikishe anamfuata kwa nyuma jambo ambalo Petit Man alishindwa kulitekeleza baada ya Wema kukataa.

WANATUPIA PAMBA F’LANI AMAZING

Msanii wa Bongo Fleva, Juma Musa 'Jux'.
Lucy Mgina,Dar es Salaam
UTANASHATI ni jambo kubwa sana kwa wasanii na watu wa kawaida. Mara nyingi utanashati humtambulisha muhusika namna anavyojiweka kuanzia nyumbani hadi katika mwili wake.Hapa Tanzania kuna wasanii kibao ambao wamekuwa wakijitahidi kujiweka fresh kwa uvaaji wao na hilo limewafanya kujiongezea umaarufu zaidi na sifa kujaa kwao.

Msanii wa Bongo Fleva, Gerry wa Rhymes.
Mara nyingi imekuwa ikichukuliwa kuwa watu wenye mkwanja ndiyo wanatakiwa kupendeza, lakini siyo hivyo! Unaweza kuwa na fedha nyingi na ukanunua kila aina ya nguo unayotaka lakini kitu kidogo tu kikakuangusha ambacho ni kushindwa kupangilia rangi ya nguo au kutojua uvae nini kwa wakati gani.
Wasanii wengi wa Bongo Fleva ambao leo ndiyo nawazungumzia wamekuwa wakijitahidi kujiweka sawa, na hii ni kutokana na kuwa na mizunguko mingi ya ndani na nje ya nchi hasa katika shoo, hivyo hupata fursa zaidi za kujifunza huko.
Sasa wafuatao ni baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva ambao wanajua kupangilia mavazi yao na kufanya waonekane ng’aring’ari muda wote wanapokuwa mbele ya jamii.

Jux
Juma Mussa maarufu kama Jux, ndiye msanii anayeongoza kwenye utupiaji wa nguo zenye brand kali za aina mbalimbali na huwa zinampendeza. Wapo wengi ambao wanavaa vizuri lakini Jux amekuwa akiwavutia wengi kila anapoonekana kutokana na kutupia vyema mavazi yake.

Anafanya muziki wa R&B na amekuwa akifananishwa zaidi na msanii wa Marekani, Trey Songz katika uimbaji. Licha ya kuwa hajaoa (anatajwa kutoka na msanii Vanessa Mdee) lakini linapokuja suala la mavazi jamaa ni msafi na anajua kupangilia hiyo yote inasababishwa na yeye mwenyewe.
Kamikaze ‘Cyril’
Anafahamika zaidi kwa jina la Cyril ambapo alilazimika kulibadili na kujiita Kamikaze, ni msanii ambaye pengine katika orodha hii anaweza kuwa hafahamiki sana lakini jamaa anajua kutupia.Staa huyu mavazi yake mara nyingi anakuwa akipendelea kupiga fulana za kubana na ‘jeans’. Sasa hivi Kamikaze anayefanya muziki wa Bongo Fleva anakimbiza na Kibao cha Nikikuona.

Izzo Business.
Izzo Business
Ukimtaja kwa jina la Emmanuel Simwinga utapata tabu kumtambulisha kwa mashabiki wa Muziki wa Hip Hop lakini ukimtaja kwa jina lake la kisanaa la Izzo Business utakuwa umepatia. Jamaa pia hufahamika kama Mr Mbeya City, huyu yupo mstari wa mbele kulitangaza jina la mkoa huo ambako ndiko alikozaliwa. Mavazi yake mara nyingi huwa ni suti au ‘jeans’, fulana na sweta jepesi juu yake, hapo utamtaka.

Thursday, May 28, 2015

KHADJA: NILIYEZAA NAYE, SITAKI HATA KUMSIKIA

LEO kupitia safu hii tunaye staa wa muziki wa kizazi kipya, Khadija Maige ‘Khadja’. Naye kama kawaida alibanwa na Mwandishi Wetu Shani Ramadhani kwa maswali 10 na bila hiyana alitoa ushirikiano katika kuyajibu.
Unajua aliulizwa nini na akajibu vipi? Ungana nami hapa chini.

Staa wa muziki wa kizazi kipya, Khadija Maige ‘Khadja’.
Ijumaa: Changamoto zipi unazozipata kupitia kazi yako ya muziki?
Khadja: Napata changamoto nyingi tu ikiwemo kutongozwa sana na wanaume. Pia baadhi wananikatisha tamaa wakidai eti siwezi kufika mbali wakati najua naweza.

Ijumaa: Wewe ni msanii sawa, lakini unajisikiaje unapovaa nguo za nusu utupu?
Khadja: Kwani tatizo liko wapi? Kama nikivaa hivyo najihisi niko huru, wewe kinakuuma nini?
Ijumaa: Wewe ni mtu wa aina gani, na je, ikitokea mtu amekuudhi ni kitu gani huwa unakifanya?
Khadja: Mimi ni mcheshi halafu napenda sana utani lakini kuna muda huwa nakuwa na roho mbaya hasa mtu akinikosea.

Ijumaa: Inasemekana wewe ni chapombe ile mbaya na ukilewa unakuwa mkorofi sana, hili likoje?
Khadja: Ni kweli huwa nakunywa pombe ila huwa silewi sana. Huwezi kuamini nikinywa pombe nakuwa mpole.
Ijumaa: Unawezaje kumudu muziki huku ukiwa unalea?
Khadja: Ni ishu ya kujipanga tu, yupo dada ambaye huwa ananisaidia kumlea lakini muda mwingi nikiwa sina shoo, nakuwa na mwanangu.

Ijumaa: Uliwahi kutamani kujiua kwa sababu ya kitu fulani?
Khadja: Sijawahi ila huwa natamani kuua kwa maana unakuta mtu anakuudhi kupita maelezo wakati muda huo una ‘stress’ zako.

Ijumaa: Wasanii mnatajwa kuwa na tabia ya kupora mabwana wa wenzenu, ulishawahi kupora au kuporwa?
Khadja: Huwa nasikia tu kwamba wapo mastaa ambao zao ni kuchukua waume za watu lakini mimi sijawahi kuporwa wala kupora.

Ijumaa: Ni kitu gani kinakufurahisha katika maisha yako?
Khadja: Mtoto wangu ndiyo furaha yangu, kila ninapomuona huwa nafurahi sana.
Ijumaa: Una mpango wa kuingia kwenye ndoa na mwanaume uliyezaa naye?

Khadja: Sina mpango huo na sitaki hata kumsikia kwani alinioa, tukashindwanwa hivyo siwezi kurudiana naye.
Ijumaa: Wewe ni mrembo, unawezaje kukabiliana na wanaume wakware?
Khadja: Mimi ni mrembo ndiyo ila kitu ninachokifanya ni kutowapa nafasi watu wa aina hiyo.

JOKATE: ALI KIBA NI KILA KITU KWANGU

Na Musa Mateja
MREMBO mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja ukimya na kusema kuwa mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu katika mambo yake mengi ya kimaisha.

Mrembo mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza na Ijumaa Jokate alisema, watu wanaongea sana kuhusiana na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa ndiye kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na wasioelewa, ipo siku wataelewa.
Mwanamuziki Ali Kiba.
“Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.

MIMBA YA ZARI YAMPA MAMILIONI DIAMOND

Musa Mateja
Imebainika kuwa mimba ya mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ inamwingizia jamaa huyo mamilioni ya fedha, Ijumaa limebaini mchezo mzima.
KUMBE!
Mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Imeelezwa kwamba, katika kila shoo anayokwenda na mama kijacho huyo amekuwa akilamba dau kubwa kwani wengi wanahudhuria burudani inayotolewa na Diamond ili kumuona Zari akiwa na kibendi.Uchunguzi wetu ulibaini kwamba, ujauzito wa Zari kwa sasa unamuingizia mkwanja mrefu Diamond kufuatia kila shoo anayohitaji kwenda kufanya, mapromota wengi wamekuwa wakimtaka aende na Zari ili tu mashabiki wamshuhudie.
TUJIUNGE NA CHANZO
Katika uchunguzi wake, Ijumaa lilizungumza na vyanzo mbalimbali akiwemo mtu wa ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye alithibitisha kuwa ni kweli uwepo wa mimba ya Zari kwa sasa umeongeza mamilioni ya fedha kwa Diamond kupitia shoo ambazo amekuwa akihitajika na mapromota kwenda na Zari.
DIAMOND ASHTUKIA
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kuwa, Diamond ameshalishtukia jambo hilo kiasi kwamba kuna sehemu sasa analazimika kwenda na Zari kwa siri.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz akibusu mimba ya Zari.
ZARI AFICHWA MWANZA
Ilifahamika kwamba, kwenye Shoo ya Jembeka iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Mwanza, Diamond alikwenda na Zari kwa kificho kikubwa kiasi kwamba hata umati uliyojitokeza kumpokea uwanja wa ndege jijini humo hawakuweza kumuona kwa kuwa makubaliano yake na waandaaji hayakumhusu Zari.
“Alichokifanya Diamond ni kumficha hotelini kwa kuwa katika shoo hiyo mapromota walikuwa hawakuelewana naye kwenda na Zari kama ilivyo kwenye shoo nyingine anazofanya kwa sasa,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika na kuongeza:
“Ni kitu ambacho Watanzania wengi hawakijui lakini ukweli uko hivyo kwamba, Diamond kwa sasa anavunja mkwanja mara mbili anapokuwa na Zari.”
BEI MARA MBILI?
Ilidaiwa kwamba kama Diamond alikuwa anachukua Sh. milioni 25 kwa shoo za ndani, kwa sasa akiwa na Zari ni mara mbili yake kwa hiyo inakuwa si chini ya Sh. milioni 50.
SHOO ZA KUMWAGA ZA NJE
Chanzo hicho kilieleza kwamba kwa shoo za nje ndiyo usiseme na tayari ameshaingia mikataba ya fedha ndefu kwenye nchi mbalimbali akiwa na Zari zikiwemo, Afrika Kusini ‘Sauzi’, Nigeria, Ghana, Cameroon, Togo, Angola na nyingine kibao.
DIAMOND ABANWA, AFUNGUKA
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond na kumbana ili afunguke juu ya hilo ambapo alipopatikana alikiri kwamba ni kweli kwa sasa mapromota wengi wamekuwa wakimhitaji kwenye shoo akiwa na Zari.
Diamond alisema kuwa, jambo hilo ni zuri ila kila mmoja ana malipo yake kwa maana wakitaka aende naye bei inakuwa tofauti ukilinganisha anapokwenda mwenyewe au na timu yake ya Wasafi.
Diamond: Nikiwa naenda kwenye events (matukio) namuuliza kwanza promota kama atahitaji niende na Zari? Akinijibu ndiyo, gharama inaongezeka.Ijumaa: Kwa hiyo unamaanisha kwa sasa ukienda kwenye shoo bila Zari kuna bei yake na ukienda naye unatakiwa ulipwe bei tofauti?
Diamond: Naam, namaanisha kwamba nikienda na Zari, lazima kuwepo na gharama za uwepo wake.
Ijumaa: Ni jambo gani lililokufanya kushtukia hilo hadi unasema hivyo?
Diamond: Ujue sasa hivi imefikia hatua nikiposti kwenye peji yangu kwamba kuna shoo nitaenda na Zari, idadi ya watu inaongezeka hata kama sitaingia naye ukumbini.
Ijumaa: Zari anajisikiaje mimba yake kufanywa ya maonesho?
Diamond: Zari ni mtu wa hekaheka hivyo hana tatizo kwani usalama wake upo wa kutosha.

RAY, CHUCHU HANS WAONESHANA MAHABA HADHARANI!

Richard Bukos
MAHABA popote! Licha ya kudaiwa ‘wamemwagana’, wapenzi wawili ambao ni wasanii ndani ya Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wameoneshana mahaba mazito hadharani na kuwaziba midomo waliodhani hawawezi kuwa pamoja tena.
Wasanii ndani ya Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans wakionyeshana mahaba.
Ishu hiyo ilinaswa hivi karibuni na ‘kasuku’ wetu maeneo ya Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za utoaji wa tuzo za filamu (TAFA) na kuwafanya watu wengi kushangaa huku wakionekana kuteta kwa nyakati tofauti.
“Mmh, hawa wamerudiana kwa mahaba mazito namna hiyo tena? Mbona tulisikia wameachana sasa naona wamegandana tena,” alisikika msanii mwingine (jina tunalo).
Hata hivyo, mwandishi wetu alimfuata Ray na kumuuliza kuhusu minong’ono ya wao ‘kutemana’ ambapo alijibu;
 “Huyu ndiye mke wangu, hayo mengine achana nayo kabisa.”

ZENGWE MTOTO WA AUNT APIGWA ZENGWE!

Mtoto wa kike wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson aliyejifungua mwishoni mwa wiki iliyopita na kumpa jina la Cookie (keki ndogo lakini tamu) anaanza kung’aa kwenye vyombo vya habari baada ya baadhi ya watu kumpiga zengwe la madai kwamba eti hafanani na baba yake, Moses Iyobo ‘Moze’.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.
Huku ishu hiyo ikipingwa vikali na Aunt, washakunaku wa mambo ya watu waliozungumza na Amani  baada ya kumuona Cookie walidai kwamba mtoto ni mweupe wakati Moze ni mweusi ‘tiii’.Zengwe hilo lilianza kusambaa miongoni mwa mashosti waliokwenda kumpa hongera Aunt nyumbani kwake, Kinondoni, Dar, saa chache baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.
“Unajua tangu akiwa mjamzito kuna watu walikuwa na shauku ya kumuona mtoto kujua kama kweli ni wa Moze maana mwanzoni hakuna aliyeamini kama mimba ni ya Moze ‘so’ hao ndiyo wameanza chokochoko,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutochorwa gazetini.
 

Aunt Ezekiel Grayson akiwa na mwanaye.
Baada ya kunasa zengwe hilo, Amani lilimtafuta Aunt ili azungumzie ishu hiyo ambapo alifunguka;
Amani: Kuna zengwe juu ya baba wa mtoto wako, kwani mwanao anaitwa nani?
Aunt: Anaitwa Cookie Lapri-Center.

KAJALA AMWANGUKIA WEMA

KWELI dhamira inauma! Staa mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ameamua kukifungua kinywa chake na kusema kuwa anamwomba msamaha zilipendwa wake katika urafiki, Wema Isaac Sepetu kwa mabaya yote aliyomtendea, Amani linakupa zaidi.
Staa mkali wa sinema za Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumza katika mahojiano maalum na  mapaparazi wetu mapema wiki hii jijini Dar, Kajala alisema hata kama kuna chuki ya ukubwa kwa kiasi gani baina yao lakini Wema atabaki kuwa mtu muhimu sana katika maisha yake mpaka atakapoaga dunia!
“Najua mimi na Wema hatuko sawasawa. Lakini namwomba anisamehe sana. Naumia kila siku. Yeye ni mtu muhimu sana katika maisha yangu. Atambue hilo,” alisema Kajala.

YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN LEO


KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Wasanii wa yamoto band.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani 'Isha Mashauzi'.
Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.

Tuesday, May 26, 2015

RAY ABANWA MTOTO WA JOHARI, AFUNGUKA!

Brighton Masalu na Musa Mateja
SIKU chache baada ya kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi kuwa staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba na kuzaa kwa siri huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray kufunguka kuwa hahusiki kwa lolote, Risasi Mchanganyiko ‘limemzingira’.
Staa wa filamu Bongo,Vincent Kigosi ‘Ray’.
Hivi karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa sasa na Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA ambapo aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...
kuzungumza mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na kwamba watu wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku akimtaja mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa maisha.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli zake.
Staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na mwanaye.
Huku akiwa amemganda Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray alikwenda mbele zaidi na kusema ni jambo la heri kujiweka mbali na watu wanaotafuta umaarufu kupitia migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa waandishi wetu na yeye kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita ‘hakuwa na mudi ya mazungumzo zaidi’.
“Achaneni na hayo mambo, sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na sipendi kabisa kuzushiwa mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa minong’ono na badala yake wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa mwanamke wa maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa natembea naye kila mahali ili kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni wapenzi wangu,” alisema Ray huku akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya ‘nadhani mmenielewa sasa’ na kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba wake.
Hivi karibuni Johari alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miezi saba ambaye alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.

DIAMOND ATELEKEZA WATOTO SHULE!

KABANG! Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.
Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili juzi kwamba, baada ya Diamond kuwashindanisha watoto hao, Hillary na Hamis (katika picha no. 1 na 2 zilizoko ukurasa wa mbele walipelekwa shule na Diamond) katika shindano la Ngololo lililonyika Januari, mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na kushinda aliamua kuwapeleka katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada kila mwaka lakini kuanzia hapo aliwatelekeza.
“Jamani Diamond kila kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale watoto ambao aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu,  mwezi uliopita walitimuliwa na sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa watoto walitolewa kwenye shule za kawaida na yeye ndiyo akawapeleka kule,” kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema watoto wao walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond hakuwahi kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu watoto wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la kueleweka.

Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa na wanafunzi hao pamoja na mwalimu wao.
“Tulipewa namba za simu za mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini kila tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri, mara yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye nini.
“Tunaomba sana jamani, mtusaidie na nyie waandishi maana watoto wanapitwa na masomo na isitoshe kabla ya hapo walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,” alisema mzazi huyo.

BEYONCE, JAY Z MAHABA KAMA WAMEANZA JANA!


Rapa Jay Z na mkewe Beyonce wakijiachia kwenye viunga vya jiji la Florence nchini Italia.
Florence, Italia
PENZI ni kikohozi kulificha huwezi! Ndivyo ambavyo wanaonyesha wapenzi wawili maarufu duniani, rapa Jay Z na mwimbaji Beyonce ambao hivi sasa wapo nchini Italia wakila raha na unaambiwa wamekuwa wakigandana na kuonyeshana mahaba hadharani utadhani walianza mapenzi yao jana kwa jinsi walivyoshibana.
Jay Z, 45, na Beyonce, 33, ambao kwa miezi kadhaa iliyopita walidaiwa wapo katika mgogoro wa ndoa, wameonyesha ndiyo kama mapenzi yao yameanza upya wakiwa wanakula bata katika Jiji la Florence.
Wawili hao ambao ni miongoni mwa wapenzi matajiri zaidi duniani, walionekana wakikatiza sehemu mbalimbali jijini humo huku wakionekana kuwa na nyuso za furaha.

MPENZI WA FACEBOOK AMNYONGA MKE WA MTU GESTI!

KWELI mchepuko siyo dili! Kauli hii imedhihirika kufuatia mwanadada, Ashura Maulid, mkazi wa Ilala jijini Dar, kukumbwa na mauti kwa madai ya kunyongwa ndani ya gesti na mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Charles ambaye inasemekana ni mpenzi waliyekutana kwenye mtandao wa kijamaii wa Facebook.
Marehemu Ashura Maulid enzi za uhai wake.
Tukio hilo lililojaa majonzi tele na kuacha maswali mengi, hasa kwa mume wa marehemu, Suleiman Othman, lilijiri  Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wageni (jina lipo) iliyopo kandokando ya barabara ya kutoka Sinza Afrikasana kwenda Kijitonyama kupitia Kituo cha Polisi cha ‘Mabatini’, Dar.

TASWIRA ZA AWALI ZA TAMASHA KUBWA LA BURUDANI 'JEMBEKA FESTIVAL 2015


Mmoja wa wasanii washindani wa Mkali Jembeka akionesha ufundi wake katika hip hop kwenye fainali ndani ya Tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL' lililozinduliwa Jumamosi ya tarehe 23/05/2015 uwanja wa CCM Kirmba jijini Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.  
Shengwe za wananchi kwa tamasha lililopigwa tangu saa 7 mpaka asubuhi siku iliyofuata na hapa ni mapema kabisa ngoma saa tisa huku burudani zikiwa tayari zimeshika kasi.
Ming'aro ya Mwanza wenyeji na wageni.
Mkali mwingine huyu hapa akionesha ufundi.
Dance la Jembeka wakali waliosisimua kwenye ushindani ndani ya Tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL' lililozinduliwa Jumamosi ya tarehe 23/05/2015 uwanja wa CCM Kirmba jijini Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.   
'Shikilia'
JJ Band walikisanukisha ile mbaaaayaa...
Mkali toka A town Dogo Janja ni mmoja kati ya wakali wa Bongo Fleva waliozuka kutoa burudani kwenye Tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL' lililozinduliwa Jumamosi ya tarehe 23/05/2015 uwanja wa CCM Kirmba jijini Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.  
Director Shahib wachaaaaaa......'Changamka' na 'Chemsha Ubongo'
'Mida ya night'
'Changamka'
Ze area at JEMBEKA FESTIVAL lililofanyika mwishoni mwa wikijijini Mwanza.
Mo  Music toka Mwanza.
Mensen Selector alikamua ile kisawasawa....
Kanyaboya ilibamba..
Toka kijiji cha Jembeka VIP Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula mwenye koti jekundu nyuma akiwa na wadau wa burudani akiwemo msanii Juma Nature.
Hisia....
Jembeka Red Carpet.
Pam D akiwa na shabiki wake.
Pam D (kushoto) akiwa na Baraka De Prince.
Rais wa Team Maua Classic 'Bob White Pamba' akihojiwa na mtangazaji wa 93.7 Jembe Fm mwanadada Jackline Shuma wa kipindi cha Hit Zone. 

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...