Na Musa Mateja
MREMBO
mchakarikaji Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja
ukimya na kusema kuwa mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu
katika mambo yake mengi ya kimaisha.
Akizungumza na Ijumaa Jokate alisema, watu wanaongea sana kuhusiana
na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa ndiye
kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na
wasioelewa, ipo siku wataelewa.“Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.
No comments:
Post a Comment