Friday, January 31, 2014

SHILOLE AANIKA UCHUNAJI BUZI WAKE

Shilole akiwa kwenye pozi

MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya na Filamu Bongo, Zuwena Mohamed 'Shilole',jana alianika wazi tabia yake ya uchunaji mabuzi alipokuwa kwenye moja ya mahojiano na watangazaji wa Kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, baada ya kuulizwa swali liloendana na jina la kibaochake kipya ambacho jana ndiyo ilikuwa siku rasmi akikiachia hewna kupitia stesheni za radio hiyo,baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la NACHUNA BUZI,mmoja ya watangazaji wa kipindi hicho alimuuliza ni kitugani kilichompelekea hadi kutunga wimbo wa namna hiyo na kuupa jina hilo,Shilole katika majibu yake alisema kuwa ameamua kukipa jina hilo kufuatia historia mbalimbali za maisha yake,hususani wimbo wake uliopita ambao aliupa jina la Nakomaa na jiji la Dar,sasa kudhihirisha kauli hiyo ameamua kuchuna mabuzi ili aweze kupata mkwanja wakutosha kulihimili jiji la Dar es Salaam na Igunga abaki kwenda kusalimia ndugu na jamaa tu.Baada ya manene hayo Shilole pia aliandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram:-
shilolekiunoASANTENI MASHABIKI WANGU WOTE KWA KUIPOKEA VEMA NYIMBO YANGU MPYA#CHUNABUZI# MUNGU AWABARIK# AMEEN

OMMY DIMPOZ AWEKA KWEUPE ZIARA YAKESOMA ratiba ya ziara za kimuziki za Ommydimpoz anazotarajia kuzifanya kuanzia,Friday 31-01-2014 pozkwapoz live in KAHAMA Saturday 01-02-2014 pozkwapoz live in GEITA Saturday 08-02-2014 pozkwapoz live in CALIFORNIA USA Saturday 15-02-2014 pozkwapoz live in LONDON UK Saturday 22-02-2014 pozkwapoz live in WASHINGTON DC Friday 28-02-2014 pozkwapoz live in GLASGOW SCOTLAND Saturday 01-03-2014 pozkwapoz live in MILTON KEYNES UK Nakumbuka maneno ya Bibi yangu Aliniambia "kwenye Maisha ukipata Nafasi Basi itumie inavyotakiwa" LOVE U ALL!!!#pkp#pozkwapoz#2014


WASTARA:NAPENDA SANA KUKUMBATIWA,KUKUMBATIA


Wastara Juma.
MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.

“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.”

MZEE GURUMO:MADEMU WANAJISOGEZA KWA DIAMONDMSANII mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Muhidini Gurumo ambaye kwa sasa amestaafu, amefungukia skendo ya kuwa na mademu wengi inayomuandama Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni maeneo ya Ilala jijini Dar, Mzee Gurumo alisema: “Diamond ana nidhamu sana ila vile anavyotamba jukwaani na kudatisha mashabiki hapo ndipo balaa linapokuja, watoto wa kike wenyewe wanaanza kujisogeza kwake.
“Pamoja na skendo za mademu zinazomuandama, siwezi kumshusha thamani, ana haki ya kujiopolea mwanamke yeyote anayempenda, yeye kama mwanaume rijali wakati mwingine ni vigumu kujizuia na vishawishi hivyo.”

ZITTO KABWE ADAIWA KUWAJIBU CHADEMA MIKOA 4


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

USHINDANI wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umefikia hatua mpya baada ya CCM kuibuka na mkakati wa kumtumia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kupambana na CHADEMA waziwazi.

Katika mkakati huo CCM imepanga kukodisha helikopta ya kumpeleka Zitto katika mikoa minne kwa gharama ya sh milioni 50 mara tu baada ya CHADEMA kuhitimisha Operesheni yao ya M4C Pamoja Daima.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vilivyo karibu na Zitto na CCM, yeye na chama hicho sasa wana adui mmoja – CHADEMA; na wameamua kujibu mapigo baada ya kuridhika kwamba kwa vyovyote Zitto amekwisha kupoteza uanachama wake katika CHADEMA.

Nia yao ni kumtumia Zitto kuleta mpasuko katika CHADEMA, na kufunika mjadala wa mgogoro wa CCM, kero za wananchi na mchakato wa Katiba mpya.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA – Naibu Katibu Mkuu Bara, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Baraza Kuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – anatarajia kutumia helikopta yenye uwezo wa kubeba watu wanne, ambayo inadaiwa kukodishwa na wapinzani wa CHADEMA.

Kwa mujibu wa habari hizo, lengo la ziara ya Zitto ni kujibu mapigo ya CHADEMA, hasa katika maeneo ambayo baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho wamepita na kuzungumzia hatima yake kisiasa, hasa walipojibu maswali ya wananchi kuhusu sakata lake kuvuliwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, na hatimaye Zitto kwenda mahakamani kuzuia chama kujadili uanachama wake.
Katika kesi ya msingi, Zitto aliyewahi kuwa maarufu akiwa kiongozi wa CHADEMA, anaomba arudishiwe nyadhifa zake zote, na apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ili aweze kukata rufaa Baraza Kuu.

Taarifa zinasema tayari chama kimempatia nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Zitto amekwisha kujiondoa kwenye chama hicho kwa kupeleka shauri mahakamani.

Taarifa za Zitto kuanza ziara mikoani zilianza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mikoa iliyotajwa ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam, ingawa maandalizi yanaendelea na kuna uwezekano wa kubadili baadhi ya mikoa kulingana na mkakati wao.

Kwa hadhi yake ya sasa, CHADEMA imeshasema haitahusika na mikutano yake, na wanachama wake hawatajihusisha nayo. Uratibu wa mikutano yake unafanywa na viongozi waandamizi wa CCM.

Baadhi yao walizungumza na gazeti hili kwa kujitapa kwamba hii ndiyo njia ya kuimaliza CHADEMA, lakini hawakutaka kutajwa majina gazetini.

Iwapo Zitto atakubali ufadhili huo wa CCM na kuendelea na mikutano yake, ni wazi atakuwa amekamilisha ushahidi wa kinachodaiwa na chama chake kwamba amekuwa akikisaliti kwa masilahi ya CCM.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa CCM walipoombwa maelezo juu ya urafiki wao na Zitto kiasi cha kumkosanisha na chama kilichomlea kisiasa, CHADEMA, walisema kwamba urafiki uliopo si wa Zitto na CCM, bali Zitto na Rais Jakaya Kikwete.

Gazeti hili linafahamu kwamba wakati fulani mwaka juzi Zitto alipobanwa na wabunge wenzake kuhusu tabia zake za kuwasaliti kwa Rais Kikwete, alisisitiza kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake binafsi, kwa hiyo wamwelewe.

Vilevile, wapo wanaohoji nia ya ziara hii wakati kwa muda mrefu amekuwa akikwepa kuambatana na viongozi wenzake katika ziara na operesheni nyingi za kichama.

Wanasema kwa kuwa operesheni ya sasa ya CHADEMA imepewa jina la M4C Pamoja Daima, kitendo cha CCM kuandaa ziara ya Zitto na kumkodishia helikopta, ni uthibitisho kuwa Zitto hayuko pamoja na CHADEMA tena.

Wameongeza pia kuwa kama hilo litafanyika, litakuwa limemwingiza Zitto katika orodha ya makada kadhaa wa upinzani waliotumikia CCM baada ya kufukuzwa au kunyimwa fursa za uongozi katika CHADEMA, kama Tambwe Hiza, Dk. Aman Walid Kabourou na Dk. Masumbuko Lamwai.

Alipotafutwa athibitishe kuhusu ziara hii na kama ni kweli inafadhiliwa na CCM, Zitto hakuweza kupatikana.

Mbowe kuwania tena uenyekiti

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa kamwe hatakiacha chama hicho katika uchanga wa harakati za kulikomboa taifa kama kiongozi wake wa juu.

Akihutubia katika mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima katika sehemu mbalimbali mkoani Morogoro jana, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa, bado atagombea nafasi ya uenyekiti kwa lengo la kuendeleza harakati za ukombozi wa pili wa taifa hili.

Bila kutaja jina, Mbowe alionya kuwa wenye fikra za kuachiwa chama hicho kikiwa katikati ya ukombozi huo hawatapata nafasi, kwa sababu hawana nia thabiti ya kukiendeleza, bali wana nia ya kukibomoa kwa kutumiwa na wapinzani wa CHADEMA.

“Makamanda, kumbukeni kuwa chama hiki na sisi viongozi wake tumepita katika majaribu makubwa na hata kukoswakoswa kuuawa. Mimi nimekoswakoswa kuuawa kwa bomu huko Arusha, lakini pia kuna watu wamepoteza maisha, wamefungwa jela, wengine wamekuwa vilema, halafu watu wengine wanatusaliti kwa kupewa visenti ili wakivuruge chama na wanataka tuwape chama. Huu ni uendawazimu,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema CCM imekuwa ikifanya jitihada za kuihujumu CHADEMA kwa mbinu mbalimbali, zikiwemo za kupandikiza migogoro, jambo ambalo limeshindwa kufanikiwa kwani Mungu ameweka mkono wake ili kisisambaratike.

“Harakati hizi tunazofanya za kuwakomboa Watanzania mjue tunahatarisha maisha yetu, tumejaribiwa kushawishiwa ndani na nje ya Bunge ili tuwe kondoo, tumekataa. CCM wamekuja na mbinu za kupandikiza migogoro wameshindwa na sasa wanaomba nife wakifikiri nikifa na CHADEMA itakufa. Nawaambia CHADEMA haifi kwa kuwa tumezalisha makamanda wengi, watakiendeleza,” aliongeza Mbowe.

Akielezea kwa mara ya kwanza kwa undani zaidi kuhusu mauaji ya Arusha, mwenyekiti huyo alisema wana ushahidi wa kutosha kwamba polisi walihusika na mauaji hayo na kuongeza kuwa waliohusika ni polisi wa kutoka mkoani Morogoro.

“Kwa mara ya kwanza niliseme hili, mauaji ya Arusha yaliyofanyika kwa kurusha bomu katika mkutano wa kampeni za CHADEMA, yalifanywa na polisi ambao walitoka mkoani Morogoro. Ndiyo maana tunaendelea kumwambia Rais Jakaya Kikwete aunde tume ya kimahakama ili kupata ukweli wa jambo hili,” alisema.

Kuhusu Katiba
Akizungumzia msimamo wa CHADEMA kuhusu muungano, Mbowe alisema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ya serikali tatu.

Alisema hata tafiti mbalimbali zilizofanyika, zikiwemo za wanasheria na wachumi zinaonyesha kuwa Muungano utaimalika zaidi chini ya muundo wa serikali tatu.

“Nawaonya Wana CCM wasijaribu kuingilia mjadala wa Bunge la Katiba na kama wanataka nchi ichimbike, basi walazimishe serikali mbili,” alisema Mbowe.

“Zipo tetesi za CCM kutaka kupitisha hoja zao kwa nguvu kutokana na idadi yao ndani ya wabunge zaidi ya 600, wakiwemo 356 wa Bunge la Tanzania Bara, 84 kutoka Zanzibar na 201 kutoka makundi mbalimbali watakaokwenda kwenye bunge hilo. Wasidanganyike kwamba wanaweza kutumia wingi wao kubadilisha maoni ya Watanzania kuhusu serikali tatu,” alisisitiza Mbowe.

Halima Mdee anguruma

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye yuko katika msafara wa mwenyekiti huyo, alisema vijana wengi wanaochipukia katika siasa kupitia chama hicho, wamelelewa na Mbowe, ambao leo wamekuwa chachu ya mabadiliko nchini.

“Ukweli ni kwamba kamanda huyu wa anga (Mbowe), ndiye ametulea vijana wengi nikiwemo mimi, tena wengine hatukuwa na ujasiri tulionao sasa, asiwadanganye mtu, hasa sisi vijana kwamba tuliingia CHADEMA na umaarufu, hawapo hao, tumelelewa na huyo kamanda,” alisisitiza huku akipigiwa makofi.

CHANZO NI TANZANIA DAIMA

UNDANI WA MSANII WA FILAMU KUJINYONGA GUEST TANGAMarehemu Victor Peter akiwa amepozi na mmoja wa marafiki zake siku chache kabla yakujinyonga katika Guest ya Safari Junior iliyopo katika mtaa wa Kisosora mjini Tanga

SAKATA la kujinyonga kwa msanii wa filamu Bongo, Victor Peter limegubikwa na matukio tofauti ya kustaajabisha ambayo marehemu aliyafanya siku kadhaa kabla hajapatwa na umauti, Ijumaa limefukunyua kila kitu.

Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Hamisi Koba, msanii huyo alijinyonga usiku wa Februari 27, mwaka huu mkoani Tanga ambapo marehemu alifika jijini humo kuigiza filamu yake iitwayo Our Family.

Hamisi alisema Victor aliwasili jijini humo akiwa na timu ya wasanii sita na kufikia kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Safari Junior iliyopo maeneo ya Kisosora ambapo punde walianza kushuti filamu hiyo ambayo yeye na Mzee Jengua ndiyo walikuwa wahusika wakuu.


“Mimi ndiye nilikuwa kama mwenyeji wake mkubwa hapa Tanga, alikuwa ni mpole na siku zote tulipokuwa kazini kwa ajili ya kushuti filamu hiyo aliniambia mambo mengi kuonesha amejipanga kuhakikisha anaifikisha mbali.

“Victor alitokea Mwanza, akaenda Dar ambapo alifika na kuandaa filamu yake ya kwanza aliyoiita Chozi ambayo tayari ilikuwa imekamilika na kuiuza kwenye Kampuni ya Kapiko ya jijini humo,” alisema Koba na kuongeza:

“Filamu hiyo ilikuwa bado haijatoka, akaamua kuja Tanga kuandaa filamu hiyo ya pili ambayo nayo ilikamilika juzi. Naumia sana ninapokumbuka mipango yake maana alikuwa ana ndoto za kufanya makubwa.“Siku ya Januari 27 tulipokuwa tunakamilisha filamu, kuna muda alikuwa anaonekana kama ana wenge hivi... alipomaliza kushuti sehemu yake tulienda benki, akachukua fedha na kuwalipa wasanii wote.”

Akiendelea kutiririka juu ya tukio hilo, Koba alisema marehemu alionesha kama alikiona kifo chake kabla kwani aliuliza mara mbilimbili kama kuna mtu anamdai ili amlipe.

“Wakati anatupatia fedha kila mara alikuwa anauliza kama kuna mtu anamdai hadi tuliingiwa wasiwasi na ingawa wengine walisema atakuwa amefurahia labda kumaliza muvi yake,” alisema.

Koba alizidi kueleza kuwa, marehemu akiwa na furaha ya kumaliza muvi hiyo, alikwenda chumbani kwake na kujifungia lakini alfajiri (Januari 28) walipomgongea mlango waligundua amejinyonga.


“Tulichungulia kupitia tundu la funguo tukaona kama ananing’inia ndipo tukaenda kwenye kituo cha Polisi cha Chumbageni na kuchukua askari ambao walishirikiana na mwenye gesti hiyo kuvunja
mlango na kumkuta kajinyonga, tukachukua mwili na kuupeleka kwenye Hospitali ya Bombo, mipango ya kuusafi risha mwili kwenda Kahama nyumbani kwao imeanza,” alisema Koba na kuongeza:

“Kwenye hiyo filamu yake, stori ilikuwa mzee Jengua kama baba wa Victor ambapo Mzee Jengua alikufa na baadaye Victor anakufa kiajabu, kifo kimempata kweli.”

Kuhusiana na kifo hicho, Koba alisema kilimuuma kwani alikilinganisha na kile kilichomtokea marehemu Steven Kanumba ambaye pia aliigiza filamu ya Power of Love ikionesha anakufa, akafa kikwelikweli.

Mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Bombo ulitarajiwa kusafi rishwa juzi kwenda nyumbani kwao Kahama kuzikwa.

!

Tuesday, January 28, 2014

MBUNGE CATHERINE MAGIGE AINGIAZWA KWENYE MKUMBO WA ZITTO KABWE


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Na Musa Mateja
KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika.

Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.

“Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.

“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”

Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.

“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).

“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”

Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi

Monday, January 27, 2014

BREAKING NEWS:MCD WA TWANGA AFARIKI DUNIA USIKU HUU

Mpiga Tumba wa Bendi ya Twanga Pepeta Soudi Saidi 'MCD' akiwa kwenye pozi enzi za uhai wake

TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mpiga tumba wa zamani wa bendi ya Twanga Pepeta Soud Saidi 'MCD',amefariki Dunia jioni ya leo nyumbani kwao Moshi ambako alikuwa akiuguzwa kwa muda mrefu baada ya kusumbuliwa na maladhi kwa muda mrefu,yaliyompelekea kuwa nje ya bendi hiyo zaidi ya miezi mitano hadi leo anafikwa na mauti yake.
Innalilah wainaillah raajuin

MAZIKO YA MCD WA TWANGA PEPETA KUFANYIKA KESHO MCHANA MOSHI


MCD akiwa katika pozi enzi za uhai wake

 
ALIYEKUWA mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed 'MCD' aliyefariki jana usiku, atazikwa kesho saa 7 mchana Moshi mjini.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Twanga, Luizer Mbutu mazishi ya MCD ilikuwa yafanyike leo saa 10 lakini familia ikakubali kusogeza mbele ili wafanyakazi wenzie pamoja na marafiki wa marehemu waweze kuwahi mazishi hayo.

Msafara wa wasanii wa Twanga, wawakilishi wa bendi zingine, wadau na marafiki, utaondoka Dar es Salaam leo saa 4 usiku kuelekea Moshi.

MCD aliyefariki sekunde chache baada ya kufikishwa hospitali ya KCMC atazikwa Kiislam, dini aliyoitumikia hadi kufa kwake baada ya kubadili dini mara kadhaa.

Mpiga tumba huyo, kiasi cha kama miaka 13 iliyopita alibadili dini kutoka Uislam na kuwa mkristo hiyo ni kufuatia ndoa yake na Renada mtoto wa Chang’ombe lakini walipoachana akarejea tena kwenye Uislam.

Japo katika miezi ya hivi karibuni kulikuwa na mashaka kuhusu dini yake, lakini MCD aliithibitishia familia yake pamoja na wafanyakazi wenzake kuwa yeye ni Muislam.
Katika hatua nyingine usiku wa kuamkia leo, viongozi wa Twanga Pepeta, wadau na wasanii wa bendi mbali mbali walikutana na kuchagua kamati itakayoratibu safari ya kuelekea Moshi pamoja na mambo mengine ya kusaidia taratibu za mazishi.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Omary Baraka (Mkurugenzi Msaidizi ASET), Hassan Rehani (Meneja ASET), Abdallah Dossi(Mwenyekiti Macamp ya ASET), Martin Sospeter (Meneja Mashujaa Musica), Tarsis Masela (Kiongozi Akudo Impact), Deo Mutta (Katibu wa Macamp ya ASET), Rehema Kiluvia (Mdau Twanga Pepeta) na Super Nyamwela (Kiongozi Mkuu Shoo Extra Bongo) na Luizer Mbutu (Kiongozi Mkuu Twanga Pepeta) ambaye ndiye mweka hazina wa kamati hiyo.

Luizer ameiambia kuwa leo kuanzia saa 6 mchana hadi muda wa kuelekea Moshi, wadau wote watakutana katika ukumbi wa Vijana Hostel Kinondoni kwenye ofisi mpya za Twanga Pepeta.
Kwa wote watakaotaka kuchangia msiba huo kwa njia ya simu za mkononi basi wanaombwa kutuma pesa zao kupitia simu zifuatazo ambazo zote ni za Luizer Mbutu: 0653 797976, 0762 46 00 90, 0787 090 090.

CHANZO SALUTI 5

DIAMOND ALIVYOJIACHIA NA KAMERA NAIROBI KENYA

Staa wa ngoma ya Number one Diamond akiwa nchini Kenya juzi,kwenye moja ya mihangaiko ya kufanikisha muziki wake kuupaisha anga za juu zaidi

SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME MAJUMBANI
SERIKALI YAPUNGUZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME
*Ni kwa wanavijiji wanaoishi jirani na bomba la gesi Mtwara - Dar

SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi linapita.

Hatua hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.

“Jana Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.

Alisema katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-. “Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.

Gharama hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema uzinduzi wa mradi huo wa umeme ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.

“Mpango wa kupeleka umeme nchi nzima ni wa miaka mitatu na katika sekta ya Nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme,” alisema Waziri Mkuu.

Akitoa taarifa juu ya mradi huo wa umeme wilayani Nanyumbu, Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, Eng. Mahende Mugaya alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 5.6/- na unatarajiwa kukamilika Aprili, mwaka huu.

Alisema kuzinduliwa kwa mradi huo kunafanya wilaya zote za mkoa wa Mtwara ziwe zimepata umeme wa kuanzia na kwamba kazi itaendelea kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ili kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kwenye mkoa huo.

“Chini ya mfuko wa REA tumetenga sh. bilioni 7.6 ili zitumike kusambaza umeme katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara ambao sasa hivi watumiaji wa umeme wamefikia 15,675 sawa na asilimia nne ya wakazi wote wa mkoa huu.”

Alisema katika mwaka 2012-2013 walipata wateja 2,609 tofauti na idadi ya zamani ya wateja 1,300 ambayo ilikuwa imezoeleka. Alisema hivi sasa wamepokea maombi kutoka kwa wateja 2,588 ambao tayari wamekwishalipia gharama za kuunganishiwa umeme.

Chini ya mradi wa umeme kupitia REA, jumla ya vijiji 54 katika wilaya za Tandahimba, Masasi na Newala vitanufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa Desemba 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2015.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU.
JUMATATU, JANUARI 27, 2014

KAMANDA WA POLISI IRINGA (OCD) APATA AJALIAskari waliokuwa wakielekea katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kata ya Nduli Iringa mjini wakitazama gari ambalo alikuwa akiendesha OCD Iringa lililopata ajali majira ya saa 10 jioni leo (jana) jumapili japo hakuna aliyepoteza maisha ktk ajali hiyo iliyotokea kona la Mgongo barabara ya Iringa-Dodoma


wasomi wa chuo kikuu cha Iringa wakitazama ajali hiyo ambayo dereva wake OCD Iringa alinusurika kifo na kuumia mkono wake kiasi.Picha na Francis Godwin-Iringa

WALIOIBUKA KWENYE PROMOSHENI YA AIRTEL MIMI NI BINGWA WAANZA SAFARI YA KWENDA OLD TRAFFORD


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi kabla ya kuanza safari yao ya kuelekea nchini Uingereza kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando akiwakabidhi tiketi za ndege baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel tayari kwa ajili ya safari yao ya kwenda kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando akiwa pamoja na baadhi ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi kabla ya kuanza safari yao ya kuelekea nchini Uingereza kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City itakayochezwa kesho kwenye uwanja wa Old Trafford.


WASHINDI wa tiketi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliondoka nchini kwa safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.
Wakisindikizwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, washindi na wenza wao waliowachagua watakuwa na nafasi ya kuangalia mechi baina ya Manchester United na Cardiff City moja kwa moja ‘live’ itakayochezwa Jumanne saa 12 jioni majira ya Afrika Mashariki.
Awamu ya kwanza inayowajumuisha Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao, pia watapata nafasi ya kufanya ziara katika uwanja wa Old Trafford na kuzungumza na wachezaji wa Manchester United.
Washindi hawa hawakusita kuelezea furaha yao na hamu ya kukutana na wachezaji maarufu wa kimataifa wa mpira wa miguu pamoja na hari ya kuwa sehemu ya mashabiki katika uwanja huo maarufu duniani wakati wa moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza inayoangaliwa zaidi duniani.
“Hii ni nafasi ambayo sikuwahi kuiota katika maisha yangu. Kutokana na hali yangu ya kiuchumi, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitasafiri kwenda Uingereza na hususani kuingia katika uwanja wa Old Trafford. Nina furaha sana. Naishukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii, ambayo pia imenisaidia kuonyesha upendo kwa mwenza wangu kwa kumpa nayeye nafasi ya kwenda Uingereza,” alisema Lyatuu.
Salma, ambaye ni mshindi kutoka Dar es Salaam alisema, “Hii ni kama ndoto ambayo imekuja kutokea kweli. Nilipotaarifiwa kuwa nimeshinda tiketi mbili kwenda Old Trafford, sikuamini hadi nilipokamata tiketi yangu mkononi. Nataka niwahakikishie wananchi na wateja wa Airtel kuwa promosheni hii ni ya kweli na inaweza kukupa fursa ambayo kamwe hukuwa ukihitarajia.”
Akidokeza kuhusiana na safari hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando, alisema kampuni hiyo ya simu itagharamia safari yote, chakula pamoja na gharama za malazi hadi washindi hao watakaporejeshwa makwao.
“Bado kuna safari nyingi zaidi zinakuja. Mpaka sasa, tunaandaa baadhi ya hati za kusafiria za washindi wengine waliojishindia tiketi za promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa kwenda Old Trafford na zikiwa tayari, wataondoka mapema. Promosheni bado inaendelea lakini muda umebaki mchache kabla ya kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa shilingi milioni 50. Wakati wa kushiriki ndo sasa.
“Mbali na tiketi, bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa kila siku na kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa droo. Kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kushinda zawadi hizi. Unachohitaji ni kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo,” alisema.
Bw. Mmbando alisema safari hiyo itachukua siku tano ikiwa ni pamoja na siku za safarini na washindi wanatarajiwa kurudi nchini ifikapo Alhamis ya tarehe 30 mwezi huu.
Washindi hao watakaoelekea Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa Kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa mkoani - Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam.

ANGALIA ZAWADI ALIZOLETEWA WEMA SEPETU NA DADDY AKEE


zawadi from my daddy akee.... da only good part of mtu akitoka safari is ZAWADI.....


zawadi from my daddy akee.... da only good part of mtu akitoka safari is ZAWADI.....haya ni maneno aliyoandika Wema Sepetu baada ya kupost picha hizo za pafyum kwenye peji yake ya Instagram

PENNY:DIAMOND AKILI ZAKE KAMA CHIZICHIZI VILE!


Stori: Imelda Mtema na Erick Evarist
MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa sifa ya aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni kama chizichizi lakini kwa undani zaidi ni mtu makini.
Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.
“Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali,” alisema Penny na kuongeza:
“Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani.”
Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.

Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana’, akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani.

NAIMA AMPIKU WEMA SEPETU KWA CLEMENT AJICHOLA TATU YA JINA LAKE

 

NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.
Naima Shaa.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).
“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.

NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.
WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.
Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.
UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
Baada ya kupata taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Naima ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.

Alipoulizwa kuhusu tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).

“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimandika jina Element na siyo Element (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.
WEMA ANAJUA CHOCHOTE?
Baada ya kuwasiliana na Wema kwa njia simu na kumuuliza kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.

Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.

“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.
NYUMA YA PAZIA
Uchunguzi wa gazeti ulibaini kuwa nyuma ya pazia la habari hii kuna mambo mengi ya namna CK na Naima walivyokutana.

“Ni Kinondoni pale Mwanamboka. Mke wa CK alikuwa na baa pale ambayo siku hizi imefungwa.
“Naima alikuwa ni mke wa mtoto wa Mwanamboka. Walikuwa wanakutana pale baa. Ndipo mambo yalikoanzia.

“Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK. Ona sasa wote wamekosa ndoa. Sinema inaendelea,” kilimalizia chanzo chetu.

Saturday, January 25, 2014

SHILOLE AOKELEWA NA MCHUNGAJI ...


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya na Bongo Movie Zuwena Mohamed 'Shilole',akiwa kwenye pozi na mchungaji anayemuingiza katika maongezi ya kilokole
STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa jukwaani akifanya shoo ya kidunia na kupewa darasa la wokovu.
Tukio hilo lililowagusa wengi, lilitokea juzikati katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar ambapo mchungaji huyo ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake, alifuatilia shoo ya Shilole kisha akamwita kumpa darasa la wokovu.
Akizungumzia tukio hilo kwa kinasa sauti cha Weekly Exlusive Star, Shilole aliweka plain kuwa, mchungaji huyo aliguswa na namna ambavyo watu wengi walikuwa wakifuatilia shoo yake, akaona anaweza kuwabadilisha wengi waliopotea kupitia wokovu. “Aisee ilikuwa noma, nilipoona ananiita nilishtuka kidogo. Mbaya zaidi aliniambia anataka tupige picha pamoja, ndipo alipoanza kunipa darasa la wokovu.

“Alinitaka nibadilike kimavazi, pia nisimsahau Mungu katika maisha yangu yote na alimalizia kwa kunitaka niende kanisani kwake ili ikwezekana nitumie uimbaji wangu kuwabadilisha wengi waweze kumtumaini Bwana,” alisema Shilole staa wa wimbo Nakomaa na Jiji.

Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, Shilole alionekana kuguswa na maneno ya mchungaji huyo na kusema yamemkumbusha suala la kumkumbuka Mungu kila wakati katika kazi za mikono yake.

Akasema kwa kuzingatia hilo, sehemu ya mapato yake atakuwa akiyatumia katika kutoa sadaka husan kwa watu wasiojiweza ili kutimiza amri ya Mungu. “Ni wakati wa kubadilika, huu muziki tunafanya upo na utaendelea kuwepo lakini jambo la muhimu sana ni kumuabudu Mungu katika siku zote za maisha yetu ya hapa duniani,” alisema Shilole.

PENNY ATANGAZA KUJIVUA GAMBA RASMI KWA DIAMOND


MTANGAZAJI na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila 'VJ Penny' amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
CHANZO BONGO5

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKAGUA RAMANI NZIMA YA MITAMBO YA GESI ITAKAPOFUNGWAPicha ya sura na muonekano wa kiwanda cha MEIS kitakapokamilioka. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO-Mtwara).

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na msafara wake wakiangalia eneo utakapochimbwa mtaro wa kupitishia bomba la gesi.

Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba kabla ya kuyalaza na kuyafukia chini kwenye mitaro.

Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa na Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuendelea na ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi na wafanyakazi wa ujenzi kiwanda cha MEIS faida zitzkazotokana na kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa gasi kijijini hapo kwa njia rahisi baada ya kuunganishwa kutoka bomba kuu la gasi ikiwemo ajira kwa wanachi na upatikanaji wa saruji kwa bei nafuu ili kuboresha makazi yao.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha MEIS kilichopo eneo la Machole Mkoani Lindi.
 


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi wanaojenga bomba la mradi wa gasi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi huo.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akieleza hatua iliyofikiwa katika ujennzi wa bomba la gasi linalojengwa kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kwa Waziri Mkuu na msafara wake. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Younqing.

Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akimsikiliza Waziri wa Nishati na Prof. Madini Sospeter Muhongo akizungumzia ujenzi wa bomba la gasi eneo la Bungu mkoa wa Pwani.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...