Thursday, April 30, 2015

MUVI MPYA YA PISHU KUINGIA SOKONI KESHO

MUVI mpya ya Pishu kutoka Kajala Intertaiment & Baby Black Productions itakuwa sokoni kesho usikose kujipatia nakala yako kwani ndani yake utakutana mastaa wakali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja, Hemedy Phd, Tausi, Senga na wengine kibao.
Kajala akiongea na mtandao huu amewaomba mashabiki wake na wapenzi wa filamu za Kibongo kutoikosa muvi hiyo itapatikana sehemu zote Tanzania kuanzia kesho.

DONDOO MUHIMU KUELEKEA MPAMBANO WA KIHISTORIA KATI YA MONEY NA PACMAN


Floyd Mayweather (kushoto) na Manny Pacquiao wakipozi na mkanda wa WBC jana wakati wa mkutano na wanahabari.
SIKU mbili tu zimebaki kuelekea mpambano wa kihistoria wa ngumi za kulipwa utakaowakutanisha mabondia Floyd Mayweather (Money) na Manny Pacquiao (Pacman) ndani ya Ukumbi wa MGM Grand jijini Las Vegas, Marekani.
Muonekano wa sasa wa Hoteli ya MGM Grand iliyopo jijini Las Vegas, Marekani.
Mpambano huo umekuwa gumzo kote duniani kwa sababu wapinzani hao wamekuwa wakitafutana kwa muda mrefu kabla ya kukubali kupanda ulingoni na kuzichapa Mei 2 mwaka huu ambapo kwa muda wa huku itakuwa alfajiri ya Mei 3.
Money na Pacman watakomba kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 589 za Kitanzania na iwapo Mayweather atashinda pambano hilo ataweka kibindoni dola za Kimarekani milioni 180 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 353 za Kitanzania ambayo ni asilimia 60 ya kiasi cha fedha kinachoshindaniwa.

ZIFUATAZO NI BAADHI YA DONDOO ZA MPAMBANO HUO:
MIKWANJA
$300 milioni - Kiasi cha mkwanja uliotengwa kwa ajili ya pambano hilo ambapo asilimia 60 itakwenda kwa Mayweather huku asilimia 40 ikikombwa na Pacquiao (Pacman)
$321.43 - Kiasi alichotumia Mayweather kwa upande wa vyakula wiki kadhaa akijiandaa kwa pambano hilo.
$2 - Kiasi cha fedha alizokuwa akilipwa Pacquiao kwa kila pambano wakati wa ukuaji wake huko Ufilipino
Mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg waliowekeana $250,000 kwa ajili ya mpambano huo.
$250,000 - Kiasi kilichowekwa kubashiri mpambano huo kati ya mwanamuziki Diddy na Mark Wahlberg
$600 milioni - Jumla ya kiasi cha fedha atakachokuwa ametengeneza Mayweather kutokana na ubondia baada ya pambano lake na Pacquiao
$150 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia televisheni zitakazokuwa zimefungwa katika hoteli ya MGM
£19.95 - Gharama za kuangalia pambano hilo kupitia Kituo cha Sky Sports huko Uingereza
$99.95 - Gharama ambazo watalipa mashabiki waliopo Amerika kuangalia pambano hilo kupitia HBO au Showtime
$74 milioni - Mapato yanayotarajiwa kupatikana kutokana na tiketi zilizopangiwa kiwango kati ya $1,500 na $10,000
$5.6 milioni - Kiasi kilicholipwa na Tecate kudhamini pambano hilo.
$10,000 - Malipo atakayolipwa refa wa mpambano huo, Kenny Bayless
Kenyy Bayless akiongoza mpambano kati ya Mayweather (kulia) na Maidana Septemba 2014.
WAPIGANAJI
47 - Idadi ya mapambano ya kimataifa na ushindi ambao ameupata bondia Mayweather
55.3% - Asilimia za ushindi wa Mayweather kwa knockout (KO)
62 - Idadi ya mapambano ya kimataifa aliyopigana Pacquiao
66.6% - Asilimia za ushindi wa Pacquiao kwa knockout (KO)
39 - Wastani wa makonde aliyotupa Mayweather kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
66 - Wastani wa makonde aliyotupa Pacquiao kwa kila raundi tangu alipoanza mapambano ya kimataifa.
74 - Jumla ya umri wa mabondia hao (Mayweather ana umri wa miaka 38 huku Pacquiao akiwa na miaka 36)
Milioni 5.8 - Idadi ya wafuasi wa Mayweather katika mtandao wa Kijamii wa Twitter; Pacquiao ana wafuasi milioni 1.8
309 - Idadi ya maili ambazo Pacquiao alisafiri kwa basi lake la kifahari kutoka Los Angeles kwenda Las Vegas kwa ajili ya mpambano huo.
Manny akiwa kwenye basi lake la kifahari wakati akielekea Las Vegas akitokea Los Angeles alipokuwa ameweka kambi.
MPAMBANO
36 - Idadi ya dakika ambazo kila bondia atatumia kwenye ulingo iwapo pambano litachukua muda wote uliopangwa.
5 - Idadi ya miaka tangu pambano hili la kihistoria lianze kujadiliwa kwa undani.
Wafanyakazi wa MGM Grand wakiandaa mabango kwa ajili ya mpambano huo.
UKUMBI
16,500 - Idadi ya viti vya wageni wanaoruhisiwa kuingia katika Ukumbi wa MGM Grand wakati wa pambano hilo
9,000 - Idadi ya watu walioajiriwa katika Ukumbi wa MGM Grand
100,000 - Idadi ya watu wanaotarajiwa kuwepo katika hoteli ya MGM Grand kati ya Ijumaa na Jumamosi
7,000 - Idadi ya vyumba vilivyopo katika hoteli ya MGM Grand

Wednesday, April 29, 2015

SHOO YA ZARI ALL WHITE PARTY YANUKIA, DIAMOND AJIPINDA KUHAKIKI TIKETI


STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' jana ametupia picha hii mitandaoni akihakiki tiketi kwa ajili ya shoo ya mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' ya ZARI ALL WHITE PARTY itakayofanyika Ijumaa ya Mei 1, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
Staa huyo aliisindikiza picha hiyo kwa maneno haya:
"Sio kwa kiingilio hiki cha kuanzia Elf 50 hadi Milioni 3 eti nikajifanya naleta Uboss ... Mzigo Nausimamia mwenyeweee!!! Kushoto Manager @salaam_sk katikati nna @juju_utamu huku @queendarleen4real halaf kwambaaaaaali Mtoto katulia zake Anachat chat!... HAYA WALE WA ELFU HAMSINI NA WA LAKI KESHO NTAWATAJIA VITUO ZITAPOPATIKANA TICKET!!! #ZARIALLWHITEPARTY Friday May 1st 2015 Mlimani City Dar!!"
Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika, Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014.

FAMILIA:TUNASHAKA NA MIMBA YA ZARI

Musa Mateja
SHAKA! Familia ya ‘President’ wa Kruu ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imeamua kuweka kikao kummbana staa huyo aweke wazi kama ni kweli ana uhakika mimba aliyonayo mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari’ ni ya kwake au magumashi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Diamond Plutnum akibusu tumbo la mpenzi wake Zari.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku  hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli.
Diamond akiwa katika pozi na mpenzi wake Zari.
“Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari.
“Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho
 WALITAKA ATOE MSIMAMO
“Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika mitandao na vyombo vya habari,’’ kilisema chanzo hicho.
SABABU ZAZIDI KUANIKWA
Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga.
“Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi, waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika,” kilisema chanzo hicho.

Tuesday, April 28, 2015

Kuhusu mkataba wa Ben Pol na kampuni ya Panamusiq Ltd

ben

Msanii wa rnb Ben Pol maetia wino kwenye mkataba wa usimamizi na kampuni ya Panamusiq Ltd.
Mkataba huu utasimamia kazi zote za Ben Pol na kufanikisha ndoto zake za kuwa msanii wa kimataifa. Panamusiq ni kampuni iliyosimamia kazi za Vanessa Mdee kama ‘Nobody But Me’.
” The new partnership aims at developing Ben Pol into a sustainable global brand and consolidating his fame in Tanzania and across Africa. We expect to realize this plan through the production of great music, highly professional services and the co-operations with global brands and international music industry players.”

DIAMOND, ZARI NDIO HABARI YA MJINI


 
Diamond Platinums akiwa na Mpenzi wake Zari mara tu baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wakitokea Zanzibar ambao Diamond Alifanya Show Bab kubwa na Kuacha Historia katika Maeneo yote ya Zanzibar.Wawili hao wamewasili Dar tayari kwa Maandalizi ya Mwisho ya Show Kubwa ya Zari Ijulikanayo Kama White Party Itakayofanyika Mwishoni Mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City.

NHIF YAZINDUA AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA UHAMASISHAJI MFUKO WA AFYA

1 Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.
11Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi wilaya ni Kilwa. 12Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF.

Monday, April 27, 2015

MASTAA WANAOONGOZA KUTUKANA\KUTUKANWA MTANDAONI

Imekuwa ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama. Hata hivyo, maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo.
Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii.
Miongoni mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni kutoa maneno machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Katika makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana mitandaoni lakini pia wale ambao wanaongoza kwa kutukanwa katika siku za hivi karibuni.
Wastara Juma
Huyu Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha watu.

CHOCKY, NYAMWELA WAREJEA ‘TWANGA’ KWA MBWEMBWE, CHEREKO


Ali Chocky (katikati) akiwa na waimbaji wenzake, Luiza Mbutu (kulia), na Kalala Junior baada ya kutambulishwa.
Wanamuziki wa ‘Twanga’ wakiongozwa na Kalala Junior (kushoto) wakiwa na begi ambalo ndani yake alikuwemo mnenguaji Super Nyamwela kama moja ya staili ya kutambulishwa.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakifungua begi hilo tayari kwa utambulisho wa mnenguaji mwenzao, Super Nyamwela.

USAILI TMT 2015 ARUSHA MEI 1-2, 2015 TRIPPLE A

Joh Makini Nusu Nusu official music video

VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) WAANZA KUGAWANA NCHI YA TANZANIA

 https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/04/ukwaaa.jpg
Viongozi wa Ukawa

Dar/Mikoani.
Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano ya hadhara na mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa ushindi.


Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.
Chadema kilianza ziara zake mikoani wiki zilizopita baada ya kuzindua mkakati wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka kambi mkoani Kigoma kwa kile ilichokiita kuimarisha majimbo ya kimkakati.

Sanjari na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia katika moja ya ngome zake, mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya kiushindi, kinahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.

Jitihada za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa ni majuma kadhaa tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.

ACT - Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kilihitimisha ziara yake ya kimkakati katika mikoa tisa inayoonekana kuwa ngome ya CCM, wiki iliyopita wilayani Bariadi, Shinyanga na kuvuna wanachama zaidi 6,000 katika mikoa hiyo.

NCCR-Mageuzi ipo Kigoma
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema jana kuwa Ukawa ina mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya kuhakikisha inajiimarisha kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.

Alisema siku 10 zilizopita, timu ya NCCR ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti - Zanzibar, Haji Hamis Hamad ilianza ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya mkoa huo yanaendelea kuwa ngome yake.

“Kigoma nzima ina majimbo yetu ya kimkakati na Ukawa wameshatukabidhi sasa kilichobaki ni kufanya ‘political management’ (usimamizi wa kisiasa) katika kiwango kinachotakiwa.

Saturday, April 25, 2015

LONDON DERBY KATI YA ARSENAL NA CHELSEA

NAY WA MITEGO, SHAMSA MKE NA MUME!

Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.
Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili  liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.
...Wakipozi kimahaba.
“Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo.

Friday, April 24, 2015

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUWAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE NJOO LEO UONE VITU VIPYA‏

DSC_0340
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba mmoja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi(Kulia)
Ashura Kitenge akiimba kwa pamoja na Sam Mapenzi mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Joniko Flower(wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Aneth Kushaba AK 47 (kushoto) akiimba sambamba na Sony Masamba mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiwaimbia mashabiki wa bendi hiyo waliofika kwenye Kiota Cha Thai Village kuburusika na Bendi hiyo.

MAMA KANUMBA, MAMA LULU KIMENUKA!

Mwandishi wetu
Taarifa zilizotua kwenye dawati la gazeti hili zinadai kuwa, wale wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, sasa kimenuka!

Mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila.
DALILI KUWA PAKA NA CHUI
Chanzo chetu cha kuaminika kilidai kuwa, dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini.

CHANZO NI LULU
Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.


Mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
MAMA KANUMBA NA SMS MBAYA KWA MAMA LULU
Ilidaiwa kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba, mama Kanumba alimtumia mama lulu sms mbaya ya kejeli (kuiandika hapa siyo busara) ndipo mama Lulu ‘alipofyumu’ na kuona kwa hali hiyo bora kama mbwai na iwe mbwai.“Ile sms mama Kanumba alimtumia mama Lulu siku ile (Aprili 7) majira ya saa 11:00 alfajiri.

USAILI TMT MWANZA MEI 1-2, 2015

Thursday, April 23, 2015

WALALAMIKA KWA KUTOTAJWA KATIKA FILAMU YA FURIOUS 7

The Rock, Vin Diesel na Paul Walker ni baadhi ya majina ambayo yametajwa mwishoni mwa filamu ya kusisimua ya "Furious 7" iliyoingia sokoni hivi karibuni ... tatizo ni kwamba kuna baadhi ya watu ambao walishiriki kikamilifu kwenye matukio muhimu ya filamu hiyo ambao hawakupewa 'credit' mwishoni.
Sehemu ya matukio waliyoshiriki watu hao.
Vyanzo vya karibu na wazalishaji wa filamu hiyo vimeeleza kuwa watu hao walishiriki katika matukio muhimu ya filamu hiyo ikiwemo sehemu ya magari yenye parachuti na kukimbizana kwa magari maeneo ya milimani.
Mojawapo ya picha katika filamu ya Furious 7.
Kundi hilo la watu waliosahaulika limeeleza kuwa lilitoa jumla ya watu 25 ambao walihatarisha maisha yao katika filamu hiyo japo hawajatajwa mwishoni mwa filamu hiyo iliyojizolea umaarufu na kufanya vizuri sokoni ndani ya muda mfupi tangu itolewe.
Filamu hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza huko Australia Aprili 2, 2015, na baadaye kuzinduliwa nchini Marekani Aprili 3, 2015, na baada ya hapo iliachiwa kimataifa katika mfumo wa 3D.

Shindano la TMT 2015 lazinduliwa rasmi leo, Mwanza kufungua pazia tarehe 24 April 2015

Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.
 Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P
 Mmoja wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi wa TMT 2015, Saul Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote"
Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano hili.
Kwa kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es Salaam.
Katika kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.
TMT 2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May 2015.
Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na TMT kwa mwaka 2015
Kauli Mbiu ya TMT 2015 ni Mpaka Kieleweke.

HABARI NJEMA KWA WANABLOG, FORUMS WATANZANIANIA JUU UANDIKISHAJI WANACHAMA TBN

 
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN.

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Wednesday, April 22, 2015

Rihanna topless kwenye jarida la V

Riri aka Rihanna ameng’arisha jarida la V na picha mpya zilizorudisha muonekano wake wa Bad Girl Riri. Riri kaonekana kwenye picha hizi kifu wazi akiwa na wig la ki blonde. Kwenye interview na jarida hili amefunguka kuhusu album yake ya nane iliyotayarishwa na producer Kanye West.
rihanna-v-magazine rihanna-v-magazine-1 rihanna-v-magazine-2

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...