Thursday, May 28, 2015

KHADJA: NILIYEZAA NAYE, SITAKI HATA KUMSIKIA

LEO kupitia safu hii tunaye staa wa muziki wa kizazi kipya, Khadija Maige ‘Khadja’. Naye kama kawaida alibanwa na Mwandishi Wetu Shani Ramadhani kwa maswali 10 na bila hiyana alitoa ushirikiano katika kuyajibu.
Unajua aliulizwa nini na akajibu vipi? Ungana nami hapa chini.

Staa wa muziki wa kizazi kipya, Khadija Maige ‘Khadja’.
Ijumaa: Changamoto zipi unazozipata kupitia kazi yako ya muziki?
Khadja: Napata changamoto nyingi tu ikiwemo kutongozwa sana na wanaume. Pia baadhi wananikatisha tamaa wakidai eti siwezi kufika mbali wakati najua naweza.

Ijumaa: Wewe ni msanii sawa, lakini unajisikiaje unapovaa nguo za nusu utupu?
Khadja: Kwani tatizo liko wapi? Kama nikivaa hivyo najihisi niko huru, wewe kinakuuma nini?
Ijumaa: Wewe ni mtu wa aina gani, na je, ikitokea mtu amekuudhi ni kitu gani huwa unakifanya?
Khadja: Mimi ni mcheshi halafu napenda sana utani lakini kuna muda huwa nakuwa na roho mbaya hasa mtu akinikosea.

Ijumaa: Inasemekana wewe ni chapombe ile mbaya na ukilewa unakuwa mkorofi sana, hili likoje?
Khadja: Ni kweli huwa nakunywa pombe ila huwa silewi sana. Huwezi kuamini nikinywa pombe nakuwa mpole.
Ijumaa: Unawezaje kumudu muziki huku ukiwa unalea?
Khadja: Ni ishu ya kujipanga tu, yupo dada ambaye huwa ananisaidia kumlea lakini muda mwingi nikiwa sina shoo, nakuwa na mwanangu.

Ijumaa: Uliwahi kutamani kujiua kwa sababu ya kitu fulani?
Khadja: Sijawahi ila huwa natamani kuua kwa maana unakuta mtu anakuudhi kupita maelezo wakati muda huo una ‘stress’ zako.

Ijumaa: Wasanii mnatajwa kuwa na tabia ya kupora mabwana wa wenzenu, ulishawahi kupora au kuporwa?
Khadja: Huwa nasikia tu kwamba wapo mastaa ambao zao ni kuchukua waume za watu lakini mimi sijawahi kuporwa wala kupora.

Ijumaa: Ni kitu gani kinakufurahisha katika maisha yako?
Khadja: Mtoto wangu ndiyo furaha yangu, kila ninapomuona huwa nafurahi sana.
Ijumaa: Una mpango wa kuingia kwenye ndoa na mwanaume uliyezaa naye?

Khadja: Sina mpango huo na sitaki hata kumsikia kwani alinioa, tukashindwanwa hivyo siwezi kurudiana naye.
Ijumaa: Wewe ni mrembo, unawezaje kukabiliana na wanaume wakware?
Khadja: Mimi ni mrembo ndiyo ila kitu ninachokifanya ni kutowapa nafasi watu wa aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...