Tuesday, August 28, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TANO KCMC‏


Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza na Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC {kushoto} Profesa Raimos Olomi na Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya akina mama Dkt Gileard Masenga (kulia) mara baada ya kutoa msaada wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo. 
 
Benki ya ya KCB Tanzania, imetoa msaada wa shilingi milioni tano (5m) kusadia ununuzi wa vifaa katika wodi ya akina mama katika hospitali ya rufaa KCMC ikiwa ni jitihada za kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika kwa akina mama wajawazito,
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo uliofanyika hospitali hapo jana, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau alisema kuwa msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa msaada ambao benki hiyo iliutoa mwaka jana.
Mwaka jana tulikarabati chumba cha akina mama wagonjwa hatuti kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni kumi na moja. Nilipofamishwa kuwa chumba kilikuwa tayari lakini hakuna vifaa niliona kuna umuhimu kutoa msaada wa kununulia vifaa ili pesa iliyotolewa kwanza isiwe imepotea bure,” alieleza
Meneja huyo wa tawi alisema kuwa Benki yake imeamua kutoa msaada huo kwa kutambua umuhimu wa kusaidia serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhakikisha kuwa malengo ya millennia ya kuhakikisha kuwa vifo vya akina mama na mtoto vinakwisha kufikia mwaka 2015.
Akipokea msaada huo, Kaimu mkurunzi wa hospital ya KCMC Profesa Raimos Olomi alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika hospitali hiyo kutokana.
Vifo vya akina mama na watoto hapa nchini bado ni vingi. Jitihada kubwa zinahitajika kuvipunguza. Kupitia misaada ya wadau mbalimbali kama huu wa Benki ya KCB lengo linaweza kufikiwa. Tunaishukuru sana Benki ya KCB kwa msaada huu muhimu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake hospitalini hapo Dr Gileard Masenga alisema kuwa hospitali hiyo haikuwa na wodi ya akina mama mahututi na kuongeza kuwa msaada huo utasadia kuokoa maisha ya akina mama na watoto.
Mwanzoni tulikuwa tunalazimika kuwapeleka akina mama kwenye hodi za wagonjwa hahututi ambazo wagonjwa wote wanatibiwa. Tunaamini msaada huo utasaidia kuboresha hali na hivyo kuokoa wakina mama wengi zaidi. Tunaishukuru Benki ya KCB kwa kuwekeza katika afya ya mama na mtoto,” alifafanua.

Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya makabidiano ya hundi yenye thamani ya shilingi 5m/- kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau akimkabidi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- kwa Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya KCMC {kulia} Profesa Raimos Olomi kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC.
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 5m/- mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga. Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali. Katika kati ni Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC Profesa Raimos Olomi
Kaimu mkurugenzi wa wa hospitali ya KCMC rofesa Raimos Olomi akiifurahia hundi ya shilingi 5m/-iliyotolewa na Benki ya KCB kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali ya KCMC. Kushoto ni Meneja wa Benki ya KCB tawi la Moshi Lomnyaki Saitabau.
Mkuu wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospital ya KCMC Dr Gileard Masenga akitoa maelezo kwa Emmanuel Grayson ambaye ni mkuu wa masuala ya kijamii wa Benki ya KCB tawi la moshi juu ya wodi iliyokarabatiwa na benki hiyo mwaka jana mara baada ya kutoa msaada wa wa 5m/- kusaidia ununuzi wa vifaa katika chumba cha wanawake wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...