Sunday, April 20, 2014

DUDE ‘APIGWA’ TENA!

MGANGA hajigangi! Licha ya kuwa msanii mahiri anayeelimisha jamii jinsi ya kugundua utapeli na kuepukana nao, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibiwa ‘kupigwa’ vifaa vya saluni na vibaka.

Msanii mahiri Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Akistorisha na mwanahabari wetu, Dude alisema juzikati vibaka hao walipanda kwenye dari na kukata ‘celling board’ kisha kuingia ndani ya saluni yake hiyo ya kike inayosimamiwa na mkewe, maeneo ya Jeti-Lumo, Dar na kukomba vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba.

“Ukweli nimechoka sasa kila siku wananirudisha nyuma kimaendeleo kwa kuniibia sijui nifanyeje maana imeshakuwa hatari kwangu, wamechukua TV, madela, redio aina ya sabuufa na vingine vidogovidogo,” alisema Dude ambaye mwaka 2012 na 2013 aliwahi kulizwa vifaa mbalimbali vya nyumbani.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...