Ni siku chache tu zimepita toka Paul Okoye wa kundi la P-Square afanye harusi ya kimila na mke wake Anita Isama huko Nigeria, lakini baada ya wote wawili (Peter & Paul) kukamilisha majukumu ya ndoa zao, kuna habari ambazo zimesambaa wiki hii kuwa umeibuka ugomvi baina ya mapacha hao wa kundi la P-Square ambao inasemekana sasa hawaelewani vizuri.
Mtandao wa Naija Gists umeripoti kuwa kwa mujibu wa chanzo, inadaiwa kuwa kumekuwa na kutoelewana baina ya kaka mkubwa wa mapacha hao Jude Okoye na mke wa mdogo wake Peter Okoye aitwaye Lola Omotayo, kitu kilichopelekea Jude kutohudhuria harusi yao mwaka jana.
Kama unakumbuka Jude hakuhudhuria harusi ya Peter na Lola mwaka jana, lakini alihudhuria ya Paul na Anita mwaka huu kitu kinachowafanya watu waamini kuwa kuna tatizo kubwa baina yao.
Chanzo hicho kimesema inadaiwa kuwa ugomvi huo unaomhusu Lola umesababisha Peter na Paul kugombana wakati wako kwenye rehearsle Jumatano wiki hii, mpaka walipoachanishwa na dancers wao.
Kaka mkubwa wa P-Square Jude alitweet kitu ambacho kinaaminika kuwa kinahusiana na ugomvi wao.
“After over 10 years of hard work, it’s over. (I) Am done.” ikiaminika kuwa alimaanisha amejiondoa kuli-manage kundi hilo japo kuwa yeye mwenyewe hakufafanua alichomaanisha katika maneno hayo machache.
After over 10yrs of hard work, it's over. Am done.
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 18, 2014
Jude ndiye amekuwa akiwa-manage kwa miaka yote na kuproduce hits zao paomoja na kudirect idadi kubwa ya video zao zilizofanya vizuri.
Lakini kuna baadhi ya watu nchini Nigeria wamedai kubwa kuna uwezekano kuwa ugomvi ‘hewa’ unaoendelea na kuripotiwa katika vyombo vya habari ukawa ni ‘hype’ ya kuandaa ‘kiki’ ya album yao mpya
No comments:
Post a Comment