Thursday, August 29, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 KUUNGURUMA MTWARA JUMAMOSI HII



WASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya wapatao 15 wanatarajiwa kutoa burudani kwa mara ya kwanza mjini Mtwara kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2013, katika Uwanja wa Nangwanda uliopo mjini hapo. Burudani hiyo itakuwa kivutio tosha kwa wakazi wengi kutokana na kundi kubwa la wanamuziki wa Kizazi Kipya kufanya makamzi kwa pamoja na wasanii wachanga wa mkoani hapo.

Siku hiyo majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 4, kutakuwa na Semina maalumu ijulikanayo kwa jina la Kamata Fursa Twenzetu, yenye lengo la kuwaonyesha wakazi wa pande hizo namna ya kujikwamua kimaisha katika kutumia fursa zilizopo mahali hapo, semina hiyo itaongozwa na viongozi wa Mkoa huo sambamba na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo la usiku.

Siku hiyo pia msanii mkali katika miondoko ya kuzungusha nyonga Snura Mushi anayetamba na kibao cha majanga atakamua sambamba na Nay wa Mitego, Makomandoo, Juma Nature, Matonya, Kassim Mganga, Chege na Temba,Madee, Young Killer, Stamina, Godzilla, Nikki wa Pili, Ommy Dimpoz, Kalapina na Pasha mtoto wa Mtwara wataonyesha umahiri wao katika muziki huo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...