Saturday, August 31, 2013

SEMINA YA SERENGETI FIESTA KAMATA FURSA YAZIDI KUUNGURUMA MTWARA



Mkurugenzi wa Vipindi na maendeleo wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo ndani ya Ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara, kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano wa NSSF Makao makuu jijini Dar, Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.

Meneja Kiongozi,Uhusiano wa NSSF kutoka  Makao Makuu jijini Dar es Salaaam, Eunice Chiume akizungumza mapema leo kwenye semina ya Kamata  Fursa Twenzetu, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara mjini ,kulia ni Meneja wa NSSF wa  mkoa wa Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi na Maendeleo wa  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala Mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini hapo, Semina hiyo ni mpango mathubuti wa timu nzima ya Clouds Media Group ambayo inafadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo, na hii hufanyika mapema kabla ya shoo ya Serengeti Fiesta kulindima kwa siku maalum.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha.  
Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpo ambaye pia ni mwanachama wa NSSF,akizungumzia fursa mbalimbali alizozipata ndani ya shirika la NSSF,mbele ya wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kushiriki katika semina hiyo,iliyokuwa na mafanikio makubwa.


Baadhi ya akina mama wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye semini hiyo


Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.Katika semini hiyo vijana wemejitokeza kwa wingi.

Msanii wa Kughani mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Mtwara kuhusiana na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa huo. 
PICHA:MICHUZI JR BLOG

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...