GK akiwa ndani ya Studio za Clouds FM wakati akielezea kuhusu ujio wake.
MSANII mahiri katika anga za muziki wa Bongofleva, Gwamaka Kaihura
'King Crazy GK' leo ameibuka na singo yake mpya iitwayo Baraka au Laana
aliyomshirikisha msanii Yuzo.
GK alikuwa kimya kwa takribani miaka sita
baada ya kuwa busy na masomo kitendo kilichopelekea kuupa kisogo muziki
kwa muda na kuwafanya mashabiki wake kum-mis katika fani hiyo.
Memba
huyo wa East Coast Team ameachia ngoma yake mpya leo na anataraji
kuachia video yake siku ya Ijumaa Agosti 30, mwaka huu.
Akiongea na MTANDAO HUU,
GK alisema kuwa amerudi kwenye game kwa nguvu zote na amewashukuru
baadhi ya wadau kama Eric Shigongo, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa
kumtia hamasa ya kurudi kwa nguvu mpya baada ya kupotea kwa muda.
No comments:
Post a Comment