The Hero.... Staam anatajwa kuwa shujaa wa Ndanda ambayo haijafanya vema ligi kuu bara |
Aliyewahi kuwa
kocha msaidizi wa Simba, Amri Said 'Jap Staam' ametajwa kuwa mchawi wa timu ya Ndanda
ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu imekuwa na mwendo wa ‘bata’ tofauti
na kasi iliyokuwa nayo kwenye ligi daraja la kwanza.
Said maarufu
zaidi kwa jina la Staam, kwa sasa yupo na kikosi cha Mwadui akisaidiana na Jamhuri ‘Julio’
Kihwelo ambayo ina nafasui nzuri ya kupanda ligi kuu msimu ujao iwapo tu
itashinda mechi zake dhidi ya Polisi Tabora na Burkina Faso.
Habari
zilizopatikana zinadai kuwa mashabiki wa timu ya Ndanda wamekuwa wakiuliza
kuondolewa kwa kocha huyo, kwani timu ilikuwa ikifanya vema enzi za kipindi chake
tofauti na sasa kwenye ligi kuu.
Kwa upande
wa Staam alipoulizwa kama anaweza kuwasikiliza tena Ndanda, alisema: “Mhh…ni ngumu
ndugu yangu, kwanza nina mkataba na Mwadui na pia kwa kipindi kama hiki ni vigumu
maana siwezi kuichukua timu katikati ya msimu, labda ingekuwa mwishoni mwa
msimu ili niweze kuanza program zangu mwenyewe,” alisema Staam.
Unakumbukwa sana na Wana Kuchele wa Ndanda |
No comments:
Post a Comment