Pluijm |
Uongozi wa
klabu ya Yanga, umesema unaamini kocha wake, Hans van Der Pluijm ana nafasi kubwa ya
kuwa klabuni hapo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na falsafa inayoendana na
sekretarieti iliyopo madarakani kwa sasa.
Pluijm
anatajwa kuwa kocha bora wa Jangwani katika misimu ya hivi karibuni, kutokana na mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi alichokaa na timu msimu uliopita na uongozi unaamini atafanya mambo makubwa kutokana na mtazamano wake, lakini
wakatoa angalizo kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na
kumuacha kocha afanye kazi yake.
Akizungumzia
kasumba ya timuatimua ya makocha, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha
alisema uongozi umetokea kumuamini Pluijm kutokana na mawazo chanya aliyonayo
katika maendeleo ya soka klabuni hapo na kuamini anaweza kuwa nao kwa muda
mrefu.
“Popote
pale, kocha uhukumiwa na matokeo mabaya, kwa hiyo katika hili sio kusema Yanga
ina tabia ya kufukuza makocha, sema wanafanyiwa mabadiliko kutokana na aina ya
matokeo. Lakini naweza kusema kwa sasa ni tofauti kidogo kwa kocha Pluijm.
“Kwanza ni
mtu mwenye mtazamo chanya, tunaendana kimawazo, amekuwa akitupa ushauri chanya
katika kuimarisha vikosi vyetu- vijana na wakubwa. Binafsi namuona kama ana
maisha marefu Jangwani, ila tu angalizo ni kwa mashabiki wetu, wanatakiwa kuwa
wavumilivu na kutodhubutu kuingilia kazi yake. Maana soka la Tanzania
limezoeleka kuendeshwa na mashabiki. Tunaamini wakibadilika na kumuacha afanye
kazi yake, hakika atatufikisha mbali,” alisema Tiboroha.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, kushoto. |
No comments:
Post a Comment