Moja ya mechi ambazo Messi alipigwa benchi msimu huu, jambo ambalo si rahisi kusikia kwa nyota huyo. |
KIUNGO mwenye heshima ndani ya
Barcelona, Xavi Hernández kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu sakata la
kutoelewana kwa nyota wa klabu hiyo, Leonel Messi na kocha wake, Luis Enrique
ambapo amesema kuwa wawili hao wamemaliza tofauti zao na mambo ni shwari kwa
sasa.
Messi na Luis wamekuwa wakiripotiwa
kutokuwa na maelewano mazuri na kwamba walikwaruzana kwenye mazoezi, lakini Xavi amefunguka kuwa. "Kila kitu
kimeeleweka, sio ishu kubwa kwa sasa. Kuanzia kwenye makundi yao,
tumelichukulia kwa ukubwa unaostahili, lilitokea lakini sasa limebaki historia.
Akizungumzia timu yake Xavi alisema: "Kila
mmoja na shauku ya ushindi. Kila mmoja anajisikia ari ya kushinda na tupo
tayari katika hilo."
Amekwenda mbali na kummwagia sifa Neymar kwa kusema: "Ni mchezaji wa kipaji cha juu na
tunajisikia faraja sana kuwa naye katika kikosi chetu. Ni mtu wa kipekee ana
aina yake ya uchezaji, mwenye uelewa mkubwa wa soka na maisha ya yake anayoishi
ni tofauti kabisa. Unatakiwa kujua jinsi gani ya kushinda, kushindwa, lakini
hilo ni tofauti kwa Neymar. Ana maisha yake fulani hivi.
Xavi Hernanedz |
No comments:
Post a Comment