Hatua moja mbele...kiungo wa Colombia na Fiorentina Juan Cuadrado anaenda Stamford Bridge muda wowote. |
Kocha wa Fiorentina, Vincenzo Montella
amefunguka kuwa kiungo wa timu hiyo, Juan Cuadrado atajiunga na Chelsea na
kuongeza kuwa licha ya kumhitaji lakini isingekuwa rahisi kumbakiza kutokana na
ofa kubwa waliotangaziwa ambayo katu kama klabu wasingeipiga chini.
Matajiri wa London, Chelsea, wanatajwa
kutenga kitita cha euro milioni 35 kwa ajili ya kuansa saini kiungo huyo raia
wa Colombia pamoja na kuwaongezea Mohamed Salah kwa mkopo.
Licha ya kwamba mpaka sasa pande mbili
hazigongeana mihuri ya uthibitisho wa biashara hiyo, lakini Montella amesema
kuwa anamchukulia Cuadrado kama mchezaji wa zamani wa Fiorentina alipoongea
kwenye mkutano wa habari jana Ijumaa jioni.
"Isingewezekana kwa
kukwamisha dili lake," alisema Montella.
"Kwa mtazamo wangu kama kocha inakatisha tamaa lakini klabu ilikuwa na
haki ya kufanya hivyo.
"Mchezaji wa kiwango cha juu ameondoka,
ingawa bado naona sifa zake kwa Salah (mbadala wake). Sidhani kumuuza ni sababu yetu kurudi
nyuma.
[Cuadrado] ni mchezaji wa kimataifa
na siku zote alipenda kuwa nasi , pia na mimi najivunia kuwa anakwenda
kujiunga na timu kubwa duniani."
Cuadrado kushoto katika moja ya mechi alizoichezea Fio msimu huu, hapa akijaribu kumpita moja wa mabeki wa AS Roma |
No comments:
Post a Comment