Faulo iliyomgharimu Costa wa Chelsea kwa kumkanyaga Can wa Liverpool wakati wa mchezo wa Capital One mapema wiki hii |
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ametoa
ya moyoni juu ya kufungiwa kwa straika wa Chelsea, Diego Costa kwa kumtaka
abadilike ili kuendeleza kipaji chake.
Pellegrini aliyaongeza hayo jana katika
mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu England wakati timu
hizo zitakapomenyana leo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Costa, 25, atakuwa
jukwaani leo pamoja na mechi dhidi ya Aston Villa na Everton akitumikia adhabu aliyopigwa
na Chama cha Soka England, FA, la kukosa mechi tatu kwa kosa la kumkanyaga maksudi kiungo wa Liverpool,
Emre Can wakati wa mechi nusu fainali ya Kombe la Ligi ‘Capital One’, kitendo
ambacho Pellegrini amesema: “Hatakiwi kucheza katika aina ile ya uchezaji wake
kwa kuwa yeye ni mchezaji mzuri sana.”
Mbali na tukio hilo, Costa amekuwa akitajwa kwa ugomvi uwanjani ambapo mara kadhaa amekuwa akikwaruzana na wachezaji timu pinzani huku mpaka sasa akiwa amezawadiwa kadi za njano nane msimu huu.
Kuhusu mechi
yao ya leo, kocha huyo raia wa Chile, alisema: "Sio mechi ya kuamua
ubingwa, sababu baada tya mechi yenyewe kuna pointi 45 tunapigania pia. Na ikumbukwe kuwa tuliwahi
kutwaa ubingwa baada ya kuwa nyuma kwa pointi
nane nyuma ya Manchester United, tukiwa tumebakiza mechi sita tu (ilikuwa msimu
wa 2012)".
"Kwa hiyo katika soka, huwezi kujua. Lakini mechi
hii ina umuhimu sana ambayo itatufanya
tupunguze gepu kati yetu na wao kileleni."
No comments:
Post a Comment