Monday, February 8, 2016

KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA KUUNDA MUUNDO MPYA WA UTENDAJI WA KUBORESHA HUDUMA ZAKE!


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano akifafanua jambo.





Kampuni ya Simu za mkononi nchini Airtel Tanzania, leo imetangaza mkakati wake wa kuboresha muundo katika nafasi zote za utendaji kuwa bora zaidi na kuweka idadi sahihi ili viwango vya kiutendaji kuimarika na hatimae dhamira yake ya pkibiashara ya kutoa huduma na bidhaa bora za kimawasiliano nchini Tanzania kufikiwa.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano alisema “ Mkakati huu wa kuboresha upya mfumo wa utendaji wa kampuni yetu ni sambamba kabisa na mfumo wetu wa maboresho uliowekwa na kampuni yetu ambao tunaamini baada ya muda mfupi utakuwa na mafanikio makubwa kwa wadau wote wakiwemo wafanyakazi na wateja wetu tunaowahudumia”
Singano akifafanua alisema “Maboresha haya tunayofanya yatawahusisha takribani wafanyakazi 55 kwa nafasi zao za utendandaji kutokuwepo au kuhamishiwa kwa wadau watakao toa huduma kwa kampuni yetu, mfumo ujulikanao kama “outsource model”, watoa huduma tutakaowapa jukumu la kusimamia baadhi ya huduma zetu”

Airtel tangu kuanza kwa mkakati huu wa maboresho yake ya kiutendaji kwaajili ya kutimiza malengo ya kibiashara imejizatiti kwa kuweka miundombinu madhubuti kwa kuingia mikataba ya kiutendaji.

“Vilevile kama njia ya kushirikiana na wale watakao guswa na zoezi hili la marekebisho ya mfumo huu kipindi hiki cha mpito, Airtel tayari imeingia mkataba na kampuni inayohusiana na huduma za rasilimaliwatu ili kutoa mafunzo na ushauri wa kutosha ya jinsi ya kutafuta na kuzipokea nafasi zingine zinazojitokeza, Malipo ya huduma hii kwa wote watakaohitaji yamegaramiwa na Airtel” alimaliza kwa kusema Bi, Singano .

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...