Monday, February 8, 2016

HII NDIYO KAULI YA KOCHA MPYA MBEYA CITY MUDA MFUPI BAADA YA KUKABIDHIWA KUIONGOZA TIMU HIYO!

Kocha mpya wa Mbeya City FC, Kinah Phiri (katikati), akizuingumza jambo muda mfupi baada ya kukabidhiwa kuiongoza timu hiyo.
“Nimefurahi kujiunga na timu hii, ni moja ya timu nzuri na kubwa kwenye soka la Tanzania, ila naomba watu watambue kuwa kuijenga City si jukumu langu peke yangu, ushirikiano kutoka kwa uongozi wa jiji, viongozi wa klabu, bodi pamoja na mashabiki naamini utafanikisha kazi yangu na kutufanya sote kufikia malengo, nimekuja katikati ya msimu lengo langu kwanza ni kuhakikisha timu inabaki kwenye ligi, huo utakuwa mwanzo wa ujenzi imara kwa ajili ya msimu mpya”

Kauli ya Kocha mkuu mpya wa City Kinnah Phiri akizungumza mbele ya wana habari mara baada ya kukamilisha zoezi la kutia saini kandarasi yake ya miaka mitatu kuliongoza benchi la ufundi mapema leo kwenye ofisi ya Meya wa jiji la Mbeya.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...