Monday, February 8, 2016

MRAMBA,YONA WAFANIKISHA ZOEZI LA USAFI KWENYE HOSPITALI YA PALESTINA SINZA


Daniel Yona akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili Hospitali ya Palestina, Sinza – Dar.

WALIOKUWA Mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona leo wameanza kutumikia adhabu ya kifungo cha nje, kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza, Palestina, ya jijini Dar, kulingana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita kuhusu kesi iliyokuwa ikiwakabili.

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini waliwasili mapema leo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Hospitali ya Sinza Palestina ili kuanza kutumikia adhabu hiyo kama mahakama ilivyowaamuru.

Baada ya kuwasili hospitalini hapo, Yona na Mramba walipokelewa na ofisa huduma za jamii Bw. Deogratius Shirima na wananchi wengine waliokuwepo kushuhudia vigogo hao wakitumikia adhabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Shirima alisema kuwa, leo ilikuwa ni siku ya kuwapa maelekezo namna ambavyo watafanya usafi, maeneo ya kufanya usafi pia walikabidhiwa vifaa watakavyovitumia kufanyia usafi kuanzia kesho.

Baadaye Afisa Mazingira hospitalini hapo Bi. Miriam Mongi, aliwakabidhi Yona na Mramba vifaa vya kufanyia usafi ambavyo ni; mifagio, mafyekeo, viatu vya kufanyia usafi maarufu kama “gambuti” na glovusi.

Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya ndipo hivi karibuni baada ya mahakama kupitia upya kesi hiyo ikaamuru wapewe adhabu ya kifungo cha nje huku wakifanya kazi za kijamii kwa muda wa saa nne kila siku kwa miezi sita.
Yona na Mramba wakiwa wameshika vifaa vya kufanyia usafi.
Yona akionesha vifaa vya kufanyia usafi alivyokabidhiwa.
Mramba na Yona wakikabidhiwa vifaa vya kufanyia usafi.
Wakioneshwa mazingira ambayo watakuwa wakiyafanyia usafi kwa kipindi chote cha adhabu yao.Ofisa Mazingira wa Hospitali ya Palestina-Sinza, Bi. Miriam Mongi (mwenye brauzi nyekundu) akimkabidhi Yona vifaa vya kufanyia usafi.Yona na Mramba wakiwa wamevaa ‘ovaroli’.
Ofisa Huduma za Jamii wa Hospitali ya Palestina – Sinza, Bw. Deogratius Shirima akizungumza na wanahabari hospitalini hapo 
Maeneo ya hospitalini hapo.
Gari lao likiwasili.
Yona akiwasili hospitalini hapo.Takataka katika baadhi ya maeneo hospitalini hapo. 
Wanahabari wakichukua matukio.



No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...