Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Amsha Mama 2016 Tundaman (kulia), akiongea jambo na mama Rishe Sophia Amri au maarufu kwa jina la Mama Dayna muda mfupi baada ya kumkabidhi kiasi cha shilingi laki moja ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza kampeni ya Amsha Mama 2016, aliyoanza kutekeleza majuku yake mapema leo katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia zoezi hilo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kampeni hiyo Joe Kariuki.
Tundaman akiongea jambo na mama huyo baada ya kumaliza kumchangamsha kwa kumpatia kiasi cha shilingi laki moja Antonia Msomboki.
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundaman akichagua nguo moja wapo zilizokuwa zikiuzwa na Mjasiliamali Sakina Thomas, kulia ni Mkurugenzi wa Kampeni hiyo Joe Kariuki.
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundaman (katikati), akimkabidhi kiasi cha shilingi laki moja Antonia Msomboki ambaye ni mfanya biashara wa matunda katika soko la Tandale jijini Dar, mapema leo.
Mkurugenzi wa Kampeni ya Amsha Mama Joe Kariuki (kushoto), akiingia kwenye genge la kuuzia vyakula la Sophia Amri huku akiwa sambamba na Balozi wa kampeni hiyo Tundaman.
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundamani akikatiza kwenye mitaa ya Tandale na baadhi ya wanahabari waliojitokeza kushuhudia tukio hilo
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundama kutoka kushoto akiongea jambo na muuza mitumba Sakina Thomas huku Mkurugenzi wa kampeni hiyo Joe Kariuki akisikiliza kwa makini maongezi hayo.
TUNDAMAN AAMSHA AKINAMAMA TANDALE
BALOZI wa Kampeni ya Amsha Mama Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ameanza rasmi kutekeleza majukumu yake ya Kibalozi kwa kutembelea maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam, ambapo amekukutana na baadhi ya kinamama wanaojishughulisha na biashara ndogondogo.
Msanii huyo ambaye amepewa Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha la AFWAB AMSHA MAMA 2016, lililo chini ya Mkurugenzi mtendaji wa lebo ya Candy na Candy Records Joe Kariuki, linalotarajiwa kufanyika Machi 25-27 mwaka huu katika uwanja wa Kedong ranch uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya.
Katika ziara hiyo ya kushtukiza iliyofanywa na Tundaman pamoja na Muandaaji wa Tamasha hilo Kariuki waliweza kutumia muda huo kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba katika soko hilo.
Tundaman na Kariuki waliwapatia akina mama hao kila mmoja kiasi cha shilingi laki moja ikiwa ni njia moja wapo ya kutimiza adhima yao ya kuwaamsha akina mama wa Tanzania.
Kariuki alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha akina mama katika tamasha litakalowakutanisha na akinamama wengine kutoka nchi mbalimbali Afrika kwa lengo la kujifunza na kupewa utaalam na jinsi kukuza biashara zao.
No comments:
Post a Comment