KIPINDI cha EFM Sports Headquarters kinachosikika kupitia Radio ya Efm usiku wa kuamkia leo kiliadhimisha mwaka mmoja tangu kianze kurushwa ambapo pati yake ilifanyika katika Ukumbi wa Sports Lounge, Posta jijini Dar.
Kipindi hicho cha Sports HQ ambacho kinazungumzia michezo mbalimbali hapa nchini na nje kilianzishwa mwaka jana Februari 27, ambapo kinaongozwa na mkuu wa kitengo cha michezo redioni hapo Maulid Kitenge na msaidizi wake, Omari Katanga.
Pati hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bethidei hiyo ambayo ilianza majira ya saa 12 jioni na kumalizika usiku.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Nape alisifia uwezo wa watangazaji wa kipindi hicho licha ya kuwa na muda mfupi kwa kuwa na uwezo wa kuhoji maswali ambayo yamekuwa na tija.
No comments:
Post a Comment