|
Mkurugenzi
Mtendaji wa klabu ya Jozi Lounge, Dismas
Massawe, akikata utepe kuashiria shughuli ya uzinduzi wa klabu hiyo.
|
STAA wa muziki
wa Bongo Fleva anayeupiga kwa njia ya bendi, Banana Zahir Zorro, usiku wa
kuamkia jana aliwapagawisha vilivyo
mashabiki wake kwenye uzinduzi wa klabu mpya ya burudani ya Jozi Lounge
iliyopo Msasani Village karibu na shule ya msingi Msasani jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo
uliokatwa utepe na mmiliki wa klabu hiyo, Dismas Massawe, ulifanyika usiku
mnene huku ukishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa burudani ambao walijitokeza
ambapo Banana kupitia timu yake ya
B-Band alisongesha burudani.
Akifanya
makamuzi muda mfupi tu baada ya uzinduzi kufanywa, Banana alitangaza kuwa kila siku ya Jumamosi bendi
yake itakuwa ikifanya makamuzi hapo, hivyo akawataka mashabiki wajitokeze kwa
wingi ili kupata burudani ya kipekee.
“Nimefurahi sana
leo kukutana na mashabiki wangu kwenye tukio hili la uzinduzi hivyo nitumie
fursa hii pia kuwatangazia kwamba tutakuwa tukitumbuiza hapa kila siku ya Jumamosi,
hivyo naomba mashabiki wangu wote tuwe tunakutana hapa kupata muziki mzuri na
vinywaji safi kwa bei poa,” alisema Banana Zorro.
|
Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva, Banana Zorro, akitoa burudani muda mfupi baada ya
uzinduzi wa klabu hiyo. |
|
Baadhi
ya mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo wakiingia ndani ya klabu hiyo baada ya
kuzinduliwa. |
|
Mbunifu wa
mavazi nchini, Rhemtulah (kulia) akiwa
na jamaa zake kwenye uzinduzi huo.
|
|
Baadhi ya waalikwa
kwenye uzinduzi huo wakiwa katika pozi.
|
|
Mtangazaji
maarufu Tayana (kulia), akiwa katika pozi na wenzake. |
|
Mashabiki
wakiwa ndani ya Jozi Lounge. |
|
Wadau wa klabu
hiyo wakiwa katika pozi.
|
|
Tayana
akiwa kwenye pozi. |
|
Wadau
wa Jozi Lounge wakiwa kwenye zulia jekundu (red carpet). |
|
Dismas Massawe
(kulia, akipozi mbele ya kamera.
|
|
Wageni Red
Carpet.
|
|
Baadhi
ya warembo waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa kwenye pozi. |
|
Mapozi
yalitawala kwa mashabiki waliofika hapo.
|
|
Wadau
wa ‘mastarehe’ wakiwa kwenye pozi. |
|
: Waalikwa wakiingia ndani ya Jozi Lounge muda
mfupi baada ya uzinduzi huo kufanyika.
|
No comments:
Post a Comment