Saturday, January 30, 2016

SIMBA YAIKANDAMIZA 4-0 AFRICAN SPORTS YA TANGA


Klabu ya Simba imeendelea kuzikimbiza Yanga na Azam katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu baada ya kufanikiwa kuichapa African Sports kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Hamisi Kiiza ameibuka shujaa wa mchezo huo akifanikiwa kuweka bao mbili kambani ndani ya kipindi cha kwanza huku bao la tatu ndani ya kipindi cha kwanza likifungwa na Hasan Kessy.Beki wa African Sports (kushoto) akimdhibiti Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Simba vs African Sports
Bao la ushindi la mnyama wa Msimbazi limekwamishwa wavuni na Haji Ugando na kukamilisha kalamu ya mabao kwa siku ya leo.
Matumaini ya Simba kuibuka kidedea kwa kutwaa ndoo ya ligi msimu huu yameibuka baada ya mtani wao Yanga kukwama jijini Tanga mbele ya Coastal Union kwa kipigo cha bao 2-0. Azam ambao leo wangecheza na Tanzania Prisons hawapo nchini hivyo mchezo huo umeahirishwa hadi hapo watakaporejea nchini.
Yanga bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 36, Azam wako nafasi ya pili kwa pointi 36 sawa na Yanga lakini wao wanafaida ya mchezo mmoja mkononi ambao walitakiwa wacheze leo.
Matokeo hayo yanaiingiza Simba kwenye orodha ya timu ambazo zinawania ubingwa msimu huu kutokana na tofauti ya pointi lakini bado kuna mechi nyingi ambazo zinaweza zikaamua nani ataibuka bingwa wa msimu huu.
Jackson Mayanja ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu kwa muda tangu kutimuliwa kwa Dylan Kerr ameendelea kufurahia ushindi ndani ya klabu hiyo kwani ameshinda mechi zote ambazo ameingoza Simba.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...