Friday, January 29, 2016

MBWANA SAMATTA AKABIDHIWA JEZI ATAKAYOITUMIA RASMI KATIKA KLABU YA KRC GENK UBELGIJI


Viongozi wa Klabu ya KRC Genk wakimtambulisha Samatta.

BOSI wa TP Mazembe, Moise Katumbi, amemfuata straika wake, Mbwana Samatta nchini Ubelgiji ili kuweka mambo sawa ili mchezaji huyo ajiunge na Klabu ya KRC Genk.
Samatta alitangulia kwenda Ubelgiji ambako alifika juzi Alhamisi na kukutana na wakala wake ambaye walianza kukamilisha taratibu za mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo, lakini Samatta, jana alitambulishwa rasmi klabuni hapo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na nusu.
Katumbi yeye anawasili Ubelgiji, leo Jumamosi kuungana na Samatta na wakala wake kukamilisha baadhi ya mambo licha usajili wa mchezaji huyo kuwa umekamilika.
“Katumbi amefika leo (jana) na alijiunga na Samatta kukamilisha mambo ya msingi na viongozi wa Genk na mambo yapo sawa, yaani Samatta ni mali ya Genk,” alisema ofisa huyo.
Tovuti ya Genk pia iliandika jana kuwa, Samatta tayari ni mchezaji wao na anaweza kutumika muda wowote.
Awali Katumbi alionekana hataki Samatta ajiunge na Genk kutokana na klabu hiyo kutotumia njia sahihi katika kumsainisha mkataba wa awali bila kuwasiliana na TP Mazembe.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...