Friday, January 29, 2016

Q-CHILLAH KUTAMBULISHA BENDI YAKE KESHO NDANI YA BILICANAS

Q-Chillah akicheza na mashabiki zake kwenye moja ya maonesho yake ya nyuma.
BAADA ya kuutumikia Muziki wa Bongo Fleva kwa muda mrefu, mkongwe Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ ametangaza kuibuka na bendi itakayofahamika kwa jina la QS International.
Akizungumza na gazeti hili, Januari 26, mwaka huu, Chillah alisema Jumapili hii ametangaza hali ya hatari kwa wasanii wote kwa kuzindua bendi hiyo katika Ukumbi wa Bilcanas, Posta jijini Dar ambapo itakuwa ikipiga muziki mchanganyiko kila wiki kwa ratiba itakayotangazwa hapo baadaye.

Msanii wa Bongo Fleva ‘Q-Chillah akiwa katika pozi’.
“Nimejipanga sana kuja kivingine kwani hapo mwanzo nimekuwa nikijitahidi kadiri ya uwezo wangu ili nirudi katika Bongo Fleva lakini mambo yalikuwa magumu, namshukuru Mungu kwa sasa nimepata kampuni mpya ya kusimamia kazi zangu za muziki ya QS Mhonda J Group of Company ambayo imenipa vifaa vya bendi.

“Kwenye bendi hii nitakuwa na M-Dog na wanamuziki wengine kibao yaani jumla na wapiga vyombo tunaweza kufikia hata kumi, nimejipanga kufanya vitu vizuri kwani nimefanya uchunguzi wa kina katika bendi nyingi maarufu za hapa nchini kuna upungufu mkubwa hivyo nitaufanyia kazi,” alisema Q-Chillah.
Q-Chillah anayetamba na Wimbo wa Mkungu wa Ndizi, kwenye utambulisho wake huo anatarajia kusindikizwa na wasanii kama Chaz Baba, Juma Nature, Bushoke, Abdul Misambano na Banana Zorro.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...