Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn
Mworia akionesha namba ya Red Alert ambayo watanzania wote wenye nia ya
kuwasaidia wahanga watume michango yao kwenye hiyo namba.Jinsi ya kutuma
ponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya
hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba
155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu
baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio
la mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo
imesababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha
familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.
Akiongea na waandishi wa habari leo,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano
na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba
watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye
namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya
155990.
“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na
tunawapa pole waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa
janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo
chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania
wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na
tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao
wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.
Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya
kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa
waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi
moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto
jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi
ya uchangiaji.
Jinsi ya kuchangia ni rahisi sana unachotakiwa kufanya unaponyeza
*150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo
utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990
alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya
hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
No comments:
Post a Comment