Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon Chonde amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja limepitishwa kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na wafanyabiashara hao.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo wa kodi uliopo umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili waendelee kuwa tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyabishara wadogo.
Chonde amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni ameitaka Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili kumsaidia mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
Naye Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado ni machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la zima moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
Pia amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.
No comments:
Post a Comment