Sunday, March 8, 2015

SIKIA ALICHOKISEMA KOPUNOVIC BAADA YA KUIZIMA MDOMO YANGA

Wakemaaaaaa!!!!!
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameshindwa kuzuia furaha yake baada ya kufanya maajabu ya kuipa ushindi wa kwanza Simba mbele ya Yanga, ukiwa ni mchezo wa kwanza baada ya kupita misimu mitatu.
Ushindi wa leo wa bao 1-0 wa Simba kwa upande mwingine ni mwendelezo wa ubabe kwa Yanga kwani katika michezo mitano ya mwisho kukutana, Simba imeshinda mara mbili huku wakitoa sare katika mechi tatu.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo uliopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Kopunovic alitoboa siri kuwa ni kutokana na kuwapa maelezo wachezaji wake kucheza soka la pasi fupifupi na kukaba kwa nguvu zote.
Pia maelezo yake yalitokana na kuwasoma Yanga kabla ya mchezo huo kuwa vinara wa pasi ndefu hivyo pasi fupi zingewasumbua.

Okwiiiiiii,, akishangilia bao lake la mita 20 na ushee akimtungua kipa wa Yanga, Ally Mustafa Barthez katika mchezo wa leo. Simba wameshinda bao 1-0
Beki wa Yanga, Kelvin Yondan kushoto akimbili straika wa Simba, Elias Maguri.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...