Unamkumbuka straika wa Kifaransa na klabu za Liverpool, Marseille,
QPR, Sunderland na nyinginezo nyingi Djibril Cisse? Kwa taarifa yako nguli huyu
hakuwa mkali wa kutishia dunia kisoka, lakini jambo lililomtambulisha zaidi
duniani ni kuwa kinara wa staili za kunyoa.
Cisse alikuwa hatari sana kwa mitindo ya kunyoa na jinsi
alivyopakaa rangi ndevu, nyuso na kila aina kinyweleo.
Sasa na Tanzania tunaye Cisse, Ivo Mapunda, kipa wa Simba
ambaye leo alikuwa kivutio cha aina yake katika mchezo dhidi ya timu yake ya
zamani, Yanga.
Angalia picha zenyewe, kisha mkumbuke Cisse wa Ufaransa.
Ivo Mapunda katikati jinsi alivyotokea katika mchezo wa leo, ndevu na nyuso zake zikiwa zimetapakaa rangi. Ni staili ya aina yake katika soka la Tanzania. |
No comments:
Post a Comment