Sunday, March 8, 2015

LIVE FROM TAIFA: SIMBA VS YANGA

Mpiraaa umekwishaaa
Simba inaondoka na pointi tatu, ukiwa ni mchezo wa kwanza tangu msimu wa 2011/12 kuifunga Yanga katika mchezo wa ligi kuu, achilia mbali kuwa wababe wao kwenye mechi za Nani Mtani Jembe 
Dk 76, Ngassa anatoka nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman kwa upande wa Yanga
Dk ya 75 Elias Maguri anaingia kwa upande wa Simba, anachukua nafasi ya Ajibu 
RED CARD
Dk 74, Niyonzima wa Yanga anatolewa nje kwa kupewa kadi ya pili ya njano, baada ya kupiga mpira baada ya kipyenga, hivyo mwamuzi Saanya kumpa kadi ya pili na kumtoa nje.
 
Goooaaaal Okwiii
Dk 52, Okwi anaipatia bao la kwanza Simba baada ya kuachia fataki la mbali akiwa nje eneo ambalo lilitinga moja kwa moja kwa kutumia uzembe wa kipa Barthez ambaye alikuwa mita chache kutoka langoni hivyo kushindwa kuuwahi golini. Pasi ilitoka kwa Ajibu
MPIRA NI MAPUMZIKO: Simba 0-0 Yanga
Dk 43, Haruna Niyonzima anaonywa kwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Singano karibu na eneo la hatari. Faulo inapigwa na Okwi, almanura afunge, inatoka sentimite kidogo na lango.
Dk ya 36, Yanga wanakosa bao la wazi baada ya kulivagaa lango la Simba lakini kipa Ivo anafanya kazi ya ziada. Msuva na Ngass awanakosa umakini .
Dk 34 Cannavaro anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuzozana na Banda wa Simba. Lakini hakubaliani na kadi hiyo ana maamuzi hayo anataka kumzushia zali mwamuzi, Martin Saanya, lakini wachezaji Yanga wanaingilia na kumtoa. Katika purukushani hiyo, Yondani naye anapigwa njano.
Dk 30, Mrwanda anatolewa bila kuumia, nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu. Pengine ni kutokana na kukosa nafasi ya wazi na kujikutana akinganywa mpira kwenye eneo la hatari la Simba.
Dk 24, Mrwanda wa Yanga na Kessy wa Simba wote wanapigwa njano baada ya kutaka kuzipiga. Mrwanda alifanyiwa madhabi kwa kukwatuliwa na Kessy lakini mwamuzi alipeta, hivyo Mrwanda akamfuata kwa hasira Kessy na kupiga kwa kifua na kuanguka chini
Dk 21, Said Juma wa Yanga anaonywa kwa kadi ya njano, ikiwa ni ya kwanza katika mchezo huo baada ya kumkwatua Ajib.
Dk 

Vikosi: 
 Simba
Ivo Mapunda
Ramadhan Kessy
Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
Juuko Murushid
Hassan Isihaka
Abdi Banda
Ramadhna Singano
Jonas Mkude
Ibrahim Ajib
Said Ndemla
Emmanuel Okwi
Yanga
Ally Mustafa ‘Barthez’
Mbuyu Twite
Oscar Joshua
Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Kelvin Yondani
Said Juma
Simon Msuva
Haruna Niyonzima
Amisi Tambwe
Mrisho Ngassa
Dan Mrwanda/ Hussein Javu dk 30


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...