UNAPOZUN-GUMZIA kati ya wanamuziki wa kike wenye sauti ya aina yake wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva lazima utamtaja msanii kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho Mapenzi’.
Recho anakubalika zaidi kupitia nyimbo zake kama vile Upepo, Kizunguzungu na nyingine nyingi.
Hivi karibuni alitinga ndani ya mjengo wa Global Publishers Ltd na kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja kupitia kipindi kipya cha Me and You With Love kinachoruka hewani kupitia Global TV Online.
Alizungumza mengi kuhusiana na maisha yake nje ya muziki, tiririka naye:
Kwa nini unajiita
Recho Mapenzi?
Recho Mapenzi ni jina nililopewa na mashabiki wangu nikaona siwezi kuwatenga, nikawa nao pamoja kwa kulitumia jina hilo.
Unaelewa nini
kuhusiana na mapenzi?
Kuna mapenzi ya aina nyingi tofauti na tunavyojua sisi kuwa mapenzi ni uhusiano. Siwezi kuzungumzia zaidi kwamba nayajua sana ila naweza kusema mapenzi ni kitu ambacho kipo tu wala hakiwezi kubadilika.
Hadi sasa umeshatoka
na wanaume wangapi?
Siwezi kusema wangapi lakini ninavyojua mwanaume wangu ni mmoja tu ambaye nilikutana naye mwaka 2008, niko naye mpaka sasa. Siyo staa na wala hajihusishi na sanaa ni mfanyabiashara tu.
Mlikutana wapi?
Nakumbuka nilikuwa naelekea studio kurekodi wimbo (Upepo) nikakutana naye, tukabadilishana namba za simu mimi nikachukulia kama urafiki. Nilikaa kama wiki akanipigia simu tukakutana na kuanzia hapo tukawa wapenzi rasmi.
Nani aliyemuanza mwenzake?
Mapenzi ni hisia na unaweza kukutana na mtu leo lakini ukashangaa nyoyo zenu zikakutana. Hilo siwezi kuzungumzia sana lakini kila mtu alivutiwa na mwenzake.
Anakuchukuliaje suala la wewe kufanya muziki?
Wakati nakuwa naye kwenye mapenzi nilikuwa najiandaa kutoka na wimbo wangu wa Upepo. Tangu mwanzo anajua nafanya muziki na hakuweza kuniambia niache kwani aliniambia yeye anafanya biashara zake hivyo kila mmoja asimame kwenye kazi yake.
Unamuamini
asilimia ngapi?
Namuamini kwa asilimia zote na tangu mwaka 2008 sijawahi wala sijawaza kumsaliti hata siku moja. Labda yeye anafanya kwa siri lakini sijawahi kusikia wala kuona akinisaliti.
Anapokasirika
huwa unamfanyaje?
Nikishagundua amerudi amekasirika huwa napenda kucheza wimbo wowote ili anione ninavyocheza lakini kama bado atakuwa ana hasira huwa namuimbia wimbo wangu wa Upepo ambao anaupenda sana hadi anarudi katika hali yake ya kawaida.
Kuna tetesi kuwa unapenda ngozi nyeupe ‘Wazungu’ ni kweli?
Sijawahi kufikiria kutembea na ngozi nyeupe ninaweza kusema napenda sana kusikiliza nyimbo zao hasa za Waarabu na Wahindi.
Kuonesha kuwa nawapenda kimuziki tu hata mpenzi niliyekuwa naye sasa siyo wa asili hiyo, ni Mbongo kabisa. Recho ameongea mengi kuhusiana na maisha yake nje ya muziki, ili kuyapata mahojiano kamili tembelea www.globaltvtz.com
No comments:
Post a Comment