Haya ni madai mazito! Mama mzaa chema wa staa wa sinema za Kibongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu anadaiwa kumzaba vibao askari
wa kampuni binafsi.
UJIUNGE NA SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda huyo,
tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilijiri kwenye Bandari ya Dar
es Salaam, majira ya mchana Ijumaa iliyopita.Kabla ya kushusha stori
kamili, Ijumaa Wikienda lilimhoji shuhuda huyo kama anamjua vizuri mama
Wema ambapo alithibitisha kuwa ni yeye huku akisapotiwa na wenzake
waliokuwa wakisikika kwenye simu.
KUMBE ALIFUATANA NA WEMA
“Nani asiyemjua mama wa
staa mkubwa kama Wema? Tena kafuatana na Wema mwenyewe. Kila mtu hapa
anamjua ngoja tujaribu kupata picha zake nzuri,” alisema shuhuda huyo
kwa kujiamini.
Shuhuda huyo alidai kwamba chanzo cha yote, mama Wema
alidaiwa kutumia mlango usio sahihi na alipofuatwa kuelekezwa ndipo
likaibuka timbwili zito.
ALIKUWA ANATOKEA WAPI?
“Kinachoonekana alikuwa
ameshuka kwenye boti akitokea Zanzibar kwenye shughuli binafsi. Wakati
anatoka kuchukua hamsini zake akiwa na Wema, wakapita mlango ambao siyo
sahihi.
“Sasa askari wa kampuni binafsi akawafuata na kuwazuia ili
kuwapa maelekezo lakini mama Wema alikasirika, akaanza kumpiga vibao.
“Hapo ndipo lilipoibuka timbwili zito kwani askari naye hakutaka kukubali kirahisi.
“Naye mama Wema kuonesha si mtu wa mchezo aligeuka mbogo na kusababisha watu kushindwa kuamini.
MAMA WEMA KAPITIA JESHINI?
“Yaani swali kubwa
kila mtu alikuwa anahoji kama mama Wema amepitia jeshini kwa jinsi
alivyoonekana ngangari.“Kiukweli yule mama siyo wa kumchezea anaonekana
yupo vizuri kimazoezi.
WAMALIZANA POLISI
“Baadaye walipelekana kwenye
kituo cha polisi cha pale bandarini wakamalizana lakini tayari ishu hiyo
ilishageuka gumzo maeneo hayo.“Hatujui walikubaliana nini zaidi ya
kuwaona wakitimua zao kwani hawakutaka kukusanya tena watu,” alidai
shuhuda wetu huyo.
MAMA WEMA AOMBA APUMZIKE
Baada ya kumwagiwa
tukio hilo la moto, gazeti hili lilimtafuta mama Wema ambaye hakukanusha
kutokea kwa tukio hilo badala yake aliomba aachwe kwanza apumzike
nyumbani kwake, Sinza-Mori jijini Dar.
“Niache nipumzike kwanza
nitakusimulia tukio,” alisema mama Wema.Alipotafutwa kwa mara nyingine
hakuwa tayari kutoa ushirikiano hivyo jitihada za kusikia upande wake
zinaendelea.
WEMA VIPI?
Kwa upande wake Wema, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa ikielezwa kwamba alikuwa amebanwa na majukumu.
No comments:
Post a Comment